Tafuta

2022.09.21 Papa Francisko wakati wa Katekesi 2022.09.21 Papa Francisko wakati wa Katekesi  

Papa ametoa shukrani ya ziara ya kitume huko Kazakhstan mfano wa Ustaarabu&ujasiri

Katika Ketekesi yake Papa amejikita juu ya ziara yake ya kitume nchini Kazakhstan na amefafanua kukutana na sehemu yenye thamani ya amani na udugu,sera za kisiasa na dini vina hadhi sawa kwani imetimiza chaguzi chanya kama ile ya kukataa haraka silaha za nyuklia.Papa anatoa shukrani kwa rais,Mamlaka na Kanisa la Kazakha kwa shauku na kuishi heri za udogo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika katekesi yake Jumatano 21 Septemba 2022 kwa mahujaji na waamini waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ametoa mhutasari wa hija yake ya 38 ya kitume hivi karibuni, nchini Kazakhstan kuanzia tarehe 13 – 15 Septemba 2022 kuudhuria Kongamano la Saba la Viongozi Wakuu wa Dini Duniani na Dini za Jadi  huko Nur Sultan. Hata hivyo kabla ya kuanza tafakari,limesomwa neno la Mungu: “Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. Hili ni Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli wakihubiri habari njema ya amani kwa  njia ya Yesu Kristo  huyo ndiye Bwana wa wote” (Mdo 10,34-36). Kongamano hilo liliongozwa na kauli mbiu: “Mchango wa Viongozi wa Dini Duniani na Dini za Jadi katika mchakato wa maendeleo ya kijamii na kiroho baada ya janga la UVIKO-19.”   Kwa maana hiyo Papa amepyaisha shukrani kwa Rais wa Jamhuri na Wakuu wa Mamlaka ya Kazakhstan kwa makaribisho aliyopokea na kwa ajili ya ukarimu na nguvu za kuandaa. Vile vile Papa amewashukuru Maaskofu na wahudumu kwa kazi kubwa waliyoifanya hasa kwa furaha ambayo wamempatia  kuweza kukutana na kuwaona pamoja.

KATEKESI YA PAPA FRANCISKO 21 SEPTEMBA 2022
Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022
Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022

Kama alivyotangulia kusema kuwa ziara yake ilikuwa ni kushiriki Kongamano la Vingozi Wakuu wa Dini Duniani na Dini za Jadi. Shughuli hii ilianzishwa miaka 20 iliyopita na Mamlaka ya Nchi ambayo inawakilisha yenyewe katika ulimwengu kama nafasi ya kukutana na kuzungumza, katika muktadha huo kwa ngazi za kidini na kushirikiana na kuhamasisha amani na udugu wa kibinadamu. Papa ameongeza kusema kuwa ilikuwa Juma la toleo la Kongamano hilo. Katika nchi ambazo kwa miaka 30 ya huru imefanya tayari matoleo 7 ya Makongamano hayo yafanyikayo kila baada ya miaka mitatu. Hii ina maana ya kuweka dini katikati ya juhudi kwa ajilli ya ujenzi wa ulimwengu ambamo kuna usikivu na kuheshimu tofauti. Na hii sio kuuwiana, hapana: ni kusikiliza na kuheshimu. Na hili lazima itambuliwe serikali ya Kazakh, ambayo, mara baada ya kujikomboa kutoka kwenye nira ya utawala wa watu wasioamini Mungu, sasa inapendekeza. Bila kuwachanganya au kuwatenganisha, ikilaani waziwazi ugaidi na msimamo mkali. Ni msimamo wenye uwiano na umoja.

Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022
Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022

Kongamano lilihitimishwa kwa makubaliano ya tamko la mwisho ambalo linapendekeza mwendelezo wa Waraka uliotiwa saini huko Abu Dhabi  mnamo 2019 kuhusu Udugu wa kibinadamu. Baba Mtakatifu amependa kutafsiri hatua hiyo ya mbele kama tunda la mchakato wa safari ambayo inatoka mbali. Amefikiria mkutano wa kihistoria wa kidini kwa ajili ya amani uliotishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II huko Assisi mnamo 1986 ,ambapo amesema kuwa huku “akikosolewa sana na watu ambao hawakuwa na maono”; Aidha Papa amefikiria mtazamo wa mbali wa Mtakatifu Yohane XXIII na Mtakatifu Paulo VI; hata na  ule wa roho mbili za dini nyingine, kwa kukumbuka na kutaja Mahatma Gandhi. Lakini pia akasema inawezekanajie kusahau kumbu kumbu ya mashidi wengi wanaume na wanawake wa kila rika, lugha na taifa ambao walilipa kwa maisha yao kwa uaminifu wa Mungu kwa ajili ya amani na udugu? Papa amesema: “tunajua vipindi vikuu ni muhimu, lakini pia ni jitihada za kila siku, ni ushuhuda wa dhati ambao unajedha ulimwengu kuwa bora kwa wote”.

Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022
Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022

Hata hivyo Baba Mtakatifu amesema, zaidi ya kongamano katika ziara yake aliweza kukutana na Mamlaka ya  Kazakhstan  na Kanisa linaloishi katika Nchi hiyo. Baada ya kutembelea Rais wa Jamhuri, ambaye amemshukuru tena kwa ukarimu wake, walikwenda tena katika Ukumbi wa Tamasha, mahali ambapo aliweza kuzungumza na wakuu wa nchi, wawakilishi wa jamii ya raia na wanadiplomasia. Papa amebainisha jinsi alivyojikita kuonesha wazi wito wa Kazakhstan wa kuwa Nchi ya makutano. Kwani kiukweli wanaishi karibia makundi 150 ya makabila! Wanazungumza zaidi ya lugha 80. Huu wito ni ambao upo katika tabia zake za kijiografia na za historia yake. Wito huu wa kuwa nchi ya mkutano, ya tamaduni na lugha imekuwa kikikaribisha na kukumbatia kama mchakato wa safari ambayo inastahili kutiwa moyo na kusaidiwa. Baba Mtakatifu amesema alivyowatakia waweze kuendelea katika ujenzi wa demokrasia daima komavu zaidi, yenye uwezo wa kujibu kwa dhati mahitaji ya jamii nzima. Ni kazi muhimu ambayo inahitaji muda, lakini lazima kutambua kuwa Kazakhstan ilifanya chaguzi nyingi chanya, kama ile ya kusema hapana kutumia silaha za kinyuklia na ile ya kuwa na sera nzuri za kisiasa kuhusu nishati na mazingira. Hiyo alikuwa jasiri. Wakati ambapo vita hii ya kutisha inatuongoza kufikiria katika silaha za nyuklia, kwa wazimu huo, nchi hiyo ilisema "hapana" kuwa na  silaha za nyuklia tangu mwanzo!

Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022
Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022

Kwa mtazamo wa Kanisa, Papa amebainisha alivyofurahishwa kukutana na jumuiya ya watu wenye furaha na shauku. Wakatoliki ni wachache katika Nchi hiyo ambayo ni kubwa sana. Lakini hali hiyo ikiwa wanaishi kwa imani, inawezakana kupeleka matunda ya kiinjili. Awali ya yote hadhi  za udugu, za kuwa chachu, chumvi na mwanga kwa kutegemea  Bwana tu na si juu ya mitindo inayojitokeza ya kibinadamu. Zaidi ya hayo, uhaba wa idadi Papa amesema “unatualika kukuza uhusiano na Wakristo wa madhehebu  mengine na pia udugu na wote. Hivyo kundi dogo, ndiyo, lakini kuwa na uwazi, na si kufungwa, si kujihami, uwazi na ujasiri katika hatua ya Roho Mtakatifu, ambaye anavuma kwa uhuru ni wapi aende na jinsi gani anataka”.  Kwa kuongezea Papa amesema, walikumbuka pia sehemu zenye kiza kama  ya wafidini. Hao ni Watu watakatifu wa Mungu wafiadini, kwa sababu waliteseka kwa miongo kadhaa ya ukandamizaji wa wasioamini Mungu, hadi ukombozi wake miaka 30 iliyopita, wanaume na wanawake ambao waliteseka sana kwa ajili ya imani katika kipindi kirefu cha mateso. “Kuuawa, kuteswa, kufungwa, kwa ajili ya imani”.

Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022
Katekesi ya Papa 21 Septemba 2022

Kwa kundi hilo dogo lakini lenye furaha Papa alibainisha kuwa waliadhimisha Ekaristi, pia huko Nur Sultan, katika jengo kwenye uwanja wa Maonyesho ya 2017, iliyozungukwa na usanifu wa kisasa zaidi. Ilikuwa ni sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu. “Na hii inafanya kutafakari kwamba katika ulimwengu ambamo maendeleo na kurudi nyuma vimefungamana, Msalaba wa Kristo unabaki kuwa nanga ya wokovu: ishara ya matumaini ambayo haikatishi tamaa kwa sababu msingi wake ni upendo wa Mungu, mwenye huruma na mwaminifu. Papa kwa Kuhitimisha amesema “Shukrani zetu zimwendee kwa ziara hii, na maombi yetu ili iweze kuwa na matunda mengi kwa mustakabali wa Kazakhstan na kwa maisha ya Kanisa la Hija katika nchi hiyo”.

KATEKESI YA PAPA 21 SEPTEMBA 2022
21 September 2022, 16:45