Tafuta

2022.08.02 Nembo ya Ziara ya Papa huko Aquila 2022.08.02 Nembo ya Ziara ya Papa huko Aquila 

Ziara ya Kitume ya Papa huko Aquila:msamaha ni silaha pekee dhidi ya vita!

Katika mahojiano yaliyotolewa na gazeti la Abruzzo ‘Il Centro’,siku mbili kabla ya ziara yake huko Aquila,Papa anazungumzia suala la ujenzi upya uliofanywa baada ya tetemeko la ardhi la 2009 na anatoa mwaliko kutumaini Mungu katika giza la majaribu na kuthamini ujumbe kutoka kwa Pietro da Morrone.Utamaduni wa amani lazima ukuzwe ili kuondokana na migogoro yoyote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Saa 48 kabla ya  kuwasili Aquila, Papa Francikos anageukia Aquila ili kuwathibitisha kwa matumaini ya Yesu Aliyesulubiwa na Kufufuka, lakini pia kuwahimiza kuthamini ujumbe ambao Papa Selestine aliouacha kwa Kanisa zima , akieleza kwamba unyenyekevu, upendo, ukaribu, msamaha, huruma ndiyo njia nzuri zaidi ya kutangaza Injili. Papa amezungumza hayo kutoka kwenye safu za gazeti liitwalo  “Il Centro”. Katika mahojiano yaliyotolewa kwenye gazeti la Abruzzo na kuchapishwa tarehe 26 Agosti 2022  anazungumzia kuhusu ujenzi mpya unaokabili jiji hilo, ambalo halihusu tu  nyumba bali roho za watu, na anashukuru Kanisa la Aquila kwa ushuhuda kwani limeleta katika miaka ya hivi karibuni na anaongeza kuwa umoja pekee ndio hufanya mabadiliko ya kweli na ya kudumu iwezekanavyo  na  kwamba lazima tuache nyuma mambo yote yanayotugawa na badala yake tuthamini kila kitu kinachotuunganisha", kwa sababu ni kwa njia hiyo tu haitakuwa tu utopia lakini uhakika wa kupumzika siku zijazo na kujitolea kwa kila mtu.

Maandalizi ya Ziara ya Papa huko Aquila 28 Agosti 2022
Maandalizi ya Ziara ya Papa huko Aquila 28 Agosti 2022

Baba Mtakatifu Francisko anajibu maswali manne, lakini kutokana na janga la tetemeko la ardhi la tarehe 6 Aprili 2009 ambalo lilibadilisha historia ya Aquila na maisha ya watu wengi, anaona kwamba maumivu na mateso daima ni fumbo na kwamba haitoshi “Kuwa na hoja za kusadikisha” ili usalama kutokana na giza la uzoefu fulani” Hata Yesu, Papa anakumbusha kuwa alikuwa na uzoefu wa kuishi giza hilo, kujisikia peke yake, kushindwa, lakini "litufundisha kwamba kwa usahihi wakati huo wakati kila kitu kinaonekana kupotea inawezekana kabisa kumwamini Baba. Sio rahisi   kuzaliwa kwa upya bila ishara hiyo ya uaminifu kwa wale ambao wana uwezo wa kutushika mkono wakati tu uhakika mwingine wote unakuja kuharibika, amesema Baba Mtakatifu  akikumbuka kwamba kwa mwamini maisha haya ni njia tu kuelekea  maisha ambayo hayapiti na kwamba bila uhakika huu hakuna kitu kingekuwa na maana, na kila kitu kingekandamizwa na hatima ya kifo. Lakini kuwa na ufahamu huu ni zawadi ambayo lazima iombewe na wakati huo huo inapaswa kulindwa kutokana na kila kitu ambacho kingependa kuzima.

Siku ya Jumapili 28 Agosti Papa Fransisko atafungua Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu  Maria wa Collemaggio, kutoa nafasi kwa ajili ya  Msamaha wa 728 wa  Papa Selestina, msamaha wa kikao ambao Papa Selestine V alitoa kwa wale wanaotubu na kwa kuungama kwenda mahali pa ibada kutoka tangu Masifu ya Jioni ya tarehe 28 Agosti hadi  siku inayofuata. Na ni kwa ajili ya msamaha kwamba awakaribisha kutazama vita katika Ukraine na kwa  wale wengine, migogoro ambayo inatesa maelfu ya watu na juu ya watu wote wasio na hatia. Kwa sababu hiyo uovu haushindwi kwa ubaya, bali kwa wema tu na inahitaji nguvu zaidi kusamehe kuliko kufanya vita.

Hata hivyo, msamaha unahitaji ukomavu mkubwa wa mambo ya ndani na kiutamaduni Papa Francisko anafafanua, akihimiza kila mtu kukuza utamaduni wa amani ambao unapita kwa usahihi kutokana na  kukomaa kwa msamaha unaowezekana" Kando ya hayo yote, tunabaki tukiwa tumezama katika mantiki ya uovu inayofungamana na mantiki ya maslahi ya wale wanaotumia fursa ya migogoro hiyo ili kujitajirisha na kujinufaisha” kwa hiyo msamaha ndiyo silaha pekee inayowezekana dhidi ya vita vyovyote, ameisitiza Papa Francisko .

Maandalizi ya Ziara ya Papa huko Aquila 28 Agosti 2022
Maandalizi ya Ziara ya Papa huko Aquila 28 Agosti 2022

Hatimaye, katika kurasa za kwanza za gazeti la Abruzzo, Papa anaakisi umaskini na kubainisha kwamba ni lazima kutofautishwe kati ya kile ambacho ni tunda la ukosefu wa haki na umaskini wa kiinjili ambao ni uhuru kutokana   milki. Jambo la kwanza lazima lipiganiwe kwa haki na mshikamano; pili, kwa upande mwingine, lazima ichaguliwe kama njia inayoongoza kwenye kupata amani ya kweli.  Papa Francisko anaongeza kuwa ni pale tu ambapo mtu si mtumwa wa milki ndipo inapowezekana kupata uhuru huo wa ndani unaotufanya tujisikie kuwa na furaha kwa kila kitu maishani. Kwa sababu umaskini kwa Mkristo, Papa anahitimisha, ni njia ya kuwa katika ulimwengu, na ni mtazamo wa mtu ambaye yuko huru kweli.

Ujumbe wa Papa kwa Aquila katika Gazeti la Abruzzo
26 August 2022, 18:31