Papa Luciani,kutoka utumiaji wa manati hadi kwenye Kiti cha Petro!
Vatican News
“Kutumia manati” ulikuwa ule wa Padre Remigio, Ndugu Mkapuchini ambaye alikuja kwa ajili ya utume huko Canale ya Agordo wakati Albino Luciani ambaye atakuwa ni papa wa baadaye na ambaye atatangazwa kuwa Mwenyeheri mnamo tarehe 4 Septemba ijayo, alikuwa bado mvulana mdogo. Aliwavutia vijana wenzake wadogo wa kijijini waliokuwa wanatumikia altareni kwa historia zake na baadaye wakati wa kutembea kuelekea Kanisa dogo la Garés, aliwashangaza kwa uwezo wake wa kutumia Manati. Na walipowauliza wale wavulana ni wakina nani walitaka kuingia kwenye nyumba ya watawa, Albino mara moja alisema: "Mimi, mimi!". Alitamani sana kuondoka. Paroko na familia walimzuia... Ni moja ya historia zilizomo katika podikasti ya Radio Vatican katika vipindi vinne, vilivyotolewa kwa ajili ya Papa Luciani, vilivyosimuliwa na Dk. Andrea Tornielli, Mkurugenzi wa uhariri wa vyombo vya habari vya Vatican, na kutayarishwa kwa ushirikiano wa kiufundi na ubunifu na Adriano Vitali na Patrizio Ciprari. Kipindi cha kwanza kinaweza kusikilizwa siku ya Jumatatu tarehe 6 Juni 2022, katika sehemu ya podikasti ya tovuti ya Vatican News: (https://www.vaticannews.va/it/podcast/radio-vaticana.html)
Podikasti kuhusu Papa Luciani
Kipindi cha ufunguzi kitahusu asili ya Papa kutoka Belluno, familia yake na elimu yake. Albino Luciani anadaiwa jina lake la ubatizo kuchaguliwa na baba yake Giovanni, aliyekuwa mfanyakazi wa kisoshalisti, ambaye alichagua kumtaja mtoto wake mkubwa kwa njia hii katika kumbukumbu ya rafiki yake wa Bergamo ambaye alikufa katika ajali kazini katika tanuru ya mlipuko. Katika sehemu ya pili, ambayo inaweza kusikilizwa kuanzia Jumatatu tarehe 13 Juni, tutazungumza kuhusu kuteuliwa kwa Luciani kuwa askofu wa Vittorio Veneto na kisha kuhusu miaka iliyotumia akiwa katika huduma huko Venezia. Pia katika kesi hii, itakuwa sauti ya Papa mwenyewe kusisitizia vifungu muhimu. Shukrani kwa waraka wa kipekee wa sauti, uliorekodiwa katika parokia mnamo mwaka wa 1968, ambapo tutasikia kutoka kwa sauti ya Askofu Luciani, matumaini yake kwamba Paulo VI angeweza kufanya uamuzi huria kuhusu matumizi ya tembe za kuzuia mimba. Baada ya kuchapishwa kwa waraka wa Humanae vitae, Luciani atatetea waraka huo na kuzifanya sababu za Papa kuwa zake.
"Wiki tano, upapa" ni jina la kipindi cha tatu, kitakachopatikana kuanzia Jumatatu tarehe 20 Juni 2022, ambacho kitasimulia mkutano wa mnamo Agosti 1978, wa uchaguzi wa haraka baada ya siku moja tu ya kupiga kura na siku hizo 34 za upapa. Tutasikiliza vifungu muhimu vya Katekesi na sala ya Malaika wa Bwana ya Yohane Paulo wa I, vingine muhimu vinavyogusa moyo sana, kama vile ambavyo Papa anasimulia kuwa aliteseka na njaa akiwa mtoto, akitumaini kwamba uzoefu huo utamsaidia kuelewa matatizo ya maskini wa ulimwengu. Hatimaye, sehemu ya nne, itayopatikana kuanzia Jumatatu tarehe 27 Juni 2022, itakuwa inajitoa kikamilifu kwa kifo cha ghafla cha Papa. Cha msingi itakuwa sauti ya Sista Margherita Marin ambaye asubuhi hiyo ya tarehe 29 Septemba 1978, pamoja na sista mwenzake mzee Vincenza, aliingia chumbani kwa Papa Luciani na kumkuta amefariki. Sisite Margherita, ataeleza maelezo mengi ya maisha ya kila siku ya Papa Yohane Paulo I, akifafanua kwa upya zile saa zake za mwisho wa maisha.
Kipindi cha 1 Jumatatu 6 Juni
Jina la ubatizo kwa ajili ya kukumbuka kijana aliyekufa katika ajali kazini
Kipindi cha 2 Jumatatu tarehe 13 Juni
Askofu wa karibu na maskini na matumaini yake ya "neno huria" juu ya udhibiti wa uzazi
Kipindi cha 3 Jumatatu tarehe 20 Juni
Wiki tano, upapa: lugha rahisi ambayo kila mtu alielewa
Kipindi cha 4 Jumatatu 27 Juni
Kifo cha ghafla: saa za mwisho za Papa zinazosimuliwa na mmoja wa watawa waliokuwa wakiishi naye.