Papa:Tufanye kazi pamoja kwa ajili ya mkataba wa amani na haki duniani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika ujumbe uliotiwa saini ya Kardinali Pietro Parolin kwa niaba ya Papa ametuma ujumbe kwa Mkurugenzi wa (Shirika Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Michezo (UNESCO) katika Siku ya Kimataifa ya Kusoma na Kuandika duniani Septemba 8, kwamba: “Baba Mtakatifu Francisko aliniomba niwatumie salamu na kuwatia moyo wale wote ambao wako ndani ya UNESCO wakifanya kazi kwa ajili ya kufuta ujinga”. Kwa maana hiyo Papa anawatakia mafanikio mema katika tafakari na kazi ya siku hii, ili iweze kuleta matunda mema kwa ajili ya kubadilisha nafasi za kudumu za kujifunza.
Mkataba ambao unauhisha michato ya elimu
Dunia ambayo tunayoishi inaendelea na mabadiliko, ambayo si tu kwa mtazamo wa kiutamaduni lakini hata kibinadamu na kila mabadiliko yanapalekea kusindikizwa na mchakato wa elimu. Kwa maana hiyo ni lazima kujenga kijiji cha kuelimisha mahali pa kushirikisha, katika utofauti, jitihada za kuunda mtandao wa mahusiano ya kibinadamu na iliyo wazi. Kardinali Parolin anabainisha juu ya dharura zilizoelezwa na Papa Francisko juu ya ulazima wa kuweka muhuri ambao unatoa uhai wa mchakato wa elimu rasmi na isiyo rasmi, ambayo haiwezi kutozingatia kuwa katika ulimwengu wote kwa hakika umefungamana na kwamba ni lazima kutafuta kwa mujibu wa elimu safi ya mwanadamu na mitindo mingine ambayo inazingatia uchumi wa kisiasa, ukuaji na maendeleo.
Ombi la Papa kusoma na kuandika kwa muktadha wa mwanadamu
Kama vile Papa Yohane Paulo II alivyokuwa amefanya tayari mnamo tarehe 2 Juni 1980, alipokuwa akihutubia UNESCO, Kardinali Parolin anakumbuka ombi la Papa Francisko la "elimu na kusoma na kuandika ambalo lengo lake kuu ni ujenzi wa ulimwengu unaoendana na mwanadamu, ambao matamanio yake ya kimwili na kiroho lazima kuzingatiwa, na ambayo lazima ionekane"katika uhusiano wake na wengine, na jamii, na maumbile na mazingira. Ni suala la kufikiria pamoja juu ya elimu inayozingatia vipengele vyote vya mtu, uhusiano kati ya vizazi, kati ya familia na jamii. Muungano kati ya wakazi wa Dunia na 'nyumba ya kawaida ya pamoja ambayo lazima tuilinde na kuiheshimu. Muungano unaozalisha amani, haki na kukubalika kati ya watu wote wa familia ya kibinadamu, pamoja na mazungumzo kati ya dini, ujumbe unasomeka.
Kuelimisha ni tendo la matumaini na walimu wanahitaji kuungwa mkono
Katika ujumbe huo, Katibu wa Vatican anasisitiza kwamba kwa upande wa Papa elimu siku zote ni kitendo cha matumaini kinachotualika kushiriki na kubadilisha mantiki tasa na ya kupooza ya kutojali kuwa mantiki yenye uwezo wa kukaribisha mali yetu ya pamoja. Ikiwa lengo hili halingekubaliwa, nafasi za elimu zingekuwa hatarini kukosa miadi na historia. Hali ya kazi ambayo walimu wengi na waelimishaji duniani kote wanafanya kazi zao haipaswi kupuuzwa, kiukweli mara nyingi ni hali hatari ambazo huwazuia hasa vijana wanaotaka kujitolea kufundisha. Ujumbe wa Papa Francisko unahitimisha kwa matumaini kwamba juhudi zinazoendelea za kubadilisha mfumo wa elimu zinaweza kusaidia kujenga ustaarabu wa maelewano, umoja, mshikamano, udugu na amani ya kudumu.