Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa ni vita iliyodumu kuanzia mwaka 1939 hadi 1945 . Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa ni vita iliyodumu kuanzia mwaka 1939 hadi 1945 . 

Papa Francisko: Vita Kuu ya Tatu ya Dunia Inaendelea Kutesa Watu

Bado damu ya watu wasiokuwa na hatia inaendelea kumwagika sehemu mbali mbali za dunia, kiasi kwamba, walimwengu wameshindwa kujifunza kutokana na madhara ya vita. Poland ni kati ya nchi ambazo ziliathirika sana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mchakato wa ujenzi wa amani unapaswa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi, familia, jamii na hatimaye katika jumuiya ya Kimataifa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa ni vita iliyodumu kuanzia mwaka 1939 hadi 1945 kati ya Ujerumani, Italia, Japani na mataifa yaliyoshikamana nazo (Romania, Hungaria na Bulgaria) dhidi ya nchi nyingi za dunia zilizokuwa zilishirikiana na kati yake hasa Uingereza, China, Urusi na Marekani. Hii ni vita iliyoonea duniani kote na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao. Vita kamwe haitokei kwa bahati mbaya. Vita huratibiwa na kutekelezwa na wakuu wa Serikali kwa manufaa yao binafsi na wala katika siasa hakuna jambo linalojitokeza kwa bahati mbaya. Lolote kikitokea ujue lilipangwa kama ilivyokuwa kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 31 Agosti 2022 mara baada ya Katekesi yake amelikumbuka tukio hili la kihistoria, hapo tarehe 1 Septemba 1939, changamoto na mwaliko kwa Jumuiya ya Kimataifa kukataa katu katu kutumbukia katika utamaduni wa vita na badala yake, kutafuta njia muafaka za kuweza kutatua kinzani, migogoro na mipasuko ya kijamii kwa njia ya amani.

Vita Kuu ya Tatu ya Dunian inaendelea kusababisha maafa makubwa.
Vita Kuu ya Tatu ya Dunian inaendelea kusababisha maafa makubwa.

Baba Mtakatifu anakaza kusema, bado damu ya watu wasiokuwa na hatia inaendelea kumwagika sehemu mbali mbali za dunia, kiasi kwamba, walimwengu wameshindwa kujifunza kutokana na madhara ya vita. Poland ni kati ya nchi ambazo ziliathirika sana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kumbe, mchakato wa ujenzi wa amani unapaswa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi, familia, jamii na hatimaye, Jumuiya ya Kimataifa katika ujumla wake. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kusali na kuwakumbuka wale wote wanaoendelea kupoteza maisha yao kutokana na vita sehemu mbali mbali za dunia na kwa namna ya pekee nchini Ukraine. Huu ni wakati wa kuwekeza katika amani na wala si katika vita! Kujenga na kudumisha umoja na mshikamano na maskini na wala si kuendelea kuwatumbukiza katika majanga na maafa. Bikira Maria Malkia wa Amani, awaombee na kuwaimarisha watu wote wenye mapenzi mema, waweze kujikita katika mchakato wa kukuza na kudumisha wema, haki, mshikamano wa udugu wa kibinadamu hasa na maskini, ili kuchipua tena katika nyoyo za watu matumaini, furaha, na uhuru wa ndani.

Vita Kuu ya Pili ya Dunia
01 September 2022, 15:19