2022.06.09 Dk Dani Dayan, Rais wa Yad Vashem 2022.06.09 Dk Dani Dayan, Rais wa Yad Vashem 

Rais wa Yad Vashem:Papa ni mshirika katika vita dhidi ya chuki kwa Wayahudi

Baba Mtakatifu Francisko alikutana na Dani Dayan,rais wa Yad Vashem,Kituo cha Kumbukumbu ya Maangamizi ya Kidunia huko Yerusalemu na kusisitiza dhamira yake ya kuchangia katika mapambano dhidi ya aina zote za chuki,uadui au chuki dhidi ya Wayahudi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Alhamisi tarehe 9 Juni 2022 Dk. Dani Dayan likutana na Papa Francisko ambapo amesema mkutano wao ni hatua nyingine mbele katika mapambano dhidi ya chuki dhidi ya Wayahudi. Dayan alisema hayo akizungumza na Vatican Radio/Vatican News mara baada ya kukutana na Papa Francisko mjini Vatican. Rais wa Yad Vashem amemtaja Papa kuwa ni rafiki na mshirika katika utume wa  kushinda chuki dhidi ya Wayahudi. Yad Vashem, ambacho ni Kituo cha Ukumbusho cha Maangamizi ya Ulimwengu chenye makao yake makuu mjini Yerusalem, kinatambulika ulimwenguni kote kama chanzo kikuu cha elimu, kumbukumbu na utafiti kuhusu mauaji ya  Kimbari ya Wayahudi.

Rais wa Yad Vashem Dan Dayan alikutana na Papa
Rais wa Yad Vashem Dan Dayan alikutana na Papa

Papa Franciko alikitembelea mwaka 2014 wakati wa ziara yake katika Nchi Takatifu. Katika hotuba iliyotolewa hapo, Papa alimwomba  Bwana alete neema ya kuaibishwa kwa yale ambayo  kama wanadamu, yameweza kufanya, na akapaza sauti kuwa jambo hilo lisirudiwe tena. Aidha akibainisha kuwa alikuwa rais wa kwanza wa Yad Vashem kupokelewa na Papa Francisko, Dayan alifichua kwamba wote wawili ni wenyeji wa Buenos Aires na alifurahi kuweza kuzungumza katika lugha yao ya asili, Kihispania. Rais wa Kituo alimshukuru Papa kwa kufungua kumbukumbu za Vatican juu ya Papa wa Pio XII (1939-1958).

Rais wa Yad Vashem Dan Dayan alikutana na Papa
Rais wa Yad Vashem Dan Dayan alikutana na Papa

Kiukweli, mnamo Machi 2020, Pango la Kitume la Vatican pamoja na kumbukumbu nyingine kadhaa za Vatican, zilifunguliwa kwa mashauriano na wasomi. “Nilipomshukuru kwa kuamua kufungua kumbukumbu za Vatican za kipindi husika cha Mauaji ya Kimbari kwa watafiti wetu Papa alisema kwa uamuzi sana: 'hii ni kutenda haki, kufungua kumbukumbu kwa utafiti kunamaanisha kutenda haki'. . Papa alirudia kile alichokwisha kusema mara moja: “Kanisa haliogopi, ikiwa halipendi historia”. Aliongeza kuwa anafahamu vyema kwamba, kama ilivyo katika jamii nyingine zote, katika Kanisa katika kipindi hicho cha kutisha cha ubinadamu kulikuwa na wale ambao walitenda kwa usahihi na wale ambao hawakufanya usahihi huo” alisema Dk.  Dayan.

Rais wa Yad Vashem Dan Dayan katika Studio za Vatican
Rais wa Yad Vashem Dan Dayan katika Studio za Vatican

Akiendelea na ufafanuzi huo katika mahojiano Dk Dayan, rais wa Kituo hicho amesema,  Papa Francisko yuko wazi sana kukemea janga la chuki dhidi ya Wayahudi na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kupambana nalo ili kulishinda. “Kwa Yad Vashem, ambayo imejitolea kwa kumbukumbu ya Wayahudi milioni 6 waliouawa na Ujerumani ya Kinazi na washirika wake, huu ni wakati wa kihistoria. Ni mara ya kwanza kwa Papa kumpokea rais wa Yad Vashem katika hadhara ya faragha na ninaamini kwamba hii inadhihirisha kwa ulimwengu umuhimu ambao Papa Francisko, kama mkuu wa Kanisa Katoliki, anahuisha kumbukumbu ya Mauaji kwa ajili ya mapambano dhidi ya chuki dhidi ya Wayahudi. Mwishoni mwa mkutano huo  Dani Dayan alisema alimpatia Papa  Francisko zawadi na kwamba Papa alikuwa mwema wa kumpatia  pia, akisema: “Usisahau kuwa una rafiki hapa”.

10 June 2022, 16:44