Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini Kazakhstan:kurudi Helsinki na kuzungumza na wote
ANDREA TORNIELLI
Ni wakati wa kuepuka msisitizo wa ushindani na uimarishaji wa vizingiti vinavyopingana. Tunahitaji viongozi ambao, katika ngazi ya kimataifa, wanaruhusu watu kuelewana na mazungumzo, na kuzalisha “roho mpya ya Helsinki”, utashi wa kuimarisha umoja wa kimataifa, wa kujenga mawazo ya ulimwengu wa utulivu na amani ya vizazi vipya”. Papa Francisko anafikiria juu ya mustakabali wa ulimwengu, hajisalimishi katika mantiki kubwa na ya mwisho ya kuongezeka kwa wanajeshi ambayo inatishia kuangamiza ubinadamu na kwa sababu hiyo anaendelea kuonesha njia madhubuti za amani. Njia zinazoibuka kutoka kwenye mantiki za zamani za miungano ya kijeshi, ukoloni wa kiuchumi, nguvu kubwa ya wakuu na wenye nguvu katika ngazi ya kimataifa.
Katika Mji Mkuu Nur-Sultan nchini Kazkhstani mahali ambapo mnamo Septemba 2001 Mtakatifu Yohane Paulo II katika wakati mkasa wa historia ya ubinadamu aliinua kilio chake cha kuondoa uhalali wowote wa ugaidi na vurugu zinazotumia vibaya kwa jina la Mungu, mrithi wake Papa Francisko aliomba kuhuisha roho ambayo mnamo mwaka 1975 iliibua hatua madhubuti za mazungumzo kati ya Mashariki na Magharibi. Miaka 21 iliyopita, wito wake Papa Wojtyla, ambaye alikuwa ametembea bila viatu kwenye msikiti wa Umayyad huko Damascus miezi michache kabla ya mashambulizi kwenye Minara Miwili, ya Marekani alikuwa amewaelekeza awali ya yote kwa viongozi wa kidini.
Leo hii kwa mujibu wa mfuasi wake, mwenye wasiwasi kuhusu Vita vya Kidunia vya Tatu tena vilivyogawanyika vipande vipande, amewalenga kwa namna ya pekee viongozi wa mataifa, hasa kwa wale wakuu kama ilivyokuwa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II. Na katika safari ya Kazakhstan baada ya Septemba 11, Papa Francisko, katika hotuba yake ya kwanza huko Kazakhstan, kwa mamlaka na mashirika ya kiraia, alikumbuka safari ya Papa Wojtyla, mnamo Septemba 2001, ambaye “alikuja kupanda matumaini mara moja... Makubaliano ya Helsinki, ambayo yaliona Vatican ikishiriki kikamilifu kwa mara ya kwanza katika mkutano wa aina hiyo tangu Mkutano wa Vienna, uliotiwa saini na nchi thelathini na tano, pamoja na USA, USSR na karibu mataifa yote ya Ulaya. Miongoni mwa kanuni zilizothibitishwa ni pamoja na kuheshimu haki ya kujitawala, kutotumia nguvu, kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani, kutokiukwa kwa mipaka na uadilifu wa eneo la nchi, kuheshimu haki za binadamu na uhuru wake, pamoja na uhuru wa kidini, na maamuzi ya watu binafsi.
Katika mtazamo wa historia ya hivi karibuni, pamoja na kufifia taratibu kwa matumaini mengi ambayo yalichochewa baada ya mfumo wa ukomunisti wa Kisovieti kuzuiwa, hunafanya kuelewa mada yenye kuvutia na pia ujasiri wa mtazamo uliooneshwa na Mrithi wa Petro. Njia ambayo inaweza kupitia tu uelewa, uvumilivu na mazungumzo na kila mtu. “Ninarudia, kwa wote,” Papa Francisko alisema kwa makusudi katika hotuba yake kwa mamlaka na vyombo vya kidiplomasia katika mji mkuu wa Kazakh. Katika hotuba ya kwanza aliyohutubia mamlaka, Papa alielezea nchi ya Asia kama “nchi ya kukutana" na akawa ndiye mbeba kilio dhidi ya vita vya Ukraine kwamba tunahitaji viongozi wenye uwezo ...
Maneno kama ya "mazungumzo" na "mchakato" zaidi ya miezi sita baada ya kuanza kwa vita vya uchokozi vya Urusi dhidi ya Ukraine na baada ya maelfu ya vifo vya raia chini ya shambulio la bomu la Urusi, yanapokelewa kwa hasira na kuchukuliwa kama kufuru na wale wanaolipa gharama kubwa katika ngozi zao wenyewe na juu ya wapendwa wao kwa matokeo ya migogoro. Lakini mwaliko wa Papa, ambaye alizungumza juu ya hitaji kubwa zaidi la "kupanua dhamira ya kidiplomasia katika kupendelea mazungumzo na mkutano", inaelekezwa hasa kwa "wale ambao katika ulimwengu wana mamlaka zaidi ya juu na kwa hivyo, "kuwa na jukumu zaidi kwa wengine, kwa namna ya pekee zile nchi zilizo katika mgogoro mkubwa kwa mantiki zinazokinzana."
Ni mwaliko kwa wakuu wa ulimwengu sio tu kuangalia maslahi ambayo huangukia kwa faida yao wenyewe”. Ni mwaliko wa kutoka nje ya mantiki ya vizuizi ili hatimaye kutumia kile ambacho Papa Francisko alikiita "mipango ya amani" na sio tena "mipango ya vita", watoto wa mantiki ya zamani na wazimu wa mbio za silaha tena. Na kwa kila mtu anatumaini kuwa maneno haya yatasikika.