Vita bado vinaendelea nchini Ukraine ambapo Papa ameomba kuendelea kuombea nchi hii ikiwa 24 Agosti ni miezi sita tangu kuzuka kwa vita hivi. Vita bado vinaendelea nchini Ukraine ambapo Papa ameomba kuendelea kuombea nchi hii ikiwa 24 Agosti ni miezi sita tangu kuzuka kwa vita hivi. 

Papa Francisko:Vita ni wenda wazimu wanaolipa ni wasio na hatia

Ikiwa ni miezi sita baada ya kuzuka kwa mzozo nchini Ukraine,Papa Francisko baada ya katekesi yake ametoa ombi lake ili kuepusha hatari ya maafa ya nyuklia huko Zaporizhzhia.Mawazo yake pia yamewaendea wakimbizi na watoto na ametaja shambulio la Darya Dugina,binti wa itikadi kali wa Putin na ametoa onyo la wahalifu wanaofanya biashara ya silaha kuwa wanaua ubinadamu;ame kumbuka mizozo ya Siria na Yemen na maafa ya Warohingya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Tafakari yake ya Katekesi, Jumatano tarehe 24 Agosti 2022 kwa mahujaji na waamini waliuksanyika katika ukumbi wa Paulo VI jijini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko ametoa salamu  wanaozungumza kwa lugha mbali mbali na akakumbusha kuombea nchi ya Ukraine kwani ni miezi sita tangu kuzuka kwa vita. Papa Francisko amesema "Ninasasisha mwaliko wangu wa kumwomba Bwana amani kwa ajili ya watu wapendwa wa Ukraine ambao wanateseka kwa  sababu ya vita kwa miezi sita. Ninatumaini kwamba hatua madhubuti zitachukuliwa ili kumaliza vita na kuepusha hatari ya maafa ya nyuklia huko Zaporizhzhia”.

Baba Mtakatifu Francisko ameonesha huzuni  moyo wote kwa ajili ya  wale walio katika hali tete, anaomba mamlaka zinazohusika zifanye kazi ili waachiliwe wafungwa na amefikirie watoto wengi  waliokufa, wakimbizi wengi, sana, walijeruhiwa, watoto wengi wa Kiukreni na watoto wa Kirusi ambao wamekuwa yatima na hawana utaifa, wamepoteza baba au mama zao, wawe wa kiurusi au Kiukraine.

Papa Francisko akiendelea na hilo amesema jinis anavyofikiria ukatili mwingi sana, wa watu wengi wasio na hatia ambao wanalipia gharama ya uwenda wazimu, kila upande kwa sababu vita ni uwenda wazimu na hakuna mtu katika vita anayeweza kusema:kuwa  sio mwenda wazimu. "Huu ni wenda wazimu wa vita", amerudia kusisitiza Papa. Papa amefikiria  yule msichana ambaye alilipuliwa na bomu lililokuwa chini ya kiti cha gari huko Moscow. "Wasio na hatia hulipa gharama kwa vita kwa watu wasio na hatia". Kwa maana hiyo Papa ameomba wote kufikiria ukweli huo na kusema kwamba "vita ni wenda wazimu. Na wale wanaopata mapato kutokana na vita na biashara ya silaha ni wahalifu wanaoua ubinadamu".

Papa Francisko ameomba pia kufikiria  nchi nyingine ambazo zimekuwa kwenye vita kwa zaidi ya miaka kumi,kwa mfano  Siria, kufikiria vita huko Yemen, ambapo watoto wengi wanakabiliwa na njaa, kufikiria Warohingya ambao wanasafiri ulimwenguni kwa dhuluma, wakifukuzwa kutoka katika ardhi yao. Lakini leo hii kwa namna ya pekee miezi sita baada ya kuanza kwa vita Papa amesisitiza kufikiria "Ukraine na Urusi, nchi zote mbili nilizoziweka wakfu kwa Moyo Safi wa Maria, kwamba wewe, Mama, uone nchi hizi mbili zinazopendwa, na kwamba  unaona Ukraine na uione Urusi na utuletee amani! Tunahitaji amani!"

WITO WA PAPA KWA AJILI YA KUOMBEA UKRAINE ILI VITA IISHE
24 August 2022, 12:24