Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko hujaji wa majadiliano na amani. Baba Mtakatifu Francisko hujaji wa majadiliano na amani. 

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Kazakhstan: Hujaji wa: Majadiliano, Amani na Matumaini.

Hii ni hija ya 38 ya Baba Mtakatifu Francisko Kimataifa, lengo ni kuendelea kuragibisha mchakato wa majadiliano ya kidini kwa ajili ya kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa. Baba Mtakatifu Francisko katika hija hii ni hujaji wa majadiliano, amani na matumaini kwa watu wa Mungu ndani na nje ya Kazakhstan. Umuhimu wa Majadiliano ya Kidini

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kongamano la Saba la Viongozi Wakuu wa Dini Duniani na Dini za Jadi linaadhimishwa mjini Kaza, Nur Sultan huko nchini Kazakhstan kuanzia tarehe 13-15 Septemba 2022, kwa kunogeshwa na kauli mbiu “Mchango wa Viongozi wa Dini Duniani na Dini za Jadi katika mchakato wa maendeleo ya kijamii na kiroho baada ya janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19.” Hii ni hija ya 38 ya Baba Mtakatifu Francisko Kimataifa, lengo ni kuendelea kuragibisha mchakato wa majadiliano ya kidini kwa ajili ya kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani na maridhiano kati ya watu wa Mataifa. Baba Mtakatifu Francisko katika hija hii ni hujaji wa majadiliano, amani na matumaini kwa watu wa Mungu ndani na nje ya Kazakhstan.

Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan
Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan

Kama sehemu ya desturi na utamaduni wake, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 12 Septemba 2022 Kumbukumbu ya Jina Takatifu la Bikira Maria, amekwenda kutembelea na kusali kwenye Sanamu ya Bikira Maria Afya ya Warumi “Salus Populi Romani” iliyoko kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu, Jimbo kuu la Roma, kabla ya kuanza hija yake ya kitume ya 38 huko Kazakhstan kuanzia tarehe 13-15 Septemba 2022. Itakumbukwa kwamba, Bikira Maria Malkia wa Amani ni Mlinzi na Mwombezi wa nchi ya Kazakhstan. Wachunguzi wa mambo wanasema, Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu lililoko Jimbo kuu la Roma ni kati ya Makanisa ambayo Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro ameyatembelea mara nyingi zaidi kwa ajili ya sala ya binafsi: kuomba na kushukuru kila wakati anapoadhimisha matukio makuu katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan
Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan

Baba Mtakatifu anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kukuza na kudumisha Ibada kwa Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa, ili aweze kuwasaidia kuwa ni vyombo na mashuhuda wa huruma na upendo wa Mungu kwa jirani zao, kielelezo cha imani tendaji! Bikira Maria ni mfano na kielelezo cha imani, matumaini na mapendo, kwani amediriki kuwa ni mfuasi wa kwanza wa Kristo Yesu na chombo cha huduma makini kwa jirani zake; mtindo na mfumo wa maisha unaopaswa kutekelezwa na Mapadre kama sehemu ya majiundo yao ya awali na endelevu katika maisha na utume wa Kanisa.

Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan
Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan

Baba Mtakatifu anasema, ikiwa kweli waamini wanataka kuwa wafuasi wamisionari wa Kristo Yesu na Kanisa lake; ili kuguswa na kuponywa na huruma pamoja na upendo wa Mungu, wanapaswa kuzingatia mambo makuu yafuatayo: Fumbo la Msalaba, Ekaristi Takatifu na Ibada ya Bikira Maria, Mama wa Mungu na Kanisa. Bikira Maria ni Mama wa Mungu na Kanisa, kwani ndani ya Moyo wake safi usiokuwa na doa, watu wote wanapata utambulisho wao, kwa kupenda na kupendwa, hali inayoonesha uwepo wa Mungu kati ya watu wake.

Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan
Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan

Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea Kazakhstan amepitia katika anga la Italia, Croatia, Bosnia-Erzegovina, Serbia/Montenegro, Uturuki, Bulgaria, Georgia, Azerbaijan na hatimaye Kazakhstan. Ametumia mwanya huu kuwatakia waandishi wote wa habari ambao wako kwenye msafara wake, safari njema; heri na baraka katika shughuli zao na kwamba, wataongea kwa mapana na marefu wakati wa kurejea tena Roma. Baba Mtakatifu Ametumia pia fursa hii kuwapatia na kuwatakia: furaha, neema na baraka; umoja, amani; ustawi, udugu maendeleo pamoja na kuwahakikishia sala zake katika maisha na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na wakuu wa nchi na serikali zao.

Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan
Ziara ya Kitume nchini Kazakhstan

Baba Mtakatifu katika salam na matashi mema kwa Rais Sergio Mattarella wa Italia amemwambia kwamba, anakwenda nchini Kazakhstan ili kushiriki katika Kongamano la Saba la Viongozi Wakuu wa Dini Duniani na Dini za Jadi mjini Kaza, Nur Sultan huko nchini Kazakhstan kuanzia tarehe 13-15 Septemba 2022, kwa kunogeshwa na kauli mbiu “Mchango wa Viongozi wa Dini Duniani na Dini za Jadi katika mchakato wa maendeleo ya kijamii na kiroho baada ya janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19.” Hii ni fursa kwake kukutana na kuzungumza na watu wa Mungu, lakini kwa namna ya pekee na waamini wa Kanisa Katoliki nchini humo. Baba Mtakatifu anawaombea amani, ustawi na maendeleo watu wa Mungu nchini Italia.

Papa Bikira Maria

 

13 September 2022, 16:31