Papa kwa familia:'Kamwe kutosahau sala ambayo hudumisha uhai wa imani yetu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Familia ya moja ya wajasiriamali ya Pedro Maria Guirmaraes de Mello mjini Vatican, Ijumaa tarehe 26 Agosti 2022 na kuwaleza kuwa wao ni familia kubwa na iliyoungana. Amewashukuru kwa ushuhuda wao wa upendo wao kwa Kanisa kwa hija yao katika kaburi la Mtakatifu Petro. Ni imani yao katika Yesu iliyowapeleka hao na kufawanya kufika hapo kwa pamoja. Papa amesema ni vizuri kuona familia iliyoungana kuwa na nguvu ya zawadi ya imani. Akiwatazama familia hiyo amejiwa akilini ili Zaburi ya 133 isemayo: “Ni jambo zuri na la kupendeza sana ndugu kuishi pamoja kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri yatiririkayo kichwani. (Zab 133, 1-2).
Baba Mtakatifu Francisko amesema “Mafuta ni picha nzuri ya muungano, ni picha ya furaha ya kukutana katika umoja. Lakini mafuta pia ni picha ya imani ambayo inaongeza nguvu vifungo vyetu, kwa njia ya Roho Mtakatifu na kutuwezesha maelewano katika familia, na hii ni muhimu maelewano hata katika Kanisa na katika ulimwengu”. Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo amewatia moyo wasiache kamwe mafuta hayo yaishe ya imani katika taa zao (rej. Mt 25, 1-13). Katika maana hiyo kwa kushirikiana kwa namna nyingine na neema ya Mungu ambayo inawafanya kuwa na uzoefu wa kukutana na Mungu.
Baba Mtakatifu amesema uwepo wa Bwana unafanywa uzoefu kwa namna nyingi, lakini hasa katika Sakramenti na katika kutafakari Neno lake. “Sala inatusaidia kubaki na imani iliyo hai. Amewaomba wasisahau sala, na mafuta ya imani yanahifadhiwe ili kukabiliana mara nyingi na wazo kwa Bwana, ambayeamesema “ anaweza kutusaidia kutazama Msulibiwa” . Kusimama na kutazama Yesu juu ya Msalaba ndio ushauri ambao ameweleza. “Na huo ndio mtindo wa kusali. Kama familia na kama binafsi.
Papa amewaalika wendelee mbele katika safari yao ya imani kwa kujikabidhi katika wema wa Bwana na kwa ulinzi wa mama ambaye wao wanafanya ibada sana huko Fatima. Baba Mtakatifu amewaomba wasali pamoja salamu Maria mara tatu na kuhitimisha kwa Baraka.