Papa asikitishwa na mauaji huko Chicago:maisha yaheshimiwe!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ukaribu wa kiroho na sala kwa wale waliohusika katika ufyatuaji wa risasi isiyo na maana iliyofanyika tarehe 4 Julai 2022 huko Chicago kwenye Uwanja wa Highland (U.S.A.). Ni hisia ya kiroho ya Baba Mtakatifu Francisko katika telegramu iliyotiwa saini na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin na kutumwa kwa Kardinali Blase Cupich, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Chicago. Papa Fransisko anaungana na jumuiya nzima kumwomba Mwenyezi Mungu awape pumziko la milele marehemu na uponyaji na faraja kwa majeruhi na wale wanaoomboleza. Kutoka juu ya paa la jengo alikuwa ni kijana ambaye alifyatua risasi kwa umati wa watu walioshiriki kwenye gwaride mnamo tarehe 4 Julai 4 2022 katika Siku ya Uhuru Marekani na kusababisha vya watu saba na zaidi ya watu 30 kujeruhiwa.
Hapana kwa kifo na ndiyo kwa uzima katika aina zake zote
Katika maneno ya Papa Francisko anapyaisha imani isiyotikisika na kwamba neema ya Mungu inaweza kugeuza hata mioyo migumu na kuifanya iwezekane, kama Zaburi ya (34, 14) inavyosema, kujiepusha na ubaya na kutenda mema. Papa Francisko anaomba kwamba kila mwanajamii akatae vurugu katika aina zake zote na aheshimu maisha katika kila hatua. Salamu ghizo zinahitimishwa kwa baraka zake.
Kipindi kipya cha unyanyasaji wa kipofu kiliikumba Marekani wiki chache baada ya mauaji ya Uvalde mnamo tarehe 24 Mei ambapo watu 22 walikufa katika shule ya msingi na mauaji katika duka kubwa huko Buffalo, jijini New York. Rais Joe Biden, ambaye alisema alikuwa katika mshtuko, alizungumza na nchi hiyo na mkewe Jill kutokea bustani ya Ikulu na kuahidi kwamba mapambano dhidi ya janga la utumiaji silaha yataendelea. Hivi karibuni Biden alitia saini sheria (pia iliyopigiwa kura katika Bunge na baadhi ya Wabunge wa Republican) ambayo inalenga kuanzisha udhibiti mkubwa zaidi wa biashara ya silaha. Ingawa si kitu rahisi kwa sababu ni hatua ya kwanza kuletwa nchini Marekani tangu 1994.
Hata hivyo mshukiwa huyo wa shambulio baya kwenye gwaride la Siku ya Uhuru katika kitongoji cha Chicago ameshtakiwa kwa makosa saba ya mauaji katika shambulio la risasi lililosababisha vifo vya watu saba na zaidi ya 30 kujeruhiwa. Wakili wa Jimbo la Ziwa Eric Rinehart alisema kwamba ikiwa atapatikana na hatia, Robert Crimo III atakabiliwa na kifungo cha maisha cha lazima bila msamaha. Wachunguzi, ambao wamemhoji mshukiwa na kukagua machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii, hawajabaini sababu ya shambulio hilo, msemaji wa Kikosi Maalum cha Uhalifu katika Kaunti ya Ziwa Christopher Covelli aliambia mkutano wa wanahabari. Covelli alisema Crimo alinunua kihalali silaha tano, zikiwemo bunduki mbili zenye uwezo mkubwa, moja ambayo ilipatikana katika eneo la tukio na ya pili kwenye gari lake, Covelli alisema. Katika mkutano wa wanahabari Jumanne jioni, polisi walifichua kwamba walikuwa wameitwa nyumbani kwa Crimo mara mbili mnamo Septemba 2019, baada ya kutoa vitisho vya vurugu na kujiua. Polisi walinyakua visu kadhaa, jambia na panga lakini wakasema hapakuwa na dalili yoyote ya bunduki.