Papa:hekima ya uzee ni kama ujauzito wa kuangazia maisha ya watoto!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko kama kila Jumatano, ametoa tafakari kwa waamini na mahujaji waliofika katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican tarehe 24 Agosti 2022 ambapo katekesi hiyo ilikuwa ni ya mwisho wa mfululizo wa mada kuhusu thamani kuu ya Uzee kwa kutafakari kuhusu Kupalizwa Mbinguni kwa Mama wa Yesu Bikira Maria. Papa Francisko amesema Fumbo hilo linaangaza utimilifu wa neema ambayo ilifunika hatima ya Maria na ambayo pia hatima yetu ni mbinguni. Katika picha ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, kwa nchi za Magharibi zinafanya tafakari ya kuinuliwa juu akiwa amezungukwa na mwanga mtukufu; wakati nchi za mashariki zinaonesha Maria akiwa amelalausingizi kwa kuzungukwa na mitume wakiwa katika sala, na wakati Bwana Mfufuka amemweka amemchukua kwenye mikono yake kama mtoto.
Taalimungu daima imekuwa kitafakari uhusiano huu wa kipekee wa kupalizwa na kifo, ambapo dogma haitoi maelezo yake. Papa amefikiri jinsi ambavyo ingekuwa muhimu kuelezea zaidi juu ya uhusiano wa fumbo la ufufuko wa Bwana ambao unafungua njia kwa kizazi cha maisha kwa ajili yetu wote. Katika tendo la Kimungu la Mama Maria kumfikia Kristo Mfufuka sio, suala rahisi la uharibifu wa kawaida wa mwili wa kifo cha binadamu na sio hilo tu, lakini ni utangulizi wa kupalizwa mwili wa maisha ya Mungu. Kiukweli inajitokeza mapema hatima ya ufufuko ambao unatuhusu, kwa sababu kwa mujibu wa imani ya kikristo, Mfufuka ni mzawa wa kwanza wa kaka na dada wengi. Bwana mfufuka ndiyo ambaye alikwenda kwanza, ambaye alifufuka kwanza, katika nafasi ya kwanza na baadaye tutakwenda sisi, lakini hiyo ndiyo hatima yetu ya kufufuka.
Baba Mtakatifu Francisko, ameongeza kuwa inawezekana kusema kwa kufuata neno la Yesu kwa Nikodemu, ambaye kidogo ni kama kuzaliwa mara ya pili (Yh 3,3-8). Ikiwa kwanza alikuwa amezaliwa duniani, kwa mara ya pili ni kuzaliwa mbinguni. Sio kwa bahati mbaya Mtume Paulo katika somo liliotanguliwa amezungumzia juu ya uchungu wa kuzaliwa ( Rm 8,22). Kama vile jinsi tulivyo toka kwenye tumbo la mama yetu daima ni sisi, na ndiyo sawa la kuwa binadamu ambaye alikuwa katika umbu, na ndiyo baada ya kifo, tunazaliwa mbinguni, katika nafasi ya Mungu na tunabaki kuwa sisi wenyewe ambao tulitembea katika dunia hii. Papa Francisko amesema kuwa kinachofanana na hicho kilitokea kwa Yesu. Mfufuka daima ni Yesu, hakupoteza ubinadamu wake, kuishi kwake na hata mwili wake hapana kwa sababu bila hiyo hasingekuwa Yeye, hasingekuwa Yesu yaani, kuwa na ubinadamu wake na kuishi kwake.
Uzoefu wa mitume unaeleza hayo ambapo Yeye mwenyewe aliwatokea kwa siku arobaini baada ya ufufuko. Bwana alionesha majeraha yake aliyowambwa msalabani; lakini hayikuwa tena na makali ya kuumiza kwa uchungu alioupata, kwa sababu ni majaribu ambayo sasa kwao ni uthibitisho usiofutika wa upendo wake mwaminifu hadi mwisho. Yesu mfufuka na mwili wake anaishi kwa kina ule utatu na Mungu! Na ndani kwake hapotezi kumbu kumbu, haachi historia yake, hayeyushi uhusiano wake ambao aliishi hapa duniani. Kwa marafiki zake alisema kwamba “ Nikisha ondoka nitawaadalia makao”. Yeye alikwanda na akatuandalia makao sisi sote kwani alisema atakopokwenda ataweza kuandaa nafasi, atakutaja kwa upendo na kwenda nasi kwa sababu mahali alipo na sisi tuweze kuwapo (Yh 14,3). Papa kwa maana hiyo ameongeza kusema “Na yeye atakuja na si kwamba atakuja katika mwisho wa wote, bali atakuja kila mara kwa kila mmoja. Atakuja kututafuta na kutupeleka kwake. Katika maana hiyo ya kifo ni hatua ya kukutana na Yesu ambaye anananisubiri kunipeleka kwake”.
Mfufuka anaishi duniani, anaishi mahali ambapo kuna nafasi ya wote, mahali ambapo panaundwa nchi mpya na panajengwa mji wa mbingu, makao ya mwisho wa binadamu. Sisi tunaweza kufikiria mabadiliko ya mwili wetu wa kifo, labda wa kawaida, lakini tuna uhakika kuwa unabaki unajulikana kwa sura na kuwezesha kubaki binadamu mbinguni kwa Mungu. Itaturuhusu kushiriki, kwa hisia tukufu, katika uchangamfu usio na mwisho na wa furaha wa tendo la uumbaji la Mungu, ambalo tutajionea moja kwa moja matukio yote yasiyoisha. Yesu anapozungumza Ufalme wa Mungu anafafanua kama karamu ya Arusi, kama siku kuu, anatusubiri katika sikukuu na marafiki, kazi ambayo inafanyika kamili katika nyumba ni mshangao ambao unafanya kukusanya utajiri kubwa wa kupanda. Kuchukulia kwa uzito maneno ya Injili juu ya Ufalme hutuwezesha hisia zetu kufurahia upendo wa kazi na ubunifu wa Mungu, na hutuweka sawa na hatima ambayo haikuwahi kusikika ya maisha tunayopanda.
Baba Mtakatifu Francisko akiwageukia wazee wenzake amesema: “Katika Uzee wetu umuhimu wa maelezo mengi ambayo maisha hufanywa, bembelezo, tabasamu, ishara, kazi ya kuthaminiwa, mshangao usiotarajiwa, furaha ya ukarimu, dhamana ya uaminifu inakuwa ya papo hapo zaidi. Mambo muhimu ya maisha, ambayo tunayathamini sana karibu na hitimisho letu yanaonekana wazi kwetu. Hapa ni kusema kwamba hekima hii ya uzee ni mahali kama ujauzito wetu, ambao huangazia maisha ya watoto, vijana, watu wazima, na Jumuiya nzima”. Papa Francisko amesisitiza kuwa wao kama wazee wanapaswa wawe hivyo kwa wengine yaani kuwa mwanga kwa wengine. Papa ameongeza kusema kwamba “Maisha yetu yanaonekana kama mbegu ambayo italazimika kuzikwa ili ua na matunda yake yazaliwe. Itazaliwa, pamoja na ulimwengu wote. Lakini si kukosa maumivu, na uchungu bali itazaliwa (taz. Yn 16:21-23). Na uzima wa mwili uliofufuka utakuwa hai mara mia na elfu zaidi ya jinsi tulivyoionja hapa duniani (rej. Mk 10:28-31). Si kwa bahati mbaya kwamba Bwana Mfufuka, aliwaongoja Mitume kando ya ziwa, wakati anaoka samaki (rej. Yn 21:9) na kisha kuwapati. Ishara hiyo ya upendo wa kufikiria hutufanya kutambua kile kinachotungoja tunapopita kwenye ufuo mwingine.
Papa Francisko kwa maana hiyo amewasisitizia hasa wazee wenzake kwamba "maisha bora zaidi bado yataonekana; Lakini wazee, je wanapaswa kuona nini zaidi? Ni swali la Papa Francisko alilo uliza na kusema kuwa ubora zaidi, kwa sababu maisha bora bado hayajaonekana. Na wanatumaini la utimilifu huu wa uzima unaowangoja wote, wakati Bwana anapokapoita. “Mama wa Bwana wetu aliyetutangulia Peponi atuondolee woga wa kungoja kwani sio kungojea kwa ganzi, sio kungoja kwa kuchoka, hapana, ni kungojea kwa matarajio kwamba Bwana atakuja lini? Ni lini nitaweza kwenda huko?” Kwa woga kidogo maana mapitio haya yanamaanisha nini na kuupita mlango ule kunaleta hofu kidogo lakini siku zote kuna mkono wa Bwana unaokupeleka mbele na baada ya kupita mlangoni kuna sherehe. Papa Francisko ameomba wazee kuwa makini na wasikivu kwa sababu Bwana anawasubiri japokuwa kuna hatua ya kupita na baadaye siku kuu. Amehitimisha.