Takwimu zinaonesha kwamba, hadi kufikia tarehe 30 Agosti 2022 zaidi ya watu 1, 136 wamekwisha kufariki dunia, Takwimu zinaonesha kwamba, hadi kufikia tarehe 30 Agosti 2022 zaidi ya watu 1, 136 wamekwisha kufariki dunia,  

Mshikamano wa Papa Francisko Na Watu Mungu Pakistan: Mafuriko

Hadi kufikia tarehe 30 Agosti 2022 zaidi ya watu 1, 136 wamekwisha kufariki dunia, na watu 364, 000 wameikimbia nchi yao ili kutafuta: hifadhi na usalama Waathirika wa mafuriko haya ni ni zaidi ya milioni 33 sawa na asilimia 15% ya idadi ya wananchi wote wa Pakistan. Mafuriko yamesababisha hasara ya zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 10. Watu wengi wanahitaji msaada wa dharura.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 28 Agosti 2022 baada ya uzinduzi wa Maadhimisho ya Mwaka wa 728 wa Msamaha wa Papa Celestin V, kwa kufungua lango la Kanisa kuu la “Santa Maria in Collemaggio” Jimbo kuu la Aquila, nchini Italia; ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu na kuonesha matumaini makubwa kwamba, mji wa L’Aquila utaweza kugeuka na kuwa ni mji mkuu wa: msamaha, amani na maridhiano. Baadaye, ameongoza Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la “Santa Maria in Collemaggio.” Baba Mtakatifu ametumia fursa hii, kuonesha mshikamano wa udugu wa upendo kwa watu wa Mungu nchini Pakistan ambao wamekumbwa na mafuriko makubwa na hivyo kusababisha maafa kwa watu na mali zao.

Watu wengi wameathirika kwa mafuriko nchini Pakistan
Watu wengi wameathirika kwa mafuriko nchini Pakistan

Baba Mtakatifu anaendelea kusali na kuwaombea wale waliofariki dunia, ili wapate pumziko la milele, wajeruhi waweze kupona na wasiokuwa na makazi maalum, waweze kupata hifadhi, kwa njia ya ukarimu na mshikamano wa Jumuiya ya Kimataifa  Takwimu zinaonesha kwamba, hadi kufikia tarehe 30 Agosti 2022 zaidi ya watu 1, 136 wamekwisha kufariki dunia, na watu 364, 000 wameikimbia nchi yao ili kutafuta: hifadhi, usalama na maisha bora zaidi. Waathirika wa mafuriko haya ni ni zaidi ya milioni 33 sawa na asilimia 15% ya idadi ya wananchi wote wa Pakistan. Mafuriko haya yamesababisha hasara ya zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 10. Watu wengi wanahitaji msaada wa dharura.

Papa Pakistan
30 August 2022, 07:00