Papa:kuna mabadiliko ya ziara huko Matera.Kard.Zuppi:jitihada kwa raia ni kwa Mkristo!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, Kardinali Matteo Zuppi, ametoa maoni yake juu ya mabadiliko ya ziara ya Dominika 25 Septemba 2022. Kwa mujibu wa ofisi ya Vyombo vya habari Vatican mnamo 6 Septemba kuwa kardinali amesema: “Tunamshukuru sana Baba Mtakatifu kwa nia yake kubwa ya kupeleka mbele muda wa ziara yake ya kichungaji huko Matera katika hitimisho la Kongamano la Ekaristi Takatifu la Kitaifa la 27, katika siku muhimu sana kwa nchi yetu, iliyoitwa kubuni mustakabali wake kwa njia ya kura”.
Ratiba ya awali na mpya
Katika ratiba ya tarehe 8 Julai iliyopita, ilikuwa inaonesha ratiba juu ya liadhimisha misa saa 4.00 kamili na baadaye kutembele kurudi Vatican iliyokuwa impangwa saa 6.30. Kwa mujibu wa ratiba mpya , baada ya kutua Papa Francisko atakaribishwa muda wa saa 2.45 asubuhi katika Uwanja wa Manispaa uitwao XXI Settembre, ambapo saa 9.00 ataongoza Misa itakayofungwa kwa sala ya Malaika wa Bwana. Misa inatarajiwa kumalizika saa 5.00, ambapo Papa Francisko ataaga mamlaka itakayokuwa imekaribisha, baadaye atakwenda kwa gari hadi kiwanja cha Shule ya Riadha ili kuondoka mapema, saa 5.15 asubuhi kurudi Vatican mida ya 6.45 mchana.
Kanisa ni kwa ajili ya uhuru wa dhamiri
Akikumbuksha juu ya jitihada kwa raia kwamba ni sehemu muhimu ya maisha ya Kikristo, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia( CEI) amesisitiza kwamba “kupiga kura ni haki na wajibu wa raia wote. Kanisa ni kwa ajili ya uhuru wa dhamiri, hakika si kwa ajili ya uhuru wa kutojali”. Kwa njia hiyo Kardinali Zupi anatoa shukrani kwa Papa Francisko kwa ishara yake ya tahadhari ambayo itawawezesha wajumbe wa majimbo yote ya Italia waliopo Matera kurejea miji yao kwa ajili ya mafao ya muda wa kuweza kupiga kura”.