Tafuta

2022.08.24 Katekesi ya Papa katika ukumbi wa Paulo VI 2022.08.24 Katekesi ya Papa katika ukumbi wa Paulo VI 

Papa:Suluhisho la vita nchini Ukrane ni kwa njia ya mazungumzo

Yamechapishwa ndondoo za mahojiano kati ya marefu ya Papa Francisko na mwandishi wa habari Bi Avillez ya mnamo Agosti 11 iliyopita katika TVI/CNN Ureno yatakayo tolewa yote usiku.Kati ya mada zilizokabiliwa ni 'Siku ya vijana ya 2023,''Vita nchini Ukraine' na nyanyaso za kijinsia katika muktadha wa kikanisa.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Mazungumzo ni magumu lakini ni kwa njia ya mazungumzo tu inawezekana kwenda mbele. Amesema hayo Papa Francisko akizungumza kuhusu vita nchini Ukraine, katika mahojiano yaliyofanywa na Bi Maria JoÆo Avillez mnamo tarehe 11 Agosti iliyopita katika televisheni ya TVI/CNN Ureno ambapo alikuwa ametangaza kuwa na mazungumzo kwa njia ya simu  aliyokuwa afanye  siku ya tarehe 12 Agosti na Rais wa Ukraine Bwana Zelensky. Katika swali kuhusu suala la uwepo wa safari ya kwenda Kiev, alielezea kuhusu ushauri aliokuwa amepata wakati huo kutoka kwa daktari kuhusu tatizo la kusafiri hadi ziara yake ya kwenda Kazakhstan inayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 13-15 Septemba 2022.

Mapumzisho ya goti kabla ya ziara ya kwenda kazakhistan

“Kwa sasa siwezi kwenda kwa sababu baada ya kutoka nchini Canada, goti linapumzika kidogo na daktari alinikataza”. Lakini kwa upande wa vita, kuna jitihada zisizoisha kwani: "Ninasindikiza kwa uchungu na kwa sala kila kitu ambacho ninaweza. Lakini hali halisi kiukweli ni mbaya”, alidhibitisha Baba Mtakatifu, ambaye aliokumbusha juu ya tendo la kutuma huko Kiev wawakilishi mbali mbali ili kufanya uwepo wake kwa mtindo huo wa ukaribu. Baadaye kuna hatua nyingine kuhusu nyanyaso katika Kanisa, jinamizi ambalo Baba Mtakatifu alibainisha kuwa anapaswa kuendelea na jukumu hilo hadi mwisho. “Kuhani hawezi kuendelea kuwa padre ikiwa analawiti. Hawezi. Ni mgonjwa au muhalifu, yeye yupo kwa ajili ya kuwapeleka waamini kwa Mungu na hawezi kuwapo kwa ajili ya kuwaharibu kwa jina la Mungu”.

Kesi za unyanyasaji

“Kila kesi ya unyanyasaji inanifanya niteseke, elielezea  ​​lakini lazima tukabiliane nayo: Kanisani, katika familia, katika utamaduni mzima wa unyanyasaji, kwa bahati mbaya sana, ambayo kwa hali yoyote haipaswi kufichwa. Ni mateso, machafuko yoyote ya unyanyasaji ninayojua, lakini mateso lazima yakabiliwe na Mimi ninahusika nayo ili kwamba isitokee tena. Useja hauna uhusiano wowote nayo, kwa sababu pia hutokea katika familia, na ni jambo la kishetani. Wanaume na wanawake walioitwa kutumikia, kuunda umoja, kuchangia ukuaji na zaidi ya yote kuwaleta vijana kwa Mungu, badala ya kuharibu maisha yao. Ushetani ni kwamba wagonjwa hutumia nafasi zao kukidhi mahitaji yao ya kibinafsi.

Siku ya vijana Ureno 2023

Nafasi ya kutosha ilitolewa kwa mada ya vijana na maandalizi ya Siku ya vijana (WYD) ambayo itafanyika nchini Ureno mnamo Agosti 2023. Papa  Francisko alihakikishia uwepo wa Papa kwa mzaha: kwamba “Nadhani ninakwenda. Papa anakwenda. Labda Francisko aende au Yohane  XXIV aende, lakini Papa anakwenda”. Tukio, lile la Siku vijana duniani  pia  ni la upatanisho katika wakati mgumu kwa Kanisa la Ureno, lililohusishwa na historia ya unyanyasani. Papa Francisko alizindua kwa upya ukaribu na mazungumzo. Na Hatimaye, aliwasifu vijana kwa ubunifu wao, akisisitiza haja yao ya kusikiliza na kujibu. Papa alisimulia mkutano aliofanya huko Roma na vijana wa lugha tofauti na pia imani tofauti: ihari yao  daima ni utajiri hata wakati wanashambulia au kukosoa kwa dhati na kamwe sio unafiki.

Msingi wa ukuaji wa vijana ni mazungumzo kati ya vizazi

Msingi wa ukuaji wao ni mazungumzo kati ya vizazi kwani kwa mara nyingine tena Papa  Francisko amerudia kwamba siku zijazo zinaanzia kwenye mizizi. Na baadaye Siku ya vijana ( WYD) pia ni kama wakati wa upatanisho na Kanisa la kitaifa: kwa ukaribu kuna mazungumzo na upatanisho unaweza kukanda upata upatanisho. Papa  Francisko pia anahusika na Ureno kwa kujitoa kwake kwa Bikira wa Fatima: Bikira wa ukimya, alifafanua huku akikumbuka ibada ya Maria aliyojifunza katika familia na kwa hiyo sala ya Rozari iliyofanywa tangu utotoni. Kwa nia hiyo njia ya kibinafsi ya Papa ya kuomba, iliyofanywa amekiri  pia ya kukengeushwa fikira,  lakini alisema “Mungu hababaiki na hii inanifariji”. Kuomba kunamaanisha kuwa katika uwepo wa Mungu na kumwacha azungumze, aliongeza Papa Francisko kwa maana hiyo uhuru kama sehemu muhimu na kutegemea kile ambacho Roho Mtakatifu anachovuvia, ambacho ni maelewano na maisha.

Mageuzi ya Kanisa 

Mtazamo mwingine wa kazi ya  kuleta mageuzi ndani ya Kanisa  aliyotaka kwa motu proprio Traditiones Custodes na Barua ya Kitume Desiderio desideravi, na baadaye  jukumu la wanawake. Papa Fransisko amebainisha  kwamba, Liturujia ambayo ni kazi kuu ya Kanisa ya kumwabudu na kumsifu Mungu, haina budi kuadhimishwa vyema na hivyo kuwa na heshima. Kisha kuhusu  uwepo wa wanawake katika nyanja mbalimbali, katika Curia Romana kama katika utawala wa mji wa Vatican alieleza kwamba si mtindo wa kike bali kitendo cha haki kwa sababu wanawake wametupwa kando kiutamaduni. Wabatizwa wote wana haki ya kufanya kitu kwa ajili ya Kanisa. Hapa waliobatizwa wote wana nafasi. Ni jambo ambalo sikuligundua, lakini ambalo limekuwa likiendelea kwa miaka 20 au 30 na linatekelezwa polepole”alisisitiza Baba Mtakatifu. Mifano inatokana na mahojiano ya kibinafsi au uzoefu wa zamani, ili kusisitiza kwamba wanawake wana njia tofauti ya kutazamia mambo kwa sababu wanafikiri tofauti. Na kisha mwanamke ndiye mwenye jukumu la kuendelea kuwa mama wa Kanisa na hivyo kuwachagua maaskofu, ni vyema wawepo wanawake wanaofikiria jinsi maaskofu wanapaswa kuwa”.

Nafasi ya wanawake katika Kanisa

Kulingana na Papa, inafaa kwa wanawake pia ile sifa ya Mungu ambayo ni huruma. Kwa maana hiyo Papa amerudia hayo alipokumbuka alipokuwa Buenos Aires alipotembelea magereza na kuona mistari ya akina mama wakingoja kuingia humu kwa ajili ya kuwaona watoto wao, hawakukataliwa kamwe kwa sababu walikuwa mwili wa nyama zao. Msukumo huo unatoka kwa wahusika wakuu wa kike wa Bibilia: Judith, ambaye alitetea watu wake kwa ujasiri, na ni wazi Maria, mwanamke bora ambaye ndani yake kuna nguvu, huduma, umama”. Papa Francisko pia aliulizwa kuhusu ucheshi na kusisitiza kwamba anapendelea sala maalum: Kwa zaidi ya miaka 40 nimekuwa nikiomba kwa hisia ya ucheshi ya Mtakatifu Thomas More. Ninasema maombi haya. Ninaomba neema hii, hali ya ucheshi ”. Ni sala inayoanza hivi: “Bwana, nipe usagaji chakula vizuri na pia kitu cha kuyeyusha”.

Sinodi sio bunge bali ni mahali pakufayia mang’amuzi

Katika mahojiano kuna nafasi pia ya kutoa maoni juu mchakato wa  sinodi unaofanywa na Kanisa, amapo Papa amebainisha kwamba  sio aina ya bunge, lakini ni mahali pa kufanyia mang’amuzi  ambamo Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa kuunda maelewano kutoka utofauti. Njia ya mchakato iliyowekwa kwa kuanzishwa na  Mtakatifu Paulo VI, ambayo Kanisa limekuwa likijifunza katika miaka 50 iliyopita. Njia ambayo hakuna ukosefu wa migawanyiko, ambayo itaimarishwa tu mwishoni, na ambayo, kati ya wale wanaosukuma mbele na wale wanaorudi nyuma, Askofu kama Mchungaji Mwema ataweza kubaki ulimwengu kuhusiana na watu watakatifu na waamini wa Mungu”, wakiepuka upotovu wa ukleri. Hata hivyo, katika nyanja ya kiekumene na dini mbalimbali, Papa Francisko alisisitiza tena kwamba mazungumzo ni silaha inayoshinda, kwani  katika mazungumzo - inaeleweka kuwa anajua jinsi ya kusikiliza na si mchezo wa usawa, mtu hawezi kupoteza na Mungu anatenda.

Maisha ya Papa 

Kuhusu maisha ya Papa yalivyo, jinsi anavyotumia likizo yake na wapi anapata nguvu ya kuamini ushindi wa wema dhidi ya uovu ambao unaonekana kushinda leo hii, ni tafakari ya mwishoni mwa mahojiano. Kwa maana hiyo anatumia likizo yake ya kiangazi jijini Vatican kusoma, kusikiliza muziki na kusali. Wagner na opera ni mapendeleo ya Papa Franisko katika siku zake za kila siku zinazoanza mapema, saa nne asubuhi, na kuisha saa kumi jioni. Nguvu ya kuamini mema inatoka kwa Yesu, Bwana wa historia: daima zama zimekuwa na nguvu na udhaifu, zimeona ngano na magugu kukua pamoja, Papa amesisitiza. Hatimaye, ombi la mwisho la neno la kumulikia njia ya Kanisa la Ureno katika mkesha wa Siku ya Vijana Duniani (WYD), jibu la Papa Fransisko linafika: msijifunge, angalieni zaidi, weka upeo  kwa upana na mpanue yenu

(Sasisho la mwisho ni saa 3.kamili  tarehe 6 Septemba 2022).

05 September 2022, 20:20