Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Kazakhstan:picha na video za matukio ya kipapa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko katika ziara yake ya kitume ya 38 ameudhuria Kongamano la Saba la Viongozi Wakuu wa Dini Duniani na Dini za Jadi huko Nur Sultan nchini Kazakhstan kuanzia kuanzia tarehe 13-15 Septemba 2022. Kongamano hilo limeongozwa na kauli mbiu “Mchango wa Viongozi wa Dini Duniani na Dini za Jadi katika mchakato wa maendeleo ya kijamii na kiroho baada ya janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19.” Video na picha zifuatazo zinaonesha matukio hayo tangu kufika kwake, mapokezi, mikutano mbali mbali, misa, hata Ujumbe wa mwisho wa Kongamano hilo uliotolewa tarehe 15 Septemba.
Katika kongamno la viongozi hao, mwishoni mwa yote, wameto atamko la pamoja. Katika tamko hilo, Viongozi hao wa Dini ulimwenguni watajibidhisha kutimiza kila jitihada kwa ajili ya kuhakikisha shughuli za kusaidia mazungumzo kati ya dini, tamaduni na ustaarabu. Na kutoka huko Nur-Sultan nchini Kazakhstan wanatoa ahadi ya kutumia hatua zaote za mchakato wa amani, kwa kutambua hasa juu ya umuhimu na thamani ya Hati juu ya Udugu wa kibindamu kwa ajili ya amani ulimwenguni na kusihi pamoja, uliotiwa saini huko Abu Dhabi mnamo tarehe 4 Februari 2019 na Papa Francisko pamoja na Imam Mkuu Al-Tayyib wa Azhar.
Papa alifika uwanjani akapolewa kwa shangwe]Jumatano, tarehe 14 Septemba 2022 Baba Mtakatifu amepata fursa ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano hili lililofunguliwa kwa sala ya ukimya na Baba Mtakatifu amekazia kuhusu: Utambulisho na thamani ya uhai wa mwanadamu; athari za misimamo mikali ya kidini na kiimani; Uhuru wa kidini na changamoto zinazoikabili Jumuiya ya Kimataifa kwa sasa: UVIKO-19, Amani, Udugu wa Kibinadamu sanjari na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote.
Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea Kazakhstan amepitia katika anga la Italia, Croatia, Bosnia-Erzegovina, Serbia/Montenegro, Uturuki, Bulgaria, Georgia, Azerbaijan na hatimaye Kazakhstan. Ametumia mwanya huu kuwatakia waandishi wote wa habari ambao wako kwenye msafara wake, safari njema
Katika ziara hii Papa Francisko alipowasili nchini Kazakhstan, Jumanne, tarehe 13 Septemba 2022, jioni baada ya Mapokezi ya Kitaifa, alikutana kwa faragha na Rais na baadaye alizungumza na viongozi wa Serikali, mashirika ya kiraia pamoja wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi na Mashirika ya Kimataifa. Jumatano tarehe 14 Septemba 2022, Baba Mtakatifu alishiriki katika Kongamano la Saba la Viongozi Wakuu wa Dini Duniani na Dini za Jadi. Jioni hiyo Papa aliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu.
Katika siku yake ya mwisho Alhamisi tarehe 15 Septemba 2022 Papa atakutana na kuzungumza kwa faragha na Wayesuit wanaoishi na kufanya utume wao nchini Kazakhstan. Na baadaye Papa anatarajia kukutana na kuzungumza na watu wa Mungu nchini humo kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria Msaada wa Daima. Alasiri 15 Septemba Papa Francisko atashiriki na kutoa hotuba ya mwisho wakati Wajumbe watakapokuwa wanatoa Tamko la Kongamano la Saba la Viongozi Wakuu wa Dini Duniani na Dini za Jadi mjini Kaza, Nur Sultan. Baadaye ataondoka na kurejea mjini Roma majira ya saa 2: 15 Usiku.
Hatimaye mnaweza kuona ziara nzima ya kitume ya Papa Francisko kwa klip ndogo ya vdeo kuanza tangu alipofika huko hadi kuanza safari ya kurejea.