Tafuta

Juma la kiliturujia Kitaifa 22-25 Agosti Juma la kiliturujia Kitaifa 22-25 Agosti 

Papa:ishi mchakato wa sinodi na kugeuka wataalam wa sanaa ya kukutana!

Juma la 72 ya Kiliturujia Kitaifa nchini Italia limefunguliwa huko Salerno alasiri 22 Agosti.Mpango huo unahamasishwa na Kituo cha Matendo ya Kiliturujia.Kwa washiriki hao,Kardinali Parolin Katibu wa Vatican ametuma ujumbe kwa niaba ya Papa ambapo anatumaini kuwa na matunda ya ukweli ya huduma za kikanisa katika mtazamo wa Kanisa linalozidi kujielekeza katika huduma na kuwa na utajiri mwingi wa huduma.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, Jumatatu alasiri tarehe 22 Agosti 2022 ametuma ujumbe kwa niaba ya Papa Francisko kwa Rais wa Kituo cha Utekelezaji Kiturujia, Askofu mkuu Claudio Maniago, wa Catanzaro-Squillace na kwa washiriki wote wa Juma la 72 la Kiliturujia Kitaifa nchini Italia kwenye mji wa Salerno wenye utajiri wa uzuri asili wa kisanaa, ulinzi na si tu muhimu wa kazi nzuri za sanaa takatifu, lakini pia wenye masalia ya Mwili wa Mtakatifu Matayo Mtume na mwinjili  na Baba Mtakatifu Gregori wa VII. Mada inayowaongoza ni “ Wahudumu katika Huduma ya Kanisa la Kisinodi” ambayo inafunika kwa namna ya pekee maana kwa ajili ya Kanisa la sasa katika wakati wa kihistoria na ambalo linafungamanisha kile ambacho Baba Mtakatifu alipata kusema wakati wa ufunguzi wa Sinodi juu ya mchakato wa kisinodi. Papa katika mahubiri yake alihimiza kuishi katika mpango wa Sinodi inao mwona akiwa katika shughuli nyingi leo hii na kumbba kuwa wataalam wa sanaa ya kukutana na tayari kusaidia ili utofauti wa karama, miito na huduma ambayo iweze kuwatajirisha.

Usomaji na huduma ya altareni

Miaka 50 baada ya motu proprio Ministeria quaedam, ambayo Mtakatifu Paulo VI alikuwa amepitia mambo yote ya maagizo madogo huku akihifadhi yale ya Usomaji (Lector)na Akoliti) yaani huduma kama huduma zilizoanzishwa, ambayo haikuzingatiwa tena kuwa imetengwa kwa ajili ya wagombea wa sakramenti ya Daraja tu na hivyo, Kituo cha Matendo ya Kiturujia kinapendekeza ipasavyo tafakari ya uhuishaji wa kiliturujia wa Watu wote wa Mungu, walioitwa katika utofauti wa kazi na huduma ili kumsifu Bwana wao. Mafunzo na majadiliano, kwa mujibu wa  Kardinali amebainisha kwamba yanaweza kuwakilisha mahali pazuri pa kuthibitisha matokeo ya ufanisi ya huduma mpya zilizoanzishwa za (Lector, Acolyte) yaani usomaji na huduma ya altareni,  pia  ya Katekista katika mazoezi ya kikanisa, kwa kutazama uendelezaji wa huduma sawa katika mwanga wa Majisterio ya Papa Francisko, ambayo alisema: " inatualika mara kwa mara kupyaisha mitindo ya kikanisa katika ufunguzi wa jumuiya zaidi, ili kushinda majaribu yoyote ya mabaki ya ukuhani ukuhani."

Huduma mbali mbali za Kanisa

Kwa barua binafsi ya Papa motu Proprio Spiritus Domini, Kardinali amebainisha kuwa ilishinda kikwazo, kisha kikadumishwa, ambacho kilielekeza huduma za msomaji na mtoa huduma altareni kwa wanaume pekee na kupanga kuingizwa kwa wanawake katika huduma za walei wenye ubatizo na marekebisho ya  kifungu cha Kanoni 230 § 2. Zaidi ya hayo, kwa motu Proprio Antiquum Ministerium Papa alilipatia Kanisa sura ya huduma iliyoanzishwa ya Katekista. Baraza la wakati ule ambalo sasa ni Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti za Kanisa, kwa agizo la Baba Mtakatifu, baadaye likafuata Waraka kwa Marais wa Mabaraza ya Maaskofu juu ya Ibada ya kuanzishwa kwa Makatekista, pamoja na ibada inayolingana nayo. Kwa maana hiyo Kongamano lao linatokana na fundisho hilo, linalowaleta pamoja Maaskofu, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake watawa na walei wengi, wanaojishughulisha na huduma mbalimbali. Kardinali Parolin amebainisha kuwa ni Matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, kusanyiko hilo lenye sifa zinazojiweka katika huduma ya kichungaji ya Makanisa nchini Italia, kuanzia na mtazamo wa makini hali ya sasa, miaka sitini baada ya kuanza kwa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, kuongezeka kwa taalimungu ya kina, utunzaji wa kiliturujia-kichungaji wa ukweli wa huduma, kufungua mitazamo inayopaswa kutolewa kwa utambuzi wa kichungaji wa jumuiya ya kikanisa.

Niko miongoni mwenu kama mhudumu

“Mimi niko miongoni mwenu kama mhudumu” (rej. Lk, 22:27), anasema Bwana, na hiyo ndiyo kielelezo kinachopaswa kuhamasisha kila huduma katika Kanisa. Kutokana na somo hilo la Injili huduma ya Kanisa inafanywa upya daima, ili kila mmoja aweze kuishi katika uhalisi wa imani na huduma, jukumu ambalo, kwa nguvu ya ubatizo na karama za Roho, inaitwa kutekeleza", amesisitiza Kardinali Parolin. Maono yenyewe ya Kanisa kama fumbo la muungano na kutafakari kwa kina zaidi uwepo na utendaji wa Roho Mtakatifu, kumechangia katika kumulika vyema wajibu wa walei katika jumuiya ya kikanisa. Kwa maana hiyo ni suala la kuhamasisha waamini walei ule mwamko ulio wazi zaidi wa wito wao, unaooneshwa katika wingi wa kazi na huduma kwa ajili ya kuwajenga watu wote wa Kikristo.

Kardinali Parolin hata hivyo anatoa angalizo kubwa kwamba: “Katika kushughulikia masuala haya ni lazima kuwa waangalifu ili kutochanganya ukuhani wa kawaida na ukuhani wa huduma, kwa kutafsiri kiholela dhana ya “badala2 , “clericalizing”,  yaani kufanyizwa hukuhani hukuhani na hivyo kukimbia hatari ya kuunda muundo wa kikanisa wa huduma sambamba na hiyo ulioanzishwa juu ya sakramenti ya Daraja. Kwa maana hiyo Kardinali Parolin amethibitisha kwamba Baba Mtakatifu anawahakikisha sala zake huku akiombea ulinzi wa mama Bikira  na Mama wa Kanisa, na kwa furaha amewatumia Baraka za Kitume kwa Askofu Mkuu wa  Jimbo kuu, kwa wachungaji wake, Mapadre wengine, mashemasi, watawa, wale na pia kwa watoa mada na wote wanaoshiriki Juma hilo la Liturujia. Katika kuungana na matashi  hayo na yake binafsi, Kardinali Parolin anawatakia matashi mema ya mpango huo muhimu wa kichungaji,na mechukua fursa ya tukio hilo  kushukuru tena kwa heshima ya kipekee kwa Askofu Mkuu.

UJUMBE WA PAPA KWA WASHIRIKI WA JUMA LA 72 LA KILITURUJIA KITAIFA ITALIA
22 August 2022, 21:09