2022.09.19 Papa alikutana na Washiriki maaskofu wapya wa Kozi ya Mafunzo iliandaliwa na Baraza la kipapa la Maaskofu na kwa Makanisa ya Mashariki. 2022.09.19 Papa alikutana na Washiriki maaskofu wapya wa Kozi ya Mafunzo iliandaliwa na Baraza la kipapa la Maaskofu na kwa Makanisa ya Mashariki.  

Mwaliko wa Papa kwa maaskofu wapya:wawe wachungaji karibu na maskini

Jumatatu Septemba 19 Papa Francisko alikutana katika Jumba la Kitume na maaskofu waliowekwa wakfu hivi karibuni wapatao 200 ambao walishiriki hatua ya pili ya kozi ya mafunzo katika Taasisi ya Regina Apostolorum iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na Makanisa ya Mashariki.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Ulikuwa ni mkutano wa kawaida kwa wote kukaa pamoja  katika mduara ambao ulijikita katika shuhuda, ushauri na kutia moyo ili kuhudumia maskini zaidi. Katika siku zilizofuata za kujifunza jinsi ya kuwa maaskofu, changamoto gani za kukabiliana nazo, ni mada gani za kupeleka mbele. Maaskofu wapya wapatao 200 walioshiriki katika kozi ya malezi iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na kwa Makanisa ya Mashariki  ambao walipokelewa asubuhi ya tarehe  19 Septemba 2022 na Baba Mtakatifu Francisko katika Ukumbi wa Clementine mjini Vatican. Mkutano huo, ambao Kardinali Marc Ouellet Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu alikuwepo, ulihifadhiwa ili kuruhusu mazungumzo huru kati ya Papa na maaskofu (wengi wao kutoka  Amerika ya Kusini),  katika muktadha huo  wale walioshiriki katika hatua ya  pili ya kozi, iliyofanyika tangu 12-19 Septemba katika Taasisi ya Ateneo Regina Apostolorum huko Roma.

Papa na Maaskofu wapya washiriki wa Kozi ya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na la Makanisa ya Mashariki
Papa na Maaskofu wapya washiriki wa Kozi ya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na la Makanisa ya Mashariki

Hatua ya kwanza iliyofunguliwa na Misa iliyoadhimishwa na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, ilifanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Septemba 2022 iliyopita (mgawanyiko uliundwa kwa idadi kubwa ya washiriki  kutokana na vikwazo vya Uviko). Papa Fransisko alikuwa amepokea washiriki katika kozi hiyo katika Chumba cha Clementine  ya utamaduni ulioanza mnamo mwaka 2000 chini ya upapa wa Yohane Paulo II na kuendelea kufanyika kila  mwaka ambapo kwa mwaka huu mada  ilikuwa ni:  "Kutangaza Injili katika mabadiliko ya zama na baada ya janga: huduma ya askofu”

Hata katika hali hiyo hapakuwa na hotuba iliyoandikwa, lakini  yalikuwa ni mazungumzo ya faragha kwani askofu msaidizi,Angelo Ademir Mezzari, wa Mtakatifu Paulo aliripoti katika ofisi ya uhariri kwa lugha ya  Kireno. Kwa upande wake alisema kwamba Baba Mtakatifu, aliwakaribisha wale waliohudhuria kwa ujumbe, yaani, bila kusahau ukaribu na maskini, akifahamu kwamba kila kitu kimeunganishwa na kila kitu kinahitaji huduma katika sayari hii. Kisha alitaka kuwasikiliza wageni wake moja kwa moja, hisotria  zao, maoni yao na maombi yao. Mkutadha huo ulidumu kama saa moja na nusu. Mpango huo huo ulirudiwa tena katika mazingira ya "kisinodi", kama ilivyotangazwa na askofu wa Brazil Maurício da Silva Jardim ambaye tarehe 23 Oktoba atakabidhwa jimbo la  Rondonópolis-Guiratinga.

Papa na Maaskofu wapya washiriki wa Kozi ya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na la Makanisa ya Mashariki
Papa na Maaskofu wapya washiriki wa Kozi ya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na la Makanisa ya Mashariki

 

Kwa mujibu wake alisema kukaa kisinodi ndiyo ilikuwa  hali ya juma la kazi katika  Taasisi ya Regina Apostolorum, ambapo, kwa nuru ya  uadilifu wa Papa Francisko, wasemaji waliweka mada katikati na kutoa nafasi katola mkutano, kujieleza, na kuibua maswali na matatizo madhubuti ya ukweli, kama vile njaa, vurugu, ukosefu wa usawa wa kijamii, uhamiaji, migogoro ya kisiasa na kiafya, maadili na masuala ya kijamii duniani kote" Maaskofu wapya 19 wa Brazil waliweza kuwafahamisha washiriki wa kozi hiyo na Papa, hata matatizo makubwa ambayo yanaharibu uso wa Amazonia, kama vile uchimbaji madini, unyonyaji, ukataji miti ovyo.

Papa na Maaskofu wapya washiriki wa Kozi ya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na la Makanisa ya Mashariki
Papa na Maaskofu wapya washiriki wa Kozi ya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na la Makanisa ya Mashariki

Wakati wa kozi hiyo, maandishi ya Papa  Francisko yakaririwa kwa kina hasa Wosi wa  Amoris laetitia, Fratelli tutti na Laudato si ', na baadhi ya mambo muhimu ya upapa wa Jorge Mario Bergoglio kama vile familia na udugu wa ulimwengu mzima kupitia uhamasishaji wa binafamu fungamani,. Ilikuwa ni fursa ya   kutembea pamoja katika nyanja tofauti, kututia moyo kuwa 'wachungaji wa watu' na kutoa vipengele vya kutenda katika majimbo yetu, kwa kanuni iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko wa kimisionari, Kanisa la Sinodi, umoja na ushiriki”. Kundi jingine la Maaskofu lilipokelewa katika Mkutano wa Jumamosi iliyopita tarehe 17 Septemba  na kwamba wachungaji wa nchi za kimisionari  walioshiriki katika semina nyingine ya malezi jijini  Roma, iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Katika mazungumzo ya wazi, na ya faragha,  aliwahimiza maaskofu kuona ukaribu wa wachungaji, kwanza kabisa na Mungu, kisha ushirika kati ya maaskofu na mapadre, bila kuwasahau waamini.

Papa na Maaskofu wapya washiriki wa Kozi ya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na la Makanisa ya Mashariki
Papa na Maaskofu wapya washiriki wa Kozi ya iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu na la Makanisa ya Mashariki

Kama ilivyoripotiwa kwa wenzao katika ofisi ya uhariri ya lugha ya Kihispania na Msimamizi wa Kitume wa Caroní huko Venezuela, Askofu Gonzalo Ontiveros, maaskofu walipata fursa ya kushiriki uzoefu wao wa kazi ya kimisionari na Papa, hivyo kumpa Baba Mtakatifu mwanzo wa kutafakari yake. Kwa upande wa Papa Francisko alisisitiza umuhimu wa maombi katika huduma ya kiaskofu kwa sababu askofu asipoomba, anamwacha Mungu na hunyauka.  Pia, alisema  Ontiveros, kwamba Papa alitaka umoja zaidi kati ya maaskofu kama ndugu katika uaskofu na ukaribu wa karibu na mapadre, washiriki, jumuiya za parokia kwa uwajibu kwa wote. Kuwa waangalifu kwa mahitaji yao. Miongoni mwa mapendekezo hayo, yapo pia ya kujiepusha na mbwembwe za kimbembele na kujirejea binafsi na kutoka katika kugeuza imani ambayo ni tofauti na “uinjilishaji” unaopaswa kufanywa kwa mtindo wa Yesu.

Mazungumzo ya Papa na maaskofu wapya 19 Septemba 2022
20 September 2022, 16:16