Papa ulimwengu unaotikiswa na vita vyenye hatari ya kuongezeka kwa nyuklia
Na Angella Rwezaula - Vatican
Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake Alhamisi 8 Septemba 2022 amewakaribisa wote na kumshukuru kila mmoja aliyefika hata kwa matatizo makubwa, Wawakilishi kipapa kutoka ulimwengu mzima ambao wanafanya mkutano ulionaza tarehe 7 hadi 10 Septemba 2022 mjini Vatican. Hawa ni Wawakilishi wa Kipapa katika mataifa ulimwenguni kote ambao hufanya mkutano wao kila baada ya miaka mitatu. Kundi hili linawakilisha Mabalozi 91, Mabalozi 6 wa Kudumu wa Vatican katika Mashirika ya kimataifa, 5 hawakufika kutokana na matatizo ya kiafya au vizingiti vingine. Papa amekumbusha jinsi ambavyo imepita miaka mitatu tangu walivyofanya mkutano wao wa mwisho. Dhoruba la Janga la Uviko -19 likalazimisha vizingiti fulani vya kila siku na katika shughuli zao za kichungaji. Lakini sasa utafikiri hali ngumu imepungua na shukrani kwa Mungu wameweza kukutana. Lakini kwa bahati mbaya Papa Francisko amebainisha kuwa Ulaya na ulimwengu mzima kuna mkumbo wa vita hasa vibaya pia kwa ukiukwaji wa haki za kimataifa, unahatarisha kuongezeka kwa nyuklia, ziwe nzito na matokeo yake ya kiuchumi na kijamii.
Ni vita ya Tatu ya dunia iliyogawanyika vipande ambamo wao ni mashuhuda katika maeneo ambayo wanatenda utume wao, ameeeleza Papa. Papa Francisko ameshukuru yote kwa kile ambacho Uwakilishi wa Kipapa umefanya na unaendelea kufanya katika hali hii ya mateso. Wao wamepeleka kwa watu na kwa Makanisa ukaribu wa Papa; wao wamekuwa kitovu cha kufikiwa wakati wa kukata tamaa na mahangaiko. Katika muktadha huo, Papa amependa kukumba pamoja na wao Mabalozi Joseph Chennoth, na Askofu Mkuu Aldo Giordano ambao wameaga dunia hivi karibuni wakati wa utoaji wa huduma yao; kama pia marehemu ambao tayari wamekufa kwa miaka mitatu ya mwisho. Hawa ndugu wapendwa, Papa amesema wametangulia katika safari na wanatoa mwaliko wa kutazama mbele na huko juu.
Kwa mtazamo huo, Papa amewaalika kwenda mbele katika kazi yao, katika leo ya Kanisa na leo ya ulimwengu kwa kutegemea neema ya Bwana. Kama Kanisa wote wanajibidisha katika mchakato wa kisinodi ambao unataka kufanya kukua katika watu wa Mungu hasa katika ukuu wa kisinodi. Hata mabalozi Papa amewambia kuwa wamehusishwa katika kutoa mashauri. Na baadaye kuna matarajio ya Jibilei ya 2025, ambayo tayari imeanza kuandaliwa. Kama Curia Roma, Papa amesema wameanza kutumia Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium: ambayo ilizaliwa kwa njia ya mchakato wa karibu miaka 9, na sasa inaomba muda hata wa kuweza kuingia ndani mwake, kwa mamlaka kamili. Baba Mtakatifu Francisko, amewambia kwambwa wakabidhi mkutano wao na nia zao zilizomo ndani ya moyo katika maombezi ya Bikira Maria, hasa katika Siku Kuu yake ya Kuzaliwa. Mara baada ya kumaliza hotuba yake amewamba nao kama wanayo maswali na mashauri ya kuweza kushirikishana naye.