Papa:Msisahau kamwe watu wa Siria na Wakristo wa Mashariki ya Kati
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa Sinodi ya Kanisa la Kigiriki-Melkiti Katoliki, Jumatatu tarehe 20 Juni 2022. Amefurahi kukutana nao wakia katika mwanzo wa Kazi ya Sinodi ya Maaskofu wa Upatriaki huo wa Antiokia na kumshukuru Mkuu wa Kanisa la Upatriaki Youssef Absi, kwa maneno yake aliyomwolekea. Majanga ya ya miezi ya mwisho, ambayo kwa huzuni mkubwa amesema yametulazimisha kuelekeza mtazamo kwa Ulaya Mashariki, yasitufanye kusahau kile cha miaka kumi na mbili iliyopita katika nchi yao, mamia elfu ya vifo na majeruhi, mamilioni ya Wakimbizi wa ndani na Nje, ukosefu wa kuanzisha ukarabati na ujenzi mpya. Papa Francisko amekumbuka mwaka wa kwanza wa upapa wake wakati kulikuwa na uandaaji wa kulipua mabomu nchini Siria na kwamba walisali usiku katika uwanja wa Mtakatifu Petro na kulikuwa na Sakramenti Takatifu, katika uwanja ukiwa umejaa watu wakisali. Kulikuwa hata na waislamu ambao walikuwa wamebeba majanvi yao wakisali pamoja na wakristo na tangu wakati huo ulizaliwa kielelezo cha Nchi pendwa na inayoteseka ya Siria.”
Na zaidi katika fursa imejitokeza kukutana na kusikia simulizi ya baadhi ya vijana wa Siria waliofika Italia na kwamba ilimshangaza sana majanga wanayobeba ndani mwao, kwa yale yote ambayo wameishi, na kuona lakini kwa mtazamo unaolekea kukauka kwa matumaini, kutokuwa na ndoto ya wakati ujao wa nchi yao. Baba Mtakatifu Francisko amesema, hatuwezi kuruhusu hata cheche moja ya tumaini ambalo limeendolewa katika mtazamo wao na mioyo ya vijana na familia. Papa kwa maana hiyo ametoa wito kwa wale wanahusika, ndani ya Nchi na katika Jumuiya ya Kimataifa, ili iweze kufikia suluhisho la haki na sawa katika janga la Siria. Baba Mtakatifu Francisko aidha amebainisha jinsi ambavyo Maaskofu wa Kanisa la Kigiriki, Melkiti wanaalikwa kujiuliza jinsi gani Kanisa linaweza kupeleke mbele ushuhuda, wa kishujaa, ukarimu lakini daima wenye kuhitaji kuwa chini ya mwanga wa Mungu ambaye anatakasa na kupyaisha. Ecclesia semper reformanda. Wao ni Sinodi kwa ile inayotambuliwa kama Kanisa la Upatriaki na ni lazima kwamba wajiulize juu ya mtindo gani wa Sinodi yao ilivyo na kutenda, kwa mujibu wa kile alichokiomba kwa Kanisa la ulimwenguni kuwa na uwezo wao wa kuishi muungano wa salama na maelewano kati yao na Patriaki, kati ya Maaskofu na Makuhani na mashemasi, na Watawa kike na kiume, waamini walei na wote kwa pamoja kuunda Watu wamoja watakatifu wa Mungu.
Kiukweli kama maaskofu wana wasi wasi wa kuishi kwa Wakristo wa nchi za Mashariki, ambao kwa hakika wanashirikishana; na kwa upande mwingine kwa makumi ya miaka sasa ya uwepo wa Kanisa la Kimelkiti kufikia ulimwenguni, kwa sababu tayari upartiaki wake upo Australia, Marekani, Canada, Venezuela na Argentina, kwa kutaja baadhi badhi. Na wengi wapo waamini hata Ulaya hata kama wengine bado hawajawa na uwezekano wa kuungana katika muktadha wa Kanisa lao binafsi. Katika mantiki hiyo inawakilisha bila shaka changamoto, kikanisa lakini pia kiutamaduni na kijamii, bila kukosa matatizo na vizingiti. Na wakati huo huo hata fursa kubwa ile ya kubaki wamesimikwa mizizi katika tamaduni zao na asili kwa kufungulia usikivu wa nyakati na mahali ambamo wamepandwa, ili kujibu kile ambacho Bwana anawataka leo hii. Ndani ya Sinodi, Papa Francisko amewatia moyo kutumia umahiri wao kwa hekima kubwa: Anajua kwamba tafakari imeanza katika baadhi ya Makanisa ya Mashariki kuhusu nafasi na uwepo wa Maaskofu waliostaafu, hasa wale wenye umri wa zaidi ya miaka themanini, ambao katika baadhi ya Sinodi ni idadi thabiti. Sura nyingine ni ile ya chaguzi za Maaskofu, ambayo amewaomba watafakari vizuri kila wakati na kumwomba Roho Mtakatifu awaangazie, akitayarisha vya kutosha na mapema nyenzo na taarifa za wagombea mbalimbali, kushinda mantiki yoyote ya ushabiki na ulinganifu kati ya taratibu za dini asili.
Papa Francisko aidha amewasihi na kuwashukuru kwa jitihada ambayo wataiweka katika hilo ili kufanya uso wa Kanisa ling'ae, ambalo Kristo alilipata kwa Damu yake, akiweka mbali migawanyiko na manung'uniko, ambayo hayafanyi chochote isipokuwa kuwachukiza wadogo na kuwatawanya kundi lililokabidhiwa kwao. Katika hilo Papa Francisko amependa kusimama kidogo na kutoa onyo kwamba wajihadhali na masengenyo. Ikiwa mmoja ana jambo la kumwambia mwenzake, amwambie usoni, kwa upendo, kama watu. Waweza kumwambia kaiwa peke yake , au kumwambia moja kwa moja mbele ya wengine, masahahisho ya kidugu. Lakini usiseme uvumi juu ya mwingine na mwingine nyuma yake hii haifanyiki. Kwa sababu huyo ni nondo mdudu anayeharibu Kanisa. Lazima wawe wajasiri na watazame jinsi Paulo alivykuwa anasema mambo mengi uso kwa uso wa James. Pia hata kwa Petro. Na baadaye wanafanyika umoja, umoja wa kweli, kati ya watu. Papa amewaomba kufukiza mbali kila aina ya mateto. Na kwa sababu watu wanatoa kashfa kkwa watu wasemao tazameni makuhani, maaskofu wanavyo gombana kati yao, kwa hiyo wanachotakiwa kusema ni vuzri kuambizana uso kwa uso daima. Amehitimisha kwa kuwabariki sughuli yao na Bikira Maria Mama wa Kanisa anawasindikize.