Shirika la Malta:Papa atuma salamu za rambirambi kufuatia na kifo cha Luzzago
Vatican News.
Baba Mtakatifu Francisko ameelezea ukaribu wake wote kwa Mkuu wa Shirika la Kijeshi la Malta waliokumbwa na maombolezo ya kifo cha Luteni Mwalimu Mkuu, Ndugu Marco Luzzago. Katika telegram aliyoituma kwa Kardinali Silvano Maria Tomasi, mwakilishi wa Papa kwa ajili ya Shirika hilo, Baba Mtakatifu amesema “anahusika kiroho katika machungu ya kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Ndugu Marco Luzzago, Luteni Mwalimu Mkuu”.
“Ninapenda kutoa salamu zangu za rambirambi kwa wanafamilia na Shirika zima Mtakatifu na kwa kukumbusha kujitoa kwa ukarimu aliokuwa nao katika kutekeleza wadhifa wake wa juu katika huduma ya taasisi hiyo, pamoja na upendo wake kwa Kanisa na shuhuda wa Kikristo, ninamwombea Amani ya Milele na kwa moyo mkunjufu ninatoa baraka zangu kwako, Kardinali, kwa Luteni wa muda, Ndugu 'Ruy Gonçalo do Valle Peixoto, Baraza Kuu la Majisterio na kwa wanachama wote wa Shirika Kuu la Kijeshi la Malta”, amehitimisha Baba Mtakatifu Francisko.