Maneno ya Papa kwa mabingwa wa ‘Talla Baja’ kutoka Argentina
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu alikutana mjini Vatican, Jumatano tarehe 26 Oktoba 2022 na washindi wapya wa kwanza wa Kombe fupi la Ulaya, lililofanyika nchini Hispania. Katika maneno yake alisema ujasiri wao unawafanya watumie hata kile kinachoonekana kuwa hasi. Baba Mtakatifu aliwashukuru kwa ziara hiyo na kile ambacho wanakifanya sababu ni wajasiri. "Ujasiri wa kufungua njia mpya, ya uzoefu ambao unaweka kila kitu walicho nacho, na wanakifanya kwa furaha". Wao ni wajasiri na aliwaomba waendelee na ujasiri huo na wasiuache kamwe bali uwe mbele maishani mwa kila mtu jinsi alivyo.
Hiyo ni pamoja na maadili yao ya kiakili, kihisia, kimwili, kila kitu. "Katika maisha, mtu anaweza kuangalia mambo kwa njia mbili ya kwanza juu au chini. Yaani wapo ambao huwa wanakata tamaa na wengine wanakabiliana na lolote linalowatokea kwa kutazama chini. Papa amebainisha kwamba ni hatari gani na wanapata huzuni. Watu hawa kitu pekee wanachofanya ni kufikiria upeo wa uchungu. Na kuna wale wenye matumaini, kama watu hao ambao wanakabiliwa na kila shida kwa kuangalia juu. Kwa maana hiyo aliwasihi waendelee mbele kutembea kwa kile walicho nacho sasa. Hiyo ni kufadhili kila kitu, kukifanya mtaji hata kwa kile kinachoonekana kuwa hasi.
“Huu ni ukomavu wa kibinadamu. Na nimefurahishwa kuona kwamba mmechagua njia hii ya ukomavu na kiwango mlichofikia. Ni kweli kubwa sana. Ninawashukuru nyote kutoka moyoni mwangu kwa hilo. Mungu awabariki, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Na mniombee. Niombee nami ninafanya hivyo kwa ajili yenu. Papa kwa kuhitimishia aliwasalimia mmoja baada ya mwingine.