Papa Francisko anasali kwa ajili ya waathirika wa dhoruba Fiona
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Uharibifu na waathirika ambao kupita Kimbunga Fiona kimacha nyuma, msimu wa kwanza ambao tayari umevuma kwa upepo unaozidi kilomita 210 / kwa saa huko Santo Domingo na Puerto Rico, tukio ambalo limemhuzunika Papa Francisko na ambaye ametuma telegramu mbili zilizo sainiwa na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin kwa Makanisa mahalia, akikabidhi jumuiya za nchi zote mbili katika mikono ya upendo ya Bikira Maria.
Msukumo wa ukaribu wa kindugu na mshikamano kwa Jamhuri ya Dominika
Akimwelekea Askofu Mkuu Freddy Antonio de Jesus Breton Martinez, wa Santiago de Los Caballeros na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Dominika, Baba Mtakatifu anawabariki wana na mabinti wote wa Jamhuri ya visiwa vya Karibiani huku akiwahakikishia maombi yake kwa sababu Bwana aweza kuwafariji wapendwa wa Dominika ambao wanaoteseka. Kwa upande wa Baba Mtakatifu pia amaetoa wito kwa Jumuiya nzima ya Kikristo na kwa watu wenye mapenzi mema kufanya juhudi kubwa zaidi ya mshikamano na ukaribu wa kindugu kwa wale ambao ni wahanga wa janga hilo analokabidhi kwa mikono ya upendo na ya kimama ya Mama Yetu wa Altagracia.
Papa amewakabidhi mikononi mwa Maria watu wa Puerto Rico
Katika telegramu aliyoielekezwa kwa rais wa Baraza la Maaskofu wa Puerto Rico, Askofu Ruben Antonio Gonzalez Medina, wa Ponce anaomba salamu zake ziwafikie wapendwa wa Puerto Rico ambao wanaomboleza kwa sababu ya kupoteza maisha ya binadamu, na kurekodi uzito wa uharibifu uliosababishwa na kimbunga Fiona. Nchini kulikuwa na hali ya dharura kutokana na maporomoko ya ardhi kuangusha miti na nyaya za umeme zilizopulizwa, pamoja na kuporomoka kwa miundombinu mingi. Kulingana na wataalamu, tukio la janga kutokana na matokeo ya mafuriko litabaki. Kwa ajili ya maafa"ya wakati huo Papa Fransisko anasali kwa Baba mwenye rehema ili awape faraja yake. Papa Francisko anawatumia baraka yake huku akiwaweka katika mikono ya Mama Yetu wa Maongozi ya Mungu.