Papa Francisko:Yohane Paulo I alihisi furaha ya Injili,akapenda hadi mwisho!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Dominika tarehe 4 Septemba 2022 hatimaye ni siku ambayo ilitarajiwa kwa hamu kubwa kuona Mfuasi wa Petro akiinuliwa kuwa mwenyeheri. Misa Takatifu imeadhimishwa katika Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Mjini Vatican kwa kuongozwa na Baba Mtakatifu Francisko akisaidiana na Kardinali A. Semeraro Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatanagaza watakatifu, makardinali, maaskofu na mamia elfu ya waamini na mahujaji kutoka pande zaote dunia kushiriki tukio la kutangazwa Mwenyeheri Yohane Paulo I . Mwenyeheri mpya ni Papa aliyebaki katika kiti cha Mtume Petro kwa siku 33 tu. Baada ya hatua ya kutangazwa Mwenyeheri, masomo na Injili, Baba Mtakatifu Francisko ameanza mahubiri yake na kusema kwamba Yesu alikuwa anaelekea Yerusalemu na Injili inasema kwamba watu wengi walikuwa wanakwenda naye (Lk 14,25). Kwenda na Yeye kumfuata maana yake ni kugeuka kuwa mfuasi. Lakini licha ya hayo watu hawa, Bwana anawahutubia hotuba ambayo ina mvuto kidogo na inahitaji, kwani anasema huwezi kuwa mfuasi wake ikiwa hapendwi zaidi kuliko ndugu na yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yake, kadhalika kila mmoja asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wake (Rej. Lk 26-27.33).
Je ni kwa nini Yesu aligeukia umati kwa maneno hayo? Ni nini maana ya ushauri wake? Baba Mtakatifu amejaribu kujibu maswali hayo. Awali ya yote, alisema kwa kutazama idadi kubwa, watu wengi ambao walikuwa wanamfuata Yesu. Tunaweza kufikiria kwamba wengi wao walivutiwa sana na maneno yake na kushangaa kwa ishara ambazo alitimiza; na hivyo walikuwa wameona kwake matumaini kwa sababu ya wakati wao ujao. Je kwa mwalimu yeyote wa wakati ule angefanya nini au tunaweza kujiuliza , angefanya nini kiongozi yeyote yule kwa kuona kuwa maneno yake na karama yake vinavutia umati na kuongeza umaarufu huo? Baba Mtakatifu Francisko amesema, inajitokeza hata leo hii, hasa kwa kipindi kigumu binafsi, na kijamii, tunakumbwa zaidi na hisia za hasira au tunaogopa tishio fulani la wakati wetu ujao, na kugeuka kuwa waathirika na hivyo kukugubikwa na wimbi la hisia na tunajikabidhi kwa wale ambao kwa ulaghai wao wanajifanya kutaka kusuluhisha hali, kwa kuchukua fursa ya hofu ya jamii na kuahidi kuwa “mwokozi” ambaye atatatua matatizo, wakati ukweli wanataka kuongezea kupenda kwao na nguvu zao.
Injili inasema kuwa Yesu hafanyi hivyo. Mtindo wa Mungu ni tofauti, kwa sababu yeye hatumii mahitaji yetu vibaya, hatumii kamwe udhaifu wetu kujikuza yeye mwenyewe. Kwake yeye ambaye hataki kudanganya kwa ulaghai na wala hataki kugawanya furaha, kwa sababu ya kuwa na haja ya kuwa na bahari ya watu. Hana utamaduni wa hesabu na wala kutafuta kukubaliwa, yeye si mwabudu sanamu wa mafanikio binafsi. Kinyume chake utafikiri ana wasi wasi na watu wanaomfuata kwa kujisahau na shauku rahisi. Badala ya kuvutiwa na umaarufu, Yeye anawaomba kila mmoja kung’amua na umakini sababu ambazo zinawafanya kumfuata na matukio ya ufuasi huo. Wengi wa umati uliokuwa unamfuata Yesu labda ulikuwa na matarajio kuwa Yeye angekuwa mkuu na ambaye angewaokoa dhidi ya maadui, mmoja wa ambaye angepata nguvu na angeweza kuwaweka sawa; au mmoja ambaye kwa kufanya miujiza, angeweza kutatua matatizo ya njaa na magonjwa. Ndio inawezekana kwenda nyuma ya Bwana kwa uhakika na sababu mbali mbali na baadhi inabidi kuzitambua zile za kiulimwengu.
Bwana anataka mwenendo mwingine. Kumfuata haina maana ya kuingia mahakamani au kushiriki maandamano ya kiushindi na wala kupokea uhakika juu ya maisha. Kinyume chake hata kubeba msalaba (Lk 14,27). Kama Yeye alivyobeba mzigo wake na wengine, kwa kufanya maisha kuwa zawadi, kuishi kwa kuiga upendo mkarimu na huruma ambayo Yeye alifanya kwa ajili yetu. Huu ni uchaguzi ambao unahitaji bidii yote ya maisha; kwa maana hiyo Yesu anatamani kuwa mfuasi, hachukui chochote cha upendo huo na wala upendo wa wapendwa zaidi na wala mali kubwa zaidi. Ili kuweza kufanya hivyo lazima kutamzama Yesu zaidi kuliko sisi wenyewe, kujifunza upendo, kuuchota kutoka katika Msalaba. Tunauona upendo huo ambao unajitoa hadi mwisho bila kipimo na bila mpaka. Papa Luciani alisema Sisi wenyewe ni kitu cha pembezoni cha Mungu wa upendo usio na mawio” (rej. Sala ya malaika wa Bwana 10 Septemba 1978). Kutokuwa na mawio maana yake jua halizimiki kamwe katika maisha yetu, linaangaza daima juu yetu na kumulika hata usiku wa kiza zaidi. Na kwa maana hiyo kuutazama msalaba, tunaalikwa katika uwanja wa upendo ule wa kutakasa mawazo yetu potofu juu ya Mungu na kujifungia kwetu, ili kupenda kama Yeye, na wengine, Kanisa, Jamii na hata wale ambao hawafikirii kama sisi, hadi kufikia maadui.
Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba Kupenda hata kama inagharimu msalaba wa sadaka, kuanzia kimya, kutoeleweka, upweke, kuwekewa vizingiti hadi kuteswa. Kwa sababu kama alivyokuwa anasema Yohane Paulo I kwamba ikiwa unataka kubusu Yesu Msulibiwa “Huwezi kufanya hivyo hadi unapojikunja juu ya msalaba na kuacha huchomwe angalau na mwiba wa taji ulioko juu ya kichwa cha Bwana ( Rej. Katekesi ya tarehe 27 Septemba 1978). Upendo wa kina na miiba yake yote na sio mambo yanayofanywa nusu nusu, ya kujipendelea au kuishi kwa wasiwasi. Ikiwa hatutazami juu, ikiwa hatuthubutu, ikiwa tunaridhishwa na imani kama maji juu ya waridi, Yesu anasema:“ sisi ni kama yule anayependa kujenga mnara lakini hakuhesabu vizuri zana za kuweza kufanya hivyo; anajenga na baadaye hana uwezo wa kumaliza kazi (Rej Lk 14,29). Baba Mtakatifu Francisko amesema ikiwa kwa sababu ya kuogopa kushindwa, tunakataa kujitoa, tunaacha mambo bila kumalizika, kama vile uhusiano, kazi, uwajibikaji ambao tumekabidhiwa, hata imani. Kwa maana hiyo tunaishia kuishi nusu nusu bila kufanya kamwe hatua stahiki na msingi, bila kutua, bila kuthubutu kwa ajili ya wema, bila jitihada za kweli kwa ajili ya wengine. Yesu anatutaka tuishi Injili na tunaalikwa katika kuishi maisha na wala sio nusu nusu bali kwa kina.
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema Mwenyeheri Mpya alihisi kwa namna hiyo furaha ya Injili, bila wasi wasi, akipenda hadi mwisho. Kwa kujivika umaskini wa mfuasi, ambaye s tu kuachana na mali, lakini hasa kushinda vishawishi vya kujiweka mbele , katikati na kutafuta utukufu wake. Kinyume chake, kwa kufuata mfano wa Yesu alikuwa mchungaji mpole na mnyenyekevu. Alijifikiria mwenyewe kama mavumbi ambayo Mungu alikuwa amestahili kuandika. Kwa maana hiyo Papa Yohane alikuwa anasema “Bwana alihimiza sana ; muwe wanyenyekevu. Hata ikiwa mlifanya mambo makubwa; semeni sisi ni watumishi wasio na faida ( Rej Katekesi 6 Septemba 1978).
Baba Mtakatifu Francisko amesema mwenyeheri mpya aliishi namna hiyo, katika furaha. Na kwa tabasamu Papa Luciani aliweza kufikisha wema wa Bwana. Ni vizuri kuona Kanisa lenye uso wa furaha, uso uliotulia, uso wa tabasamu ni zuri, Kanisa lisilofunga milango yake kamwe, lisiloumiza mioyo, lisilolalamika wala kuweka kinyongo, halikasiriki, lisilo na uvumilivu, halijionyeshi kwa njia mbaya, halina shida, lisilo na majuto kwa siku za nyuma, kwa kuangukia nyuma. Papa amesema “Tuombe kwa baba na kaka yetu, tumwombe atupatie "tabasamu la roho", lililo wazi, lisilodanganya: tabasamu la roho; tuliombe, kwa maneno yake, kile ambacho yeye mwenyewe alikuwa akiomba. Na kusema kwamba: “Bwana, nichukue kama nilivyo, pamoja na kasoro zangu, pamoja na mapungufu yangu, lakini nijalie niwe vile unavyonitaka”. (Re.j Katekesi 13 sSeptemba 1978),amehitimisha.