Papa:Upendo wa familia ni wito na njia ya utakatifu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko Dominika 19 Juni 2022 amewakumbusha Wakatoliki wota kwamba Mkutano wa Kumi wa Familia wa Ulimwengu (#WMOF22) utaanza mjini Roma mnamo Jumatano, tarehe 22 Juni. WMOF ni kifupi cha Mkutano wa Familia wa Ulimwengu, ulioanzisha na Papa Braza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, mada inayoongoza ya mwaka huu ni “Upendo wa Familia: Wito na Njia ya Utakatifu”.
Kila jimbo linaadhimisha siku ya familia na maaskofu wake
Badala ya mkutano wa hadhara duniani kote mwaka huu, imeamuliwa kuwa tukio hilo liadhimishwe katika kila majimbo yote pamoja na maaskofu wa mahalia, kwa uzoefu maalum, wa ndani wa malezi, maombi na ushirika. Hata hivyo, wajumbe kutoka ulimwenguni kote watakuwepo kuanzia tarehe 22 hadi 26 Juni 2022 katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican ambao watakuwa ni wakiwakilishi wa familia za Kikatoliki duniani kote.
Kongamano, mkesha na tamasha
Kwa kuzingatia mapokeo, programu inajumuisha Kongamano la Kimataifa la Kitaalimungu-Kichungaji mwanzoni na mwisho mwa mkutano huo, mbele ya Papa Francisko, pamoja na mkesha na Tamasha la Familia litakalofuatiwa na adhimisho kuu la mwisho la Ekaristi takatifu inayotarajiwa.
Mkutano mwaka huu unatofautiana na mikutano mingine ya kiutamaduni
Akizungumza mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Dominika 19 Juni, kwa maana hiyo Papa Francisko amebainisha kuwa Mkutano huo utafanyika mjini Roma na wakati huohuo duniani kote. Na amewashukuru maaskofu, mapadre wa parokia na wachungaji wa familia ambao wameita familia katika nyakati za kutafakari, kusherehekea na sikukuu. Papa amesema:
“Zaidi ya yote, ninawashukuru wanandoa na familia ambao watatoa ushuhuda wa upendo wa familia kama wito na njia ya utakatifu. Muwe na mkutano mwema!