Uchungu wa Papa kufuatia na mauaji katika kanisa katoliki nchini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Pentekoste ya umwagaji damu nchini Nigeria, ambapo watu waliokuwa na bunduki waliwafyatulia risasi waamini ndani ya Kanisa katoliki Kusini Magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu kadhaa wakiwemo watoto wengi waliokuwa wakisherehekea Sherehe hiyo, Dominika tarehe 5 Juni 2022. Kulingana tarifa za awali, makomando hao pia walitumia vilipuzi mwishoni mwa Misa. Shambulio hilo lilitokea katika Kanisa la Mtakatifu Francis Xaveri, huko Owo, katika jimbo la Ondo, mojawapo ya makanisa yenye amani zaidi nchini humo hadi sasa.
Salamu za rambirambi za Papa
Papa pia alijiunga na maumivu hayo ya jumla, wakati maelezo ya tukio yanafafanuliwa, kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican. “Papa Francisko anawaombea waathirika na nchi, iliyoathiriwa kwa uchungu wakati wa kusherehekea, na anawakabidhi wote kwa Bwana, na kutuma Roho wake kuwafariji", ameripoti msemaji wa Vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni.
Zaidi ya waathirika 40, hofu kwa waliojeruhiwa
Kulingana na vyanzo vya ndani, waathiriwa ni zaidi ya arobaini. Hofu iliyopo sasa ni kwa majeruhi hao ambao hata walipookolewa mara moja na kupelekwa hospitalini, wana hatari ya kutoweza kunusurika kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata, ukizingatia pia uhaba wa njia za matibabu. Madaktari wa eneo hilo, waliotajwa na mashirika ya kimataifa, wanaripoti kwamba watu wengi tayari wamefika hospitalini wakiwa hawana maisha. Katika masaa yale pia kuna maombi ya kuchangia damu, hasa kupitia mitandao ya kijamii.
Maaskofu wameomba utulivu
Katika mshtuko huo kwa ujumla, hofu ni kwamba kuna wengi zaidi waliokufa, wengi zaidi wamejeruhiwa na kwamba Kanisa limekiukwa, kwa mujibu wa taarifa yake Padre Augustine Ikwu, mkurugenzi wa mawasiliano ya kijamii wa Jimbo la Ondo, ambaye alikanusha habari zilizosambazwa katika dakika za kwanza za kutekwa nyara kwa baadhi ya waamini, akiwemo padre wa parokia hiyo. Kwa mujibu wake alisema Mapadre wako salama. Hata askofu wa jimbo hilo, Jude Ayodeji Arogundade, kwamba yupo pamoja nao katika wakati huu mgumu. Katika nyakati hizi za kutisha, askofu mwenyewe anaomba kuwa na watulivu, kuheshimu sheria na kuombea amani na hali ya kawaida irudi katika jamii na nchini kote.
Katika maombi kwa ajili ya wahanga na familia zao
Wahusika bado hawajajulikana ni nani, huku hali hiyo ikiwa imeiacha jamii katika simanzi kubwa. Hata hivyo, kwa sasa vyombo vya usalama vimetumwa katika jumuiya hiyo ili kudhibiti hali hiyo, kwa mujibu wa Padre Ikwu. Kwa hiyo anaomba ni kuingilia kati kwa Mungu ili kurejesha amani na utulivu:"Tunamgeukia Mungu kuzifariji familia za waliopoteza maisha katika shambulio hili baya na tunaziombea roho za marehemu zipumzike kwa amani."
Rais amelaani kitendo hicho
Wakati huo huo, aliyelaani shambulio ni Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji huyo, Buhari alisema kuwa washambuliaji wanatarajiwa kupata maumivu ya milele duniani na kesho mbele ya Mungu. Akitoa salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na Kanisa Katoliki, mkuu huyo wa nchi aliagiza vyombo vya dharura kuchukua hatua na kutoa misaada kwa waliojeruhiwa. "Nchi hii haitasalimu amri kwa uovu na waovu, na giza halitashinda nuru", kwa mujibu wa taarifa ya rais.
Waathiriwa wa unyanyasaji usiowezekana
Kilichotokea leo Nigeria kina mizizi ya mbali. Kwa takriban miaka 20, makundi yenye itikadi kali na ya kigaidi yamefanya mashambulizi dhidi ya Wakristo na Waislamu wenye msimamo wa wastani.