Tafuta

kauli mbiu: “Zungumzeni Ukweli Katika Upendo”: Veritatem facientes in caritate. “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. kauli mbiu: “Zungumzeni Ukweli Katika Upendo”: Veritatem facientes in caritate. “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. 

Siku ya 57 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni 2023: Kauli Mbiu!

Ujumbe wa Siku ya 55 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni kwa Mwaka 2023 sanjari na Sherehe ya Bwana Kupaa Mbinguni unanogeshwa kwa kauli mbiu: “Zungumzeni Ukweli Katika Upendo”: Veritatem facientes in caritate. “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Efe 4:15. Mchakato wa Sinodi: Matumaini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Siku ya 55 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni kwa Mwaka 2023 sanjari na Sherehe ya Bwana Kupaa Mbinguni unanogeshwa kwa kauli mbiu: “Zungumzeni Ukweli Katika Upendo”: Veritatem facientes in caritate. “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Efe 4:15. Hii ni sehemu ya mchakato wa Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu inayoongozwa na kauli mbiu “Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume” yatakayofikia kilele chake mwezi Oktoba 2023. Baba Mtakatifu anawataka wadau wa tasnia ya mawasiliano ulimwenguni kutekeleza dhamana na wajibu wao kwa upole na kwa hofu, wakitambua kwamba, wanapaswa kuwa ni madaraja ya kuwaunganisha watu na kawe wasiwe ni kikwazo na kuta za kuwagawa na kuwasambaratisha watu. Baba Mtakatifu anakaza kusema, ujumbe huu uguse pia maisha na utume wa Kanisa katika ulimwengu mamboleo, ambako inaonekana kuibuka kwa mijadala ya chuki na uhasama na kwamba, huu ni mwaliko wa kurejea tena kwenye msingi wa maisha na utume wa Kanisa. Ni wakati wa kutangaza na kushuhudia ukweli unaosimikwa katika tunu msingi za Kiinjili.

Waandishi wa habari: madaraja ya kuwakutanisha watu
Waandishi wa habari: madaraja ya kuwakutanisha watu

Huu ni ukweli unaosimikwa katika huruma na ushiriki mkamilifu wakati wa furaha, mateso na hata mahangaiko ya watu, hasa wale waliovunjika na kupondeka moyo. Wanafunzi wa Emau waliokuwa wamekata tamaa, kielelezo cha hali ya maisha ya waamini wengi hata katika ulimwengu mamboleo, walianza kuona cheche za matumaini wakati Kristo Yesu alipokuwa anawafafanulia Maandiko Matakatifu! Si rahisi kuweza kuwaona mabingwa wa matumaini katika Biblia, kwani Mwenyezi Mungu anataka kuthaminiwa na kupendwa; kutangazwa na kushuhudiwa kutoka katika undani wa mtu! Baba Mtakatifu Francisko anasema, katika ulimwengu ambao umesheheni vita, magomvi na mipasuko ya kijamii, kuna haja ya kujenga na kudumisha mawasiliano yatakosaidia mchakato wa ujenzi wa misingi ya haki, amani, upendo na mshikamano wa udugu wa kibinadamu. Waraka wa Mtakatifu Yohane XXIII “Pacem in terris” ulitolewa wakati ambapo dunia ilikuwa inashuhudia kinzani na vitisho vya vita ya kinyuklia.

Tangazeni na kushuhudia ukweli katika upendo
Tangazeni na kushuhudia ukweli katika upendo

Mtakatifu Yohane wa XXIII akapiga moyo konde, akawaalika wakuu wa Jumuiya ya Kimataifa kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano katika ukweli na uwazi ili kujenga misingi ya haki, amani na utulivu, utu na heshima ya binadamu vikipewa kipaumbele cha kwanza. Katika waraka huu, Mtakatifu Yohane wa XXIII alikazia kwa namna ya pekee, umuhimu wa kujenga na kudumisha mahusiano dhabiti kati ya watu wa mataifa kwa kujikita katika ukweli, haki, upendo na uhuru wa kweli, kwani haya ni mambo msingi yanayogusa uwajibikaji wa kimaadili katika ngazi mbalimbali za maisha ya binadamu. Wadau wa tasnia ya mawasiliano watambue kwamba, wanao wajibu wa kushiriki katika ujenzi wa jamii inayosimikwa katika haki na udugu wa kibinadamu kwa leo na kesho iliyo bora zaidi. Jamii inapaswa kujenga pia utamaduni wa majadiliano ya kidini na kiekumene kama njia ya kudumisha misingi ya haki na amani, kwani kwa miaka ya hivi karibuni, dini zimekuwa ni chanzo kingine cha kuvurugika kwa amani kati ya watu hasa kutokana na misimamo mikali.

Kauli mbiu siku 57 Upashanaji Bahari Ulimwenguni
30 September 2022, 15:28