Tafuta

Papa Francisko,Assisi:Uchumi mpya usikilize kilio cha maskini na dunia

Uwezo wa kujihoji ni mtindo gani wa sasa wa maendeleo,kusikiliza kilio cha masikini na dunia,ndio matarajio ya Papa Francisko kutoka kwa wanauchumi vijana,wafanyabiashara na wajasiriamali waliokusanyika Assisi kutoka zaidi ya nchi 100 katika mkutano wa Uchumi wa Francisko. Hali ya dunia ya sasa inahitaji dhana mpya za kiuchumi zinazoweka katikati maskini,mazingira.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu ametoa hotuba yake Jumamosi tarehe 24 Septemba 2022 huko Assisi Italia, kwa vijana elfu moja kutoka nchi 120 duniani kote, waliofika katika tukio la "Uchumi wa Francisko" ambapo hawa ni wajasiriamali, wafanyabiashara na wanamabadiliko. Akianza hotuba yake Papa amesema ni miaka 3 akiwa anasubiri wakati huu kwani ni tangu Mei Mosi 2019 alipowaandikia barua ambayo iliwaita na baadaye imewapeleka Assisi. Wengi wao wamesikika katika ushuhuda wa mkutano huo wa Uchumi wa Francisko ambapo barua hiyo iliwazindua ndani mwao kile ambacho tayari walikuwa nacho.  Walikuwa tayari wanajibidisha kuunda uchumi mpya. Barua ile iliwaweka pamoja na kuwapa upeo mpana zaidi, iliwafanya wahisi sehemu ya jumuiya ya ulimwengu wa vijana ambao wana wito unaofanana. Wakati kijana anapoona kijana mwenzake mwenye wito sawa na baadaye katika uzoefu katikati ya mamaia na maelfu ya vijana wengine, inawezakana kufanya mambo makubwa, hadi kutumaini kubadili mfumo mkubwa na mgumu kama uchumi duniani. Papa Francisko amewaeleza vijana kwamba, kwa msaada wa Mungu wao wanajua kufanya na wanaweza kufanya; kwa sababu vijana walifanya zaidi katika mchakato wa historia.

Ziara ya kichungaji huko Assisi ya Papa Francisko katika Mkutano wa "Uchumi wa Francisko"

Papa Francisko akiendelea amebainisha jinsi ambavyo wao wako wanaishi kipindi ambacho sio rahisi. Kipindi cha matatizo ya mazingira, baadaye janga la uviko na sasa vita nchini Ukraine na vita vingine vinavyoendelea kwa miaka  sasa katika nchi tofauti, na ambavyo vinaathiri maisha yao. Kizazi hiki kimewaachia urithi wa utajiri mwingi, lakini hawakujua kuhifadhi sayari na wala hatuko tunahifadhi amani. Kama vijana wanaalikwa kuwa wahunzi na mafundi rafiki wa ardhi na uchumi wa amani. Hii ni katika kubadili uchumi ambao unaua (taz. Evangelii gaudium, 53) kuwa katika uchumi wa maisha na aina zake zote. Baba Mtakatifu Francisko amefuarahishwa  na  chaguzi zao za kuandaa mkutano wa Assisi kuhusu Unabii. Maisha ya Mtakatifu Francis, baada ya uongofu yalikuwa ni unabii, ambao unaendelea katika wakati wetu. Katika biblia, Unabii unaendelea kwa  vijana. Samueli alikuwa kijana, Yeremeah na Ezekieli walikuwa vijana; Danieli alikuwa kijana mdogo sana na aliweza kutoa unabii kwa hasiye na hatia Susana na kumwokoa dhidi ya kifo (Taz. Dn 13,45-50);  na Nabii Joeli alitangazia watu kuwa Mungu atawapa Roho na watageuka manabii wa mabinti na wana wao (Joeli 3,1). Kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu, Papa ameongeza kusema vijana ni wachukuzi wa roho moja ya sayansi na ya akili.

Alikuwa ni kijana Daudi aliye mnyenyekeza mwenye kiburi Goria (1Sam 17,49-51). Kiukweli ikiwa jumuiya ya kiraia na makampuni yanapokosekana uwezo wa vijana, jumuiya nzima ambayo inayonyauka, inazimika maisha ya wote. Unakosekana ubunifu, ari na shauku. Jamii moja na uchumi bila vijana ni yenye huzuni m ngumu na  tamaa. Lakini shukrani kwa Mungu wao wapo,  si kwa ajili ya kesho lakini lakini leo hii; wao tayari wapo, kwa wakati uliopo. Uchumi ambao unaacha kuhuishwa na ukuu wa kinabii unajieleza leohu katika maono mapya ya mazingira na  dunia.  Kuna watu wengi, makampuni na taasisi ambazo zipo zinafanya kazi ya kubadilika kiikolojia. Lazima kwenda mbele katika njia na kufanya zaidi. La zaidi wao wako wanafanya na wanaendelea kuomba wote. Haitoshi kufanya  vipodozi, lazima kijikita katika mjadala wa mtindo wa maendeleo. Hali halisi ndivyo ilivyo,  ambayo haiwezekani kusubiri mkutano ujao wa kimataifa,  tu wakati dunia inawaka moto sasa na ni leo ambayo lazima kubadilika kwa ngazi zote. Kwa mwaka uliopita wamekuwa wakifanya kazi kwenye uchumi wa mimea, mada ya ubunifu ambapo wameona kwamba dhana ya mmea ina mtazamo tofauti kwa dunia na mazingira.

Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko
Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko

Mimea inajua jinsi ya kushirikiana na mazingira yote yanayoizunguka na hata inaposhindana, kiukweli inashirikiana kwa manufaa ya mfumo ikolojia. Tujifunze kutokana na upole wa mimea, amesisitiza Papa: unyenyekevu na ukimya wao unaweza kutupatia mtindo tofauti ambao tunauhitaji haraka. Kwa sababu, ikiwa tunazungumza juu ya mpito wa ikolojia lakini tukabaki ndani ya dhana ya kiuchumi ya karne ya ishirini, ambayo ilipora maliasili na ardhi, njia tutakazopitisha hazitatosha kila wakati. Biblia imejaa miti na mimea, kuanzia mti wa uzima hadi mbegu ya haradali. Na Mtakatifu Francisko anatusaidia na udugu wake wa ulimwengu na viumbe vyote vilivyo hai. Sisi watu katika karne mbili zilizopita, tumekua kwa gharama ya ardhi. Mara nyingi tumeipora ili kuongeza ustawi wetu binfasi na sio ustawi wa kila mtu. Huu lakini  ni wakati wa ujasiri mpya katika kuacha vyanzo vya nishati, ili kuharakisha maendeleo ya vyanzo vya athari sifuri au chanya. 

Na baadaye tunapaswa kukubali kanuni ya kimaadili ya ulimwengu wote ambayo hatupendi  na kwamba uharibifu lazima urekebishwe: ikiwa tumekua tukiitumia vibaya sayari na tabianchi,  leo hii tunapaswa pia kujifunza kujitoa katika maisha ambayo bado hayawezi kudumu. Vinginevyo, watoto wetu na wajukuu watakuwa wakilipa bili, ambayo itakuwa ya juu sana na isiyo ya haki. Mabadiliko ya haraka na madhubuti yanahitajika. Papa anategemea vijana hao wasiwachwe peke yao bali watoe mfano. Katika hilo Papa ameongeza  kusema "Nilimsikia mwanasayansi muhimu sana ulimwenguni, miezi sita iliyopita, ambaye alisema: "Jana nilizaliwa mjukuu. Ikiwa tutaendelea hivi, maskini, ndani ya miaka thelathini italazimika kuishi katika ulimwengu usioweza kukaliwa".  kwa kuongezea Papa amesema "Na ninawaambia ukweli: kuishi kwenye njia hii inahitaji ujasiri na wakati mwingine inachukua ushujaa kidogo. Nilisikia, katika mkutano, mvulana mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikuwa ametoka tu kama mhandisi wa ngazi ya juu, hakuweza kupata kazi; mwishowe alijikuta katika tasnia ambayo haikujua kabisa ni nini maana yake; aliposoma alichopaswa kufanya hata kama hakuwa na kazi, katika nafasi ya kufanya kazi, alikataa, kwa sababu walitengeneza silaha. Hawa ndio mashujaa wa siku hizi”.

Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko
Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko

Uendelevu, basi, ni ukweli wa pande nyingi. Mbali na ile ya mazingira, pia kuna mwelekeo wa kijamii, uhusiano na kiroho. Ule wa  kijamii  huanza polepole kutambuliwa kwani tunatambua kwamba kilio cha maskini na kilio cha dunia ni kilio sawa (taz.Laudato si ', 49). Kwa hiyo, tunapofanyia kazi mabadiliko ya kiikolojia, ni lazima tukumbuke madhara ambayo baadhi ya chaguzi za kimazingira zinaathiri  umaskini. Sio suluhishi zote za mazingira zina matokeo sawa kwa walio maskini zaidi, na kwa hivyo zile zinazopunguza taabu na ukosefu wa usawa zinapaswa kupendelewa. Ingawa tunajaribu kuokoa sayari, hatuwezi kupuuza wanaume na wanawake wanaoteseka. Uchafuzi unaoua sio tu ule wa  hewa chafuzi (kaboni dioksidi), lakini pia ukosefu wa usawa unachafua sayari yetu. Hatuwezi kuruhusu majanga mapya ya kimazingira kufuta maafa ya kale na ya kila mara ya ukosefu wa haki wa kijamii kutoka katika maoni ya umma. Halafu kuna kutokuwa endelevu kwa uhusiano wetu: katika nchi nyingi, uhusiano wa watu unazidi kuwa duni. Hasa katika nchi za Magharibi, jumuiya zinazidi kuwa tete na kugawanyika. Familia, katika baadhi ya maeneo ya dunia, zinakabiliwa na janga kubwa, pamoja na kukaribishwa na kutunzwa kwa maisha. Utumiaji wa sasa unatafuta kujaza pengo la uhusiano wa kibinadamu na bidhaa za kisasa zaidi, na upweke ni biashara kubwa katika wakati wetu! lakini hivyo inazalisha njaa ya furaha.

Hatimaye, kuna kutokuwa na uendelevu kiroho kwa ubepari wetu. Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba mwanadamu, aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, kabla ya kuwa mtafutaji wa mali ni mtafutaji wa maana. Ndiyo maana mtaji msingi wa kila jamii ni ule wa kiroho, kwa sababu ndio unaotupatia  sababu za kuamka kila siku na kwenda kufanya kazi, na kuzalisha furaha hiyo ya maisha ambayo ni muhimu pia kwa uchumi. Ulimwengu wetu unatumia kwa haraka sana aina hii muhimu ya mtaji iliyokusanywa kwa karne nyingi na dini, kwa mapokeo ya hekima, na ibada maarufu za watu  kwa Mungu. Na hivyo zaidi ya yote vijana wanakabiliwa na ukosefu huu wa maana na  mara nyingi wanakabiliwa na uchungu na kutokuwa na uhakika wa maisha wanajikuta na nafsi maskini za rasilimali za kiroho kushughulikia mateso, kuchanganyikiwa, kukata tamaa na huzuni. Udhaifu wa vijana wengi unatokana na ukosefu wa mtaji huo wa thamani ya kiroho: mtaji usioonekana lakini  ambao ni halisi zaidi kuliko mtaji wa kifedha au kiteknolojia. Kuna uhitaji wa haraka wa kuunda upya urithi huo muhimu wa kiroho. Mbinu inaweza kufanya mengi: na inatufundisha "nini" na "jinsi" gani ya kufany, lakini haituambii  ni kwa nini"; na hivyo matendo yetu yanakuwa tasa na hayajazi maisha, hata maisha ya kiuchumi, papa amesisitiza.

Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko
Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko

Kwa kujikuta katika jiji la Mtakatifu Francis , Papa Papa amesema  hawezi  kujizuia kujikita kueleza umaskini. Kufanya uchumi uliohamasishwa Francis kunamaanisha kujitolea kuwaweka masikini katikati. Kuanzia wao kwa kutazama uchumi, na kuanzia wao kutazama dunia. Bila heshima, huduma, upendo kwa maskini, kwa kila mtu maskini, kwa kila mtu dhaifu na mazingira magumutangu kutungwa kwa  mimba ndani ya tumbo la mama hasi kufikia mtu mgonjwa na mlemavu, kwa wazee katika shida, hakuna “Uchumi wa Francisko”. Papa Francisko amependa kusema kuwa  uchumi wa Fransisko hauwezi kuwa na kikomo kwa kufanya kazi au pamoja na maskini. Maadamu mfumo wetu unazalisha waliobaguliwa  na kufanya kazi kulingana na mfumo huu, tutakuwa tumeshiriki katika uchumi unaoua. Kwa hiyo Papa amesema wajiuliza je: tunafanya vya kutosha kubadili uchumi huu, au tunaridhika na uchoraji wa ukuta kwa kubadilisha rangi, bila kubadilisha muundo wa nyumba? Pengine jibu haliko katika kile tunachoweza kufanya, bali ni jinsi tunavyoweza kufungua njia mpya ili maskini wenyewe waweze kuwa  wahusika wakuu wa mabadiliko.

Mtakatifu Francis hakuwapenda maskini tu, bali alipenda umaskini pia. Mtakatifu Francis alikwenda kwa wenye ukoma sio sana kuwasaidia, alikwenda kwa sababu alitaka kuwa maskini kama wao. Kumfuata Yesu Kristo, alijivua kila kitu ili kuwa maskini pamoja na maskini. Kiukweli, uchumi wa kwanza wa soko ulizaliwa katika karne ya 13 huko Ulaya katika mawasiliano ya kila siku na Waftratelli Wafransiskani  ambao walikuwa marafiki wa wafanyabiashara hao wa kwanza. Uchumi huo ulitengeneza utajiri, hakika, lakini haukudharau umaskini. Ubepari wetu, kwa upande mwingine, unataka kuwasaidia maskini lakini hauwathamini, hauelewi msema wa ?Heri walio maskini” (rej. Lk 6:20). Hatupaswi kupenda taabu, kinyume chake ni lazima tupambane nazo kwanza kabisa kwa kuunda kazi, kazi inayostahili. Lakini Injili inatuambia kwamba bila kuwaheshimu maskini, hakuna taabu inaweza kutatuliwa. Na kinyume chake  kutoka hapo  vijana lazima waanze, kama  wajasiriamali na wachumi huku wakikaa katika madala wa kiinjili wa Francis.

Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko
Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko

Katika nuru hiyo ya tafakari Papa Francisko amependa kuwaachia maelekezo matatu ya mchakato wa njia ya  kwenda mbele. Ya kwanza: kuangalia ulimwengu kupitia macho ya maskini zaidi. Shiria la  Wafransiskani liliweza kuvumbua nadharia za kwanza za kiuchumi katika Zama za Kati na hata benki za kwanza za mshikamano ("Monti di Pietà"), kwa sababu liliutazama ulimwengu kwa macho ya watu maskini zaidi. Wao pia wataboresha uchumi wakiangalia mambo kwa mtazamo wa wahanga na waliotupwa. Lakini wawe makini kwa  maskini na waathirika, mtu lazima awajue, lazima awe rafiki yao. Papa anaamini  ikiwa wanakuwa marafiki na maskini, ikiwa wanashiriki maisha yao, pia watashiriki kitu cha Ufalme wa Mungu, kwa sababu Yesu alisema kwamba Ufalme wa mbinguni ni wao, na kwa sababu hiyo wamebarikiwa (taz.Lk 6:20). Kwa njia hiyo Papa amerudia tena kwamba uchaguzi wao wa kila siku si kuzalisha wa kutupa

Pili Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa wao hasa ni wanafunzi, wasomi, wajasiriamali, lakini wasisahau ya kazi , wasisahau ya wafanyakazi kazi  ambayo tayari ina changamoto ya wakati wetu na itakuwa bado ya changamoto zaidi kesho. Bila kazi yenye hadhi vijana wengi hawawezi kuwa watu wazima,ukosefu wa usawa unaongezeka. Na wakati mwingine inawezekana kuishi bila kazi lakini  bila kuishi vizuri. Kwa maana hiyo wakati wanaunda bidhaa na huduma, wasisahau kuunda kazi, kazi nzuri, kazi kwa kila mtu.

Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko
Mkutano wa Vijana wa Uchumi wa Francisko

Elekezo  la tatu ni kufanyika mwili. Katika wakati mgumu wa historia, aliyeachwa aongozwa na alama nzuri aliweza kufanya kwa sababu alitafsiri mawazo na shauku, thamani na matendo ya dhati. Zaidi ya kuandika na kufanya mikutano, wanaume na wanawake hawa walitoa maisha katika shule na vyuo vikuu, kwa benki, vyama vya wafanyakazi, vyama vya ushirika, na taasisi. Watabadilisha ulimwengu wa uchumi ikiwa pia watatumia mikono yao pamoja na moyo wao na kichwa. Mawazo ni muhimu, yanatuvutia sana hasa vijana, lakini yanaweza kugeuka kuwa mitego ikiwa hayatakuwa mwili kwa sababu huo ni ukamilifu, ambao unatakiwa kujitolea kila siku. Kanisa daima limekataa jaribu ambalo linadhani kuwa linaweza kubadilisha ulimwengu tu kwa ujuzi tofauti, bila uchovu wa mwili. Matendo haya "angavu" kuliko mawazo makuu, kwa sababu ni thabiti, hasa, yenye mipaka, na mwanga na kivuli pamoja, lakini hurutubisha dunia siku baada ya siku: ukweli ni bora kuliko wazo. ( taz Evangelii gaudium, 233).

Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kwa jitihada ya kazi yao.Amewaomba waendelee mbele kwa msukumo na maombezi ya Mtakatifu Francis. Na amependa kuhitimisha kwa maombi pamoja kwamba “Baba, tunaomba msamaha wako kwa kujeruhi vibaya dunia, kwa kutoheshimu tamaduni za asili, kwa kutowaheshimu na kuwapenda walio maskini zaidi, kwa kuunda mali bila umoja. Mungu aliye hai, ambaye kwa Roho wako alivuvia mioyo, mikono na akili za vijana hawa na kuwapeleka katika nchi ya ahadi, watazame kwa wema ukarimu wao, upendo wao, shauku yao ya kutumia maisha yao kwa ajili ya ubora zaidi. Wabariki katika biashara zao, katika masomo yao, katika ndoto zao; wasindikize  katika shida na mateso, wasaidie kuwageuza kuwa wema na hekima. Uwasaidia matamanio yao ya mema na maisha, waunge mkono wakati wa kukata tamaa kwao mbele ya mifano mibaya, usiwaache wakate tamaa na kuendelea na safari yao. Wewe, ambaye mtoto wako  wa pekee alifanya kuwa fundi seremala, uwape furaha ya kubadilisha ulimwengu kwa upendo, ustadi na mikono. Amina.

Hotuba ya Papa kwa Vijana wa Uchumi wa Francisko
24 September 2022, 13:31