2022.08.25 Papa Yohane Paulo I aliwahi kuwa askofu wa Vittorio Veneto Italia  2022.08.25 Papa Yohane Paulo I aliwahi kuwa askofu wa Vittorio Veneto Italia  

Luciani,mahubiri kuhusu kuhani “mtumishi anayehusika na watu”

Katika fursa ya kutangazwa mwenyeheri,Papa Yohane Paulo I,tunachapisha audio na maneno yaliyotamkwa mnamo tarehe 29 Juni 1968 wakati ule akiwa Askofu wa Vittorio Veneto,katika tukio la kutoa daraja la ukuhani kwa Padre Giuseppe Nadal:maneno kuhusu mfano wa mama na utambulisho ambao hata sasa ni muhimu kuhusu kuhani kwa kutaja sababu ambazo ni za dhati kwa ajili ya useja.

Andrea Tornielli

Mama yangu hakuniambia kamwe kuwa nenda uwe padre, kamwe lakini alikuwa mwema, alipenda sana Bwana ambaye kwa kuwasiliana naye na mimi kwa hiari yangu nikafuata njia hii”. Sauti hiyo haina shaka, na ndio ambayo bado inakumbukwa sana na waamini wengi ambao katika siku hizo 34 za upapa walianza kumfahamu na kumpenda Papa Yohane Paulo I, ambaye sasa atatangazwa mwenyeheri na mfuasi wake Papa Francisko tarehe 4 Septemba 2022. Ni sauti ya Albino Luciani, ambaye wakati ule mnamo tarehe 29 Juni 1968, katika Kanisa kubwa la Parokia ya Mtakatifu Maria wa Piave, Jimbo katoliki la Vittorio Veneto, alikuwa amekuja kumweka wakfu wa daraja la Upadre kwa Padre Giuseppe Nadal.  Dakika kumi na moja za mahubiri bila kusoma, zinatoa utambulisho stahiki wa kikuhani. Hati hiyo inawezekana kuisikiliza yote ambayo imehifadhiwa kwa miaka hamsini iliyopita lakini ambayo ina manen hata leo hii ni muhimu sana. Yanazungumza kwa wachungaji kuwa na arufu ya kondoo na yanatusaidia kuingia katika moyo wa mwenyeheri mpya.

SAUTI YA LUCIANI (PAPA YOHANE PAULO I WAKATI WA MISA YA KUWEKA DARAJA LA UPADRE

Tunapaswa mkumshukuru Padre Giuseppe mwenye umri wa miaka 79 leo hii na ambaye sasa ni Paroko wa Pieve ya Soligo baada ya kuwa mmisionari wa Fidei donum nchini  Burundi kwa  kuwezesha vyombo vya habari Vatican kuwa na  Audio iliyorekodiwa katika Parokia aliyozaliwa katika siku yake ya kupewa daraja la upadre. Hapo mwanzo Luciani alikuwa na mawazo kwa ajili ya familia ya kuhani mpya na kwa ajili ya sadaka alizotoa kwa ajili yake. Askofu anakumbuka mwandishi wa Kifaransa ambaye alisema: “Kuna mama ambao wana moyo wa kikuhani na kuuingiza ndani ya watoto wao”. Kisha anamkumbuka mama yake, Bortola Tancon, ambaye kwa ushuhuda wake wa imani alikuwa amempeleka kuukumbatia ukuhani na kusema: “ilionekana kwangu kwamba hapakuwa na njia nyingine kwangu. Bwana alitumia mazingira ya familia”.

 “Kiukweli ninatumaini - aliongeza Luciani - kwamba Bwana atamsaidia kuhani mpya, kama makuhani niliowaweka wakfu leo asubuhi, na kuwaweka wakfu kwa watu, wenye uwezo wa kuhudumu. Ninyi mnasikia wanaitwa wahudumu wa Mungu: wahudumu  maana yake ni watumishi, watumishi wa Mungu na watumishi wa watu. Kuhani ni kuhani mwema anapokuwa mtumishi wa wengine; ikiwa ni mtumishi wa nafsi yake mwenyewe hayuko sawa”. Askofu Luciani alimtaja “padre mtakatifu” Padre  Francesco Mottola, mwenyeheri baadaye, ambaye alikuwa ameandika kuwa: “Kuhani lazima awe mkate, kuhani lazima ajiruhusu kuliwa na watu”. Kwa hiyo “kuwa tayari kwa watu nyakati zote; alikana familia yake kwa makusudi ili aweze kupatikana katika familia nyingine ”.

Katika mahubiri  hayo pia kuna rejea ya wazi juu ya useja wa kipadre ambapo alisema: “Mtu fulani anasema: ‘Mapadre hawaoi kwa sababu Kanisa halithamini ndoa, linaogopa kuweka ndoa pamoja na mambo haya matakatifu’: si kweli, si kweli! Mtakatifu Petro alikuwa ameowa, si hivyo. Badala yake, sisi tunafikiri hivi: familia ni jambo tukufu na kubwa na kwa usahihi kwa sababu hiyo ikiwa mtu ni baba wa familia ana mambo ya kutosha kufanya wajibu wake: watoto wa kuelimishwa, watoto wa kulea; kuna shughuli nyingi, kwa njia hiyo, familia ni kubwa sana kwa mtu kuwa na familia na kuweza kufanya kazi kubwa kama vile ukuhani. Ama kitu kimoja au kingine”. Aliendelea askofu wa Vittorio Veneto kwamba: “Kwa hivyo ninarudia: kuhani ndiye mtumishi wa wote. Hii ni kazi yake hasa, mahali pake, kutumikia. Na watu wanajua jinsi ya kuelewa wanapoona kwamba kuhani ni mtumishi ambaye anajifungua kwa ajili ya wengine. Kwa hiyo akasema: 'Tuna kuhani mwema', basi anafurahi, basi anafurahi kweli”.

Baada ya kuhakikisha kwamba kabla ya kumweka wakfu padre, “mitiahani mingi inafanywa na “kile ambacho watu wanafikiri juu yake” kinasikilizwa, Luciani alisisitiza juu ya ushuhuda wake binafsi, yaani, juu ya umuhimu wa kumwilisha maishani kile anachokiri na kuhubiri. Na alifanya hivyo akiwa na sifa zinazoeleza unyenyekevu wake. Kwa sababu neno lililohubiriwa, “kwanza, yamkini, lazima aliishi; Siwezi kuwaambia ninyi wengine, Kuwa wema, ikiwa kwanza mimi si mwema; na kama wakati fulani mlijua jinsi ya kuonea haya hata kwa askofu, kujionesha mbele ya watu na kusema: 'Kuwa mwema, kuwa mwema zaidi, labda sijafanya vya kutosha, mimi pia sitoshelezi'. “Ingependeza sana ikiwa mimi, kabla ya kuwahubiria wengine, ningefanya kila kitu ninachowaambia wengine. Haiwezekani kila wakati. Unapaswa kuridhika na juhudi, sisi pia tuna tabia, sisi pia tuna udhaifu. Walakini, ikiwa kuhani anataka kuwa kuhani, lazima asijitokeze kuhubiri kwa wengine ikiwa yeye mwenyewe hajajaribu angalau - kwa juhudi za mara kwa mara - kufanya kile anawaomba wengine kufanya”.

Hatimaye, pendekezo: katika maisha ya kichungaji na katika adhimisho la sakramenti, alisema: “maungamo juu ya yote”, mtu lazima awe mpole na kuwatendea watu vizuri: Daima ninawaambia makuhani wangu: 'Ndugu wapendwa ... watu lazima watibiwe vizuri. Ikiwa ni kweli kwamba sisi ni watumishi, lazima tuwatendee watu mema; haitoshi kujitolea kwa watu, bali kuwa mpole na watu hata kama mtu fulani hana shukrani”. Na ikiwa siku zote hakuna shukrani inayofaa, hatupaswi kufanya kazi kwa shukrani hii. Bwana anatungoja huko, ili kuona ikiwa, licha ya kila kitu, tunaweza kuendelea kufanya mema kidogo kwa watu”. Hitimisho ni sala na nia ya “kuwa na  makuhani ambao ni watakatifu kweli na watumishi wa watu”.

Papa Paulo I mnamo 1968
27 August 2022, 10:34