Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko anasema, madhara makubwa ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 pamoja na vita, Jumuiya ya Kimataifa imejikuta ikikabiliana na mgogoro wa kijamii na kiuchumi! Baba Mtakatifu Francisko anasema, madhara makubwa ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 pamoja na vita, Jumuiya ya Kimataifa imejikuta ikikabiliana na mgogoro wa kijamii na kiuchumi!  

Nia za Papa Francisko Kwa Mwezi Agosti, 2022: Wafanyabiashara

Baba Mtakatifu Francisko anasema, madhara makubwa ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 pamoja na vita inayopiganwa sehemu mbalimbali za dunia, Jumuiya ya Kimataifa imejikuta ikikabiliana na mgogoro wa kijamii na kiuchumi! Pengine, watu wengi hawajalitambua hili. Waathirika wakuu katika mgogoro huu ni wafanyabiashara wadogo wadogo na wale wa kati,

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Waraka wa Kitume wa Papa Leo XIII: “Rerum Novarum” yaani “Mambo Mapya” ni msingi wa Mafundisho Jamii ya Kanisa katika ulimwengu mambaoleo. Huu ulikuwa ni mwanzo wa Kanisa kuangalia changamoto zilizokokuwa zinajitokeza katika medani mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kitamaduni; ukinzani uliojitokeza kati ya mtaji, nguvu kazi na itikadi mbalimbali zilizoibuka katika kipindi cha Karne ya kumi na tisa. Mama Kanisa alipenda kupenyeza tunu msingi za Kiinjili ili kuitajirisha jamii, kwa kuinjilisha na kuenzi utu, heshima na haki msingi za binadamu; kwa kubainisha haki na dhamana ya Kanisa katika masuala ya kijamii. Huu ni ufahamu unaopata chimbuko lake kutoka katika mwanga wa imani, ili kufundisha na hatimaye, kukuza na kudumisha haki na upendo katika jamii, daima kwa kusoma alama za nyakati na kuendelea kupyaisha ulimwengu ili uweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi! Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko katika Nia zake za Jumla kwa Mwezi Agosti 2022, katika ujumbe wake kwa njia ya video, inayosambazwa na Mtandao wa Utume wa Sala Kimataifa anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusali na kuwaombea wafanya biashara wadogo wadogo na wale wa kati, katika kipindi hiki cha mgogoro wa kiuchumi na kijamii, waweze kupata njia ya kuendelea na shughuli kwa kuhudumia jumuiya zao.

Vita na athari za mabadiliko ya tabianchi vina madhara katika ukuaji wa uchumi.
Vita na athari za mabadiliko ya tabianchi vina madhara katika ukuaji wa uchumi.

Baba Mtakatifu anasema, madhara makubwa ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 pamoja na vita inayopiganwa sehemu mbalimbali za dunia, Jumuiya ya Kimataifa imejikuta ikikabiliana na mgogoro wa kijamii na kiuchumi! Pengine, watu wengi hawajalitambua hili. Waathirika wakuu katika mgogoro huu ni wafanyabiashara wadogo wadogo na wale wa kati. Hawa ni wale wanaotekeleza dhamana na majukumu yao kwenye maduka, wakati wa semina na warsha mbalimbali; wanaoshughulikia masuala ya usafi, usafirishaji pamoja na shughuli nyingine nyingi. Hawa ni wale ambao majina na shughuli zao haziwezi kuoneshwa kwenye orodha ya wenye nguvu kiuchumi. Licha ya matatizo na changamoto wanazokabiliana nazo, bado wameendelea kuchangia katika mchakato wa kutengeneza fursa za ajira sanjari na kutekeleza dhamana na wajibu wao wa kijamii. Hawa ni watu wanaowekeza katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi na wala si wafanyabiashara wanaoficha fedha zao katika “Paradisi za kiuchumi” ili kukwepa kodi.

Wafanyabiashara wadogo wadogo na wale wa kati wameathirika sana.
Wafanyabiashara wadogo wadogo na wale wa kati wameathirika sana.

Wafanyabiashara hawa wanajisadaka bila ya kujibakiza na kwa kweli ni wabunifu wanaoleta mabadiliko ya kweli ndani ya jamii kwa kuanzia kwenye msingi, chimbuko la mchakato wa ubunifu. Wafanya biashara hawa, kwa ujasiri, nguvu na sadaka kuu wanawekeza kwenye Injili ya maisha na hivyo kuchangia katika ustawi wa jamii, fursa sanjari na nafasi za kazi. Baba Mtakatifu Francisko mwishoni wa ujumbe wake kwa njia ya video, anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kusali na kuwaombea wafanyabiashara wadogo wadogo na wale wa kati, ambao wameathirika na mgogoro wa kiuchumi na kijamii, ili waweze kuona na kupata njia ya kuendelea kufanya shughuli zao za biashara pamoja na kuwahudumia jirani zao.

Nia Agosti 2022
04 August 2022, 16:26