2022.09.18Sala ya Malaika wa Bwana. 2022.09.18Sala ya Malaika wa Bwana. 

Papa Francisko:Shukrani ya makaribisho nchini Kazakhstan

Ikiwa ni Diminika ya XXV ya Mwaka B,Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari yake amekushukuru Mungu kwa ziara yake aliyotimiza hivi karibuni nchini Kazakhstan.Amekumbuka kwa uchungu vita kati ya Azerbaigian na Armenia,pia kuomba kuendelea na sala kwa ajili ya Ukraine.Amewaombea marehemu,familia na watu wote waliokumbwa na mafuriko mabaya mkoa wa Marche Italia.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa Mahujaji na Waamini waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican,Dominika tarehe 18 Septemba 2022, amesema “Ninamshukuru Mungu kwa safari ambayo nimeitimiza hivi karibuni nchini Kazakhstan, katika fursa ya Kongamano la VII la Viongozi wa Dini Ulimwenguni na dini za Jadi na kwa maana hiyo ninapendekeza kuzungumza wakati wa katekesi ijayo.

Maskitiko ya Papa kwa ajili ya Azerbaigian na Armenia

Baba Mtakatifu akiendelea amekumbuka mapigano ya hivi karibuni kati ya nchi mbili Azerbaigian na Armenia. Kwa maana hiyo ameonesha uchungu na kuelezea ukaribu wake wa kiroho kwa familia za waathirika na kushauri sehemu zote mbili kuheshimu na kuacha  mapigano hayo, katika matazamio ya makubaliano ya amani.  Papa amesema “Tusisahau kwamba amani inawezakana zinaponyamaza silaha na kuanza mazungumzo”. Papa  vile vile ameomba kuendelea kusali kwa ajili ya nchi ya Ukraine na kwa ajili ya amani ya kila nchi iliyomwagikiwa na  damu kutokana na vita.

Mafuriko Mkoa wa Marche Italia

Baba Mtakatifu pia amependa kuwahakikishia sala zake watu wa  Mkoa wa Marche, Italia  walishambuliwa na mafuriko ya nguvu sana. Anasali kwa ajili ya marehemu, familia zao, waliojeruhiwa na wale wote waliopata hasara kubwa.  “Bwana awajalie nguvu jumuiya hiyo”, amesema Papa.

Mafuriko mabaya katika mkoa wa Marche Italia
Mafuriko mabaya katika mkoa wa Marche Italia

Baada ya kusema hayo Papa amewasalimia waroma, mahujaji wa kutoka pande zote ambao walifika kwa wingi katika uwanja wa Mtakatifu Petro, kwa namna ya pekee watawa wa Maria Msafi wa Moyo na jumuiya mbali mbali za Afrika, Amerika Kusini, Asia na Ulaya  na wengine wengi yakiwemo makundi ya kiparokia. Papa amesalimia hata vijana wa “Economy of Francesco”, yaani Uchumi wa Francisko, ambao walikuwa kwenye uwanja huo na kuwaleza kuwa waendelee mbele zaidi na wataonana muda si mrefu huko Assisi. Amehitimisha kwa kutakia Dominika Njema na kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

Papa baada ya sala ya Malaika wa Bwana
18 September 2022, 12:11