Malkia wa Uingereza ameaga dunia tarehe 8 Septemba 2022 akiwa na umri wa miaka 96 Malkia wa Uingereza ameaga dunia tarehe 8 Septemba 2022 akiwa na umri wa miaka 96 

Papa ametoa Salamu za Rambi rambi:Elizabeth II ni mfano stahiki wa kujitoa!

Papa Francisko anamkumbuka Malkia na utumishi wake bila kuchoka kwa wema.Katika telegram ya rambirambi,Papa ametoa salamu za rambirambi,huku akiwakikishia kusali kwa ajili ya roho ya Malkia na kwa ajili ya majukumu yaliyo ya juu ambayo Mfalme mpya Charles III anatakiwa.

Vatican News

Katika telegram yake Papa Francisko amemwandikia Charles III, Mfalme mpya wa Uingereza kufuatia na kifo cha mama yake kilichotokea siku ya Alhamisi jioni tarehe 8 Septemba 2022, kwamba: “Nimehuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Mtukufu Malkia Elizabeth II, na kwa maana hiyo ninatoa rambirambi za dhati kwa Mtukufu, wanafamilia ya Kifalme, watu wa Uingereza na Jumuiya ya Madola.

Malkia wa Uingereza na mikutano ya Mapapa wakati wa maisha yake

Papa Francisko akiendelea amebainisha kuwa: “Kwa moyo ninaungana na wale wote wanao omboleza kwa ajili ya kifo chake,​​ kumwombea apate pumziko la milele Marehemu Malkia na kutoa heshima kwa maisha yake ya utumishi wake bila kuchoka kwa ajili ya manufaa ya Taifa na Jumuiya ya Madola, kwa mfano wake wa kujitolea na uwajibu, kwa ushuhuda wake thabiti wa imani katika Yesu Kristo na tumaini lake thabiti katika ahadi zake”.

"Kwa kumkabidhi roho yake tukufu kwa wema wa rehema wa Baba yetu wa Mbinguni, Baba Mtakatifu  ameongeza "ninakuhakikishia mkuu mpya maombi yangu kwamba Mungu Mwenyezi atakutegemeza kwa neema yake isiyoyumba wakati sasa unachukua majukumu yako ya juu kama Mfalme.  Na kwako wewe na wote wanaohifadhi kumbu kumbu ya marehemu mama yako, naomba wingi wa baraka za kimungu kama ahadi ya faraja na nguvu katika Bwana” amehitimisha  Baba Mtakatifu.

Salamu za Rambi rambi za Papa Francisko kufuatia kifo cha Malkia wa Uingereza
08 September 2022, 22:00