2022.07.06 Padre Guillermo Marcó na  Papa Francisko. 2022.07.06 Padre Guillermo Marcó na Papa Francisko. 

Papa:Moyo wangu uko tayari kwa wema wanaonipatia watu

Katika podcast iliyondaliwa na Guillermo Marcó wa Argentina,ambaye alikuwa mkuu wa ofisi ya waandishi wa habari ya jimbo kuu la Buenos Aires kwa miaka 10,wakati wake Kardinali Bergoglio(Papa Francisko)kuna baadhi ya maswali na majibu,kuanzia anavyosali hadi kufikia jinsi anavyopitia uzee.“Ninajicheka mwenyewe na ninaendelea mbele”,ameeleza Papa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Moyo wangu ni amana, umejaa vitu ambavyo ninavihifadhi. Lazima niendelee kupanua makabati. Katika hilo mimi ni nusu mkusanyaji, kwa maana nzuri ya neno, sitaki kupoteza mambo yoyote mazuri ambayo watu hunipatia. Watu wanakufurahisha sana, kwa mifano, kwa maneno na kwa vitendo. Kuhani ana kazi ya kufundisha watu, lakini ninaamini tunaweza kujifunza mengi kutoka kwa watu ikiwa tutasimama na kuwatazama. Ndivyo yanaanza mahojiano ambayo Papa Francisko alitoa kwa padre mmoja wa Argentina Guillermo Marcó. Padre  hapo awali aliwahi kuwa mkuu wa ofisi ya waandishi wa habari wa jimbo kuu la porteña nchini Argentina  wakati  Bergoglio yaani Papa Francisko akiwa Kardinali. Ni dakika ishirini na mbili za mazungumzo, ambayo yalichukua saa moja na nusu kwa jumla yaliyofanyika tarehe 9 Juni iliyopita, na kuchapishwa Dominika  tarehe 3 Julai  2022 katika podikasti ya kila wiki  ya Padre  Marcó.

Mazungumzo kuhusu maisha binafsi ya Papa

Mazungumzo yalijikita katika masuala binafsi ya maisha ya Papa,  na maisha yake ya sasa. “Niliona mambo ambayo wakati mwingine yanaonekana katika vyombo vingine vya habari wakati anafanya mahojiano na mwandishi wa habari”.  Padre Marcó alieleza katika uwasilishaji wa podikasti yake, akisisitiza kwamba alikuwa amezungumzia na  Papa mwenyewe. Kuhani huyo alipendelea kuuliza maswali yanayohusu mada ya maisha ambayo alieleza kwamba yeye hufanya kwa sababu kadiri unavyouliza maswali ndivyo unajua mtu anavyoishi. Mara nyingi Papa alikuwa akisema kwamba anapokabiliana na tatizo kwanza kabisa anataka atulie  aombe kwanza, alafu atoe jibu na hivyo kuhusiana na swali la sala Papa alisema kwamba sala ya askofu ni kuchunga kundi, kuliweka katika maneno ya kiinjili, na Papa ni askofu hivyo anatabia hiyo ya kuomba, kushukuru kwa mema yote yanayotendeka. Na kuhusu suala la kuamka kusali mapema, Papa alijibu, ‘ndiyo’ kwa sababu asipoomba asubuhi , hataombi tena, kwa sababu ni kuishia kwenye shughuli nyingi.

Kuzunguka mitaani, kumbu kumbu ya maisha huko Buenos Aires

Hata hivyo kile ambacho Mfuasi wa Petro  anakosa mji mkuu wa Argentina ni ule uwezo wa kuzunguka  kwa uhuru mitaani. Kwa sababu amesema huko Buenos Aires alizunguka kwa miguu au kwa basi; lakini hapa Roma  mara mbili alizofanya kutoka nje, tayari walimwona kwa haraka na ilikuwa mara mbili kipindi cha baridi. Saa 1 jioni, wakati hakuna kinachotokea na giza lote. Alikumbusha siku aliyokwenda kwa daktari wa macho, mwanamke kutoka kwenye balcony (alipiga kelele): 'Papa! Na baadaye alipokwenda kwenye duka la kuuza diski za muziki hapakuwapo na watu na alikwenda kubariki kwa sababu ilikuwa duka la kumbukumbu la marafiki ambapo walikuwa wameikarabati na kuombwa kwenda. Lakinimara tu baada ya kutoka nje kulikuwa na mwandishi wa habari ambaye alikuwa hapo bila kujua akisubiri rafiki kumchukua na Taxi  na huyo tayari akasambaza habari.

Unajisikiaje mbele ya wajibu mkubwa wa Kanisa?

Kuhusu hali yake kiakili mbele ya utume wake mkuu wa Kanisa, Papa alisema kwamba RohoMtakatifu anatoa matunda mengi, lakini haisemwi kamwe kwamba anakugandishwa na wakati mwingine, huhisi kupigwa butwaa mbele ya hali ambazo zinaweza kukufanya uteseke sana na kwa maana hiyo anazikabidh ili aweze kuendelea mbele.

Mahali penye shida, tunakua

Mada nyingine iliyojadiliwa katika mahojiano hayo ilikuwa ni usimamizi wa mgogoro: ambapo Papa alisema ni moja ya mambo aliyojifunza hapo kwamba hatujui jinsi ya kudhibiti migogoro na mizozo na ndiyo inayotufanya kukua. Baadaye Papa Francisko akiwakumbuka na kunukuu waanzilishi wa Umoja wa Ulaya kama mifano ya wanaume ambao walijua jinsi ya kusimamia migogoro na ambao walikua pamoja na migogoro, alisema haikuwageuza kuwa migogoro, (kutofautisha kati ya) nyeupe au nyeusi. Kwa sababu unapogeuza mgogoro kuwa mzozo, umeshindwa. Umoja ni nguvu kuliko migogoro, yaani migogoro inakupunguza.

Ushuhuda wa mtu mzee

Hatimaye, akichukua dokezo kutokana na  mzunguko wa katekesi kwa wazee, ambao Askofu wa Roma alianza  mnamo tarehe 23 Februari mwaka huu wakati Padre Marcó alitaka kujua jinsi  gani Papa anavyoikabili hatua hii ya maisha yake na akajibu kwamba  “Mimi, katika umri wangu , najicheka na kuendelea ”.

07 July 2022, 15:35