Papa Francisko:amani ni kilio kinachohitaji kusikilizwa!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Katika hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mkutano wa sala kwa ajili ya amani uliokuwa na kauli mbiu " kilio cha amani" akiwa na viongozo wa kikristo na Dini nyingine ulimwenguni Jumanne jioni tarehe 25 Oktoba 2022 katika magofu jijini Roma amewashukuru wote walioshiriki katika mkutano huo. Amekuwa na utambuzi wa viongozi wa kikristo na madhehebu mengine kwa kuuhishwa na roho ya udugu ambao unauhisha historia ya kwanza iliyopendwa na Mtakatifu Yohane Paulo II huko Assisi miaka 36 iliyopita. Kwa mwaka huu, sala hiyo inakuwa ni kilio kwa sababu leo hii amani imekiukwa vibaya sana, imejeruhiwa na kukanyagwa na katika bara la Ulaya, yaani katika bara ambalo zamani katika karne iliyopita, ilifanya uzoefu wa janga kuu la vita mbili za ulimwengu na sasa ni vita ya tatu. Kwa bahati mbaya tangu wakati ule, vita havijakoma kamwe vya umwagaji damu na kufanya nchi ziwe maskini na katika wakati ambao tunaishi ni kwa namna ya pekee mgumu sana. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha jinisi ambavyo wameinua sala zao kwa Mungu ambaye daima anasikiliza kilio cha watoto wake wenye huzuni.
Amani imo ndani ya dini, katika maandiko yao na katika ujumbe wao. Katika ukimya wa sala, waliyofanya jioni, hiyo Papa amesema kwamba wamehisi kilio cha amani, amani iliyosongwa katika dini nyingi ulimwengini, iliyo nyenyekeshwa kwa vurugu nyingi, iliyokataliwa hadi watoto na wazee ambao hawakosi katika dharau hii mbaya ya vita. Kilio cha amani mara nyingi kinanyamazishwa zaidi ambapo katika marudio ya silaha, hata na sintofahamu. Amani imezuiwa na chuki ambayo inakua wakati wanaendelea kupigana. BabaMtakatifu Francisko akiendelea amesema: “Kila vita inaacha ulimwenguni mabaya zaidi ya yaliyokutwa humo. Vita ni kushindwa kwa sera za kisiasa na kibinadamu ambazo zimefanya aibu, kushindwa mbele ya nguvu za ubaya (Ft 261). Ni uyakinifu ambao unatokaa na uchaguzi wa uchungu sana wa karne ya 20 na kwa bahati mbaya hata katika sehemu ya karne ya 21. Leo hii kiukweli inaonekana kile ambacho kilikuwa kinaogopwa na kuwa hakuna aliyekuwa anataka kusikiliza, yaani utumiaji wa silaha za atomiki, ambazo zilipuliwa baada ya Hiroshima na Nagazaki, na zimeendelea kuzalishwa na kufanyiwa mazoezi na sasa zinatishia.
Katika hali hii ya giza, ambapo kwa bahati mbaya miundo ya wenye nguvu duniani haitegemei matakwa ya haki ya watu, mpango wa Mungu haubadiliki, kwa ajili ya wokovu wetu, ambao ni mpango wa amani na si wa bahati mbaya. ( Yer 29,11). Hapo ni kupata usikivu wa sauti kwa yule hasiye kuwa na sauti; hapo ni msingi wa matumaini kwa wadogo na maskini, kwa Mungu ambamo jina ni Amani. Amani ni zawadi yake na ambayo wameomba kwake. Lakini katika zawadi hiyo inapaswa kupokelewa na kukuzwa na wanaume na wanawake hasa kwa waamini wote. Baba Mtakatifu Francisko ameomba wasiambukizwe na mantiki iliyojaa vita; wasiangukie katika mtego wa chuki kwa adui. Ameomba kuweka moyo wa maono ya wakati ujao, kama lengo msingi la utendaji kibinafsi, kijamii na kisiasa kwa ngazi zote. “Tutatue migogoro kwa kutumia silaha ya mazungumzo”, Papa ameshauri.
Wakati wa mgogoro mkubwa wa kimataifa, ulionekana kuwa karibu mnamo Oktoba 1962, wakati mapambano ya kijeshi na mlipuko wa nyuklia, Mtakatifu Yohane XXIII alitoa wito: “Tunawasihi watawala wote wasibaki viziwi kwa kilio hiki cha ubinadamu. Wafanye kila wawezalo kuokoa amani. Kwa hivyo wataokoa ulimwengu kutokana na vitisho vya vita, na matokeo mabaya ambayo hayawezi kutabiriwa. [...]. Kuhamaisha, kutia moyo, kukubali mazungumzo, katika ngazi zote na wakati wote, ni kanuni ya hekima na busara inayovutia baraka za mbingu na dunia. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo ameongeza: Miaka sitini baadaye maneno haya ambayo yanatoa mwangwi, wa kushangaza sasa.ya ujumbe huo ameufanya kuwa kama wake kwamba: “ Hatuko nje lakini tuliokaa kwa ajili ya amani."
Kwa hivyo tunaomba amani kama haki ya wote kusuluhisha migogoro bila vurugu. Katika miaka hii, udugu kati ya dini imetimiza maendeleo stahiki, kwa sababi dini dada Papa amesema tunawasaidia ndugu ili kuishi kwa amani. Daima tuhisi kama ndugu kati yetu! Mwaka mmoja uliopita, akikutana hapo mbele ya Magofu, Papa amekumbusha walivyo toa wito na hivyo kwa mara nyingine tena amesema: “Dini haziwezi kutumiwa kwa ajili ya vita. Ni amani na hakuna kutumia jina la Mungu kubariki vita na kujikabidhi! Watu wanatamani amani. Hili ndilo tutajaribu kuendelea kufanya, ubora zaidi, siku baada ya siku. Tusijikabidhi kwenye vita, tupande mbegu za upatanisho; na leo tunainua kilio cha amani Mbinguni, tena kwa maneno ya Mtakatifu Yohane XXIII: “Watu wote wa dunia na wawe kaka na dada na amani inayotamaniwa na kustawi ndani yao na kutawala daima”. Kwa kuhitimisha Papa amesema "Na iwe hivyo, kwa neema ya Mungu na mapenzi mema ya wanaume na wanawake anaowapenda."