Papa:watunze watu na si rasilimali ili kutoanguka katika biashara ya upendo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 5 Septemba 2022 amekutana na uwakilishi wa Caritas Hispania na kueleza furaha ya kukuta nao uwakilishi wa huduma ya kikanisa ambayo ni Caritas Hispania, zaidi kukutana katika fursa ya kuadhimisha miaka 75 ya Mfuko wa Taasisi hiyo ambayo ilipata mafaniko makubwa ukilinganisha na jamii ya hispania licha ya imani na itikadi zao, kwa sababu amesema hisani- upendo ni msingi zaidi wa kuwa binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, kwa maana hiyo ni lugha ambayo inatunganisha wote zaidi. Baba Mtakatifu Francisko anaamini kwamba hilo ni jambo muhimu sana ambalo linaturuhusu kuona kwa namna ya upendo wa kimungu, unavyoweza kuwa mtindo wa kazi ya Caritas.
Kiukweli ikiwa Kristo anatoa mwaliko wa kuwa na umoja na Mungu na ndugu, kazi yao moja kwa moja ile ya kuweza kuupata umoja ambao kwa mara nyingine umepotea kwa watu na katika jumuiya. Kwa upande wa Baba Mtakatifu utafikiri hili ni jambo kubwa mno ambalo tayari wanapendekeza, hasa wanapokumbana na baadhi ya changamoto katika jitihada hizo. Awali ya yote kuna haja ya kufanya kazi ya kuanzisha na uwezo na nguvu za kusindikiza mchakato huo. Kwa hakika kuhisi kuhusika na kufanya kufikia malengo yaliyopangwa, lakini si tu kuona matokeo, bali kujiweka mbele katika mtu aliyevunjika moyo, hasiye pata nafasi yake na kumkaribisha, kumfungulia njia za kuweza kujirudi kwa namna ya kwamba, anaweza kujipata binafsi na kuwa na uwezo licha ya vizingiti vyake na vyetu, kwa kutafuta nafasi yake na kujifungulia wengine na Mungu.
Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amesema ni lazima kuwa na pendekezo la changamoto ya pili ili kutimiza kwa dhati azimio msingi. Haitoshi ishara ambazo zinatafuta kutoka nje, lakini zile ambazo zina hamasisha mabadiliko ya kweli ya watu. Katika parokia moja ya Hispania, Papa amesema kulikuwa na watu wanaomba Paroko kama angewapa bahasha, yaani ikiwa wangeweza kutimiza kile kinachowezekana cha kukidhi maisha na ambacho kiukweli kilikuwa kinawafanya kufunga mahitaji na kuzuia kuwa na maendeleo yao. Lakini Yesu anasema wazi kwa njia ya maisha yake na huduma yake kwamba haitoshi kutoa lakini pia kijibidisha.
Upendo unahitaji daima kutoa kwa moyo katika maisha binafsi. Na hiyo itakuwa na maana mbali na matendo ya dhati, ikiwa itamfanya mtu kukuta mlango ulio wazi wa maisha mapya. Kwa kufikiria Injili ya Yohane, Papa Francisko amesema iwapo tungetafutwa na kusifi watu kwa sababu, watu walikula mkate na kwa sababu hiyo tukajisifu kama mfalme, tungeweza kukwamisha ujumbe wa Yesu. Badala yake Bwana anapendekeza kwetu kuwa chachu ya ufalme wa haki, wa upendo na amani. Anaomba wote kuwa kama wale ambao wanawapatia chakula watu wake mkate ule uliomegwa na ambao ni Yeye mwenyewe na kutufundisha kuwa ‘anayetaka kweli kuwa mkubwa lazima awe mtumishi wa wote’.
Changamoto ya mwisho inayounganisha na ile ya kwanza ni kutafuta kuwa mkono wa matendo ya jumuiya ya kikanisa. Kanisa kama mwili wa Kristo, kadiri muda unavyopita wa historia ya matendo yake, ndivyo kwa namna hiyo Caritas inapendekeza kuwa kama mkondo iliyonyooka na ambao ni wa Kristo hasa tunapotoa kwa yule mwenye kuhitaji zaidi ya sisi, na wakati huo huo, tunaruhusu kumshika Kristo anapotualika katika mateso ya ndugu. Kuwa kama mkondo haina maana kiurahisi uratibu uliopangwa zaidi wa rasilimali, au nafasi ambayo unaweza kupakua uwajibikaji wa utume huo nyeti wa kikanisa. Kuwa mkondo kuelewake hasa kama ile fursa ambayo wote tunapaswa kukaribisha ili kuweza kufanya uzoefu wa kipekee na wa lazima ambapo Bwana anatualika kwamba“ unataka kujua ni nani jirani? Nenda na wewe ufanye hivyo hivyo”.
Baba Mtakatifu ameomba wawe makini kwa rasimilia , wasiangukie kufanya makampuni makubwa ya upendo wa biashara, kwa sababu kuna makampuni barani Ulaya na ya kitaasisi yanafanya hivyo. Amewaomba kufanya kazi kama wito na sio kuajiriwa kwana amesema “Kuna vyama vya hisani ambapo asilimia 40, 50, 60 ya rasilimali inakwenda kulipa mishahara kwa wale wanaofanya kazi huko. Lazima kuwepo upatanishi mdogo na unawezekana. Ametoa onyo kwamba suala la kuita: “Njoo hapa, nitatoa wewe kazi katika Caritas ... ', hii sio nzuri”.Amehitimisha kwa kuwabariki na kuomba wasali kwa ajili yake.