Papa Francisko:Mtaguso wa II wa Vatican ni jibu la swali unanipenda?
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku ambayo Mama Kanisa amemkumbuka Mtakatifu Yohane XXIII, sambamba na maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya kufunguliwa kwa Mtaguso wa II wa Vatican mnamo tarehe 11 Oktoba 1962, Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe 11 Oktoba, jioni ameadhimisha Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Katika mahubiri yake ameanza kusema kuwa:Unanipenda? Ni sentensi ya kwanza ambayo Yesu anamwelekea Petro katika Injili ambayo ilisomwa (Yh 21,15) na kinyume chake ya mwisho ni Chunga Kondoo wangu (Yh 21,17). Katika kumbukizi la ufunguzi wa Mtaguso wa II wa Vatican, tunahisi kuambiwa hata sisi, kama Kanisa, maneno hayo ya Bwana kuwa je Unanimependa? Chunga Kondoo wangu.
Baba Mtakatifu amesema hawali ya yote unanipenda? Ni swali kwa sababu , mtindo wa Yesu si ule wa kutoa jibu, lakini wa kuuliza, maswali ambayo yanashawishi maisha. Na Bwana ambaye katika upendo wake mkubwa anazungumza kwa watu kama marafiki na anakaa nao, anawauliza tena, na anauliza daima kwa Kanisa mchumba wake: Je unanipenda? Mtaguso wa II wa Vatican, ulikuwa jibu kubwa katika swali hilo: kwa ajili ya kuanza upendo wake ambao Kanisa, kwa mara ya kwanza katika historia ulijikita ndani ya Mtaguso kwa kijiuliza lenyewe, kutafakari juu ya asili yake na utume wake. Na lilitambua fumbo la neema iliyotokana na upendo; lilijigundua kuwa Watu wa Mungu, Mwili wa Kristo, hekalu hai la Roho Mtakatifu. Huo ndio mtazamo wa kuwa nao juu ya Kanisa, Mtazamo kutoka juu. Ndio, Kanisa awali ya yote linapaswa kutazamwa kutoka juu, kwa macho ya upendo wa Mungu.
Baba Mtakatifu Francisko amesema ni bora kujiuliza ikiwa katika Kanisa tunaanzia na Mungu, kutoka katika mtazamo wa upendo juu yetu. Kuna kishawishi daima cha kuanzia na umimi, badala ya kuanzia na Mungu, kuweka mipango kwanza ya Injili, kuacha kumezwa na upendo wa kidunia ili kufuata mitindo ya wakati au kutupilia mbali kipindi ambacho Mungu alituzawadia. Hata hivyo lazima kuwa makini iwe katika maendeleo ambayo yanajielekeza ulimwenguni na hata katika utamaduni ambao unalilia ulimwengu uliopita. Sio majaribu ya upendo lakini ya ukosefu wa uaminifu. Ni ubinafsi wa wapinga dini ambao huweka ladha zao na mipango yao wenyewe juu ya upendo unaompendeza Mungu, upendo rahisi, unyenyekevu na uaminifu ambao Yesu amwomba kwa Petro.
Unapenda mimi? Baba Mtakatifu amesema tugundue kwa upya Mtaguso ili kutoa ukuu wa Mungu, na yale yaliyo msingi; katika Kanisa ambalo liweze kuwa kichaa wa upendo kwa ajili ya Bwana wake na kwa ajili ya waamini, ambao aliwapenda; katika Kanisa ambalo liwe tajiri wa Yesu na maskini wa zana; Kwa Kanisa ambalo liwe huru na linalotoa uhuru. Mtaguso unaoelekeza kwa Kanisa sura hii, unafanya kurudi kama Petro katika Injili huko Galilaya, katika kisima cha upendo wa kwanza, ili kugundua umaskini wake wa utakatifu wa Mungu (Lumen gentium 8c, V), kuona mtazamo wa Bwana Msulibiwa na mfufuka ile furaha iliyopotea, na kurudi kwa Yesu. Baba Mtakatifu ameeleza kwamba katika kuelekea siku za mwisho za Papa Yohane, aliandika: “Maisha yangu haya ambayo yanageuka mawio ya jua, hayangeweza kutatuliwa bora kuliko kuzingatia kila kitu kwa Yesu, mwana wa Maria ... urafiki mkubwa na endelevu na Yesu, unaozingatiwa katika picha: mtoto, aliyesulubiwa, aliyeabudiwa katika Sakramenti (Maandiko ya kiroho 977-978).
Kwa maana hiyo hapo kuna mtazamo wetu wa juu, chanzo cha chemi chemi hai daima! Baba Mtakatifu Francisko ameomba kurudi katika chanzo cha upendo wa Mtaguso pia. Ni kupata upendo wa Mtaguso na kujipyaisha upendo kwa ajili ya Mtaguso. Kuingia ndani ya fumbo la Kanisa, mama na mchumba, tunasema hata sisi na Mtakatifu Yohane XXIII, Gaudet Mater Ecclesia! yaani furahi Mama Kanisa!(Hotuba ya Ufunguzi wa mtaguso 11 Oktoba 1962). Kanisa liweze kuhusu furaha. Ikiwa haliishi furaha linasema uongo wake kwa sababu linasahau upendo ambao uliufanywa. Na zaidi kati yetu sisi wakati mwingine hatuwezi kuishi imani kwa furaha, bila kusengenya na bila kukosoa. Lakini Kanisa ambalo limependwa na Yesu hali muda wa mapigano, kuwekeana sumu na mabishano. Kwa maana hiyo Papa amesema kuwa: “Mungu atuepushe na kuwa wakosoaji na wasiostahimili, wakali na wenye hasira. Na si suala la mtindo tu, bali la upendo, kwa sababu wale wanaopenda, kama mtume Paulo anavyofundisha, hufanya kila kitu bila kunung'unika” (rej.Fil 2,14). Baba Mtakatifu Francisko amesema: “Bwana utufundishe kuwa na mtazamo wako wa juu, kutazama Kanisa kama unavyoliona wewe. Na wakati sisi tunakuwa wakosoaji na kutoridhika, tukumbushe kuwa Kanisa ni kushuhudia uzuri wa upendo wako, ni kuishi kwa kujibu swali lako: unanipenda?”.
Unanipenda? Chunga Kondoo wangu. Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba Yesu anaelezea kwa neno upendo ambao anatamani Petro. Tufikirie Petro, alikuwa ni mvuvi wa samaki na Yesu alikuwa amembadili kuwa mvuvi wa watu ( Lk 5,10) . Na sasa anamkabidhi kazi mpya ile ya kuwa mchungaji, ambaye hakuwahi kuifanya. Na kwa mara hii wakati mvuvi anavutia kwake na kupeleka kwake, mchungaji kinyume chake anahangaikia wengine, samaki wa wengine. Na zaidi mchungaji anaishi na zizi, analilisha na analipenda. Yeye hayuko juu yao kama mvuvi, bali yuko katikati yao. Na ndiyo mtazamo wa pili ambao Mtaguso unatukabidhi, mtazamo wa kuwa katikati; kubaki katika ulimwengu na wengine na bila kuhisi kuwa juu ya wengine, kama mtumishi wa Ufalme mkubwa wa Mungu. (Lumen gentium, 5): kwa kupeleka tangazo jema la Injili ndani ya maisha na lugha za waamini, kushirikishana furaha na matumaini (Gaudium et spes,1).
Ni jinsi gani Mtaguso ni wa wakati ufaao kama nini! Papa amesisitiza na kwamba: unatusaidia kukataa kishawishi cha kujifungia ndani ya uzio wa starehe na usadikisho wetu, ili kuiga mtindo wa Mungu, ambao nabii Ezekieli alitueleza leo: “kwenda kuwatafuta kondoo waliopotea na kuwarudisha kwenye zizi lililopotea, kuwafunga jeraha na kuwaponya wagonjwa” (taz. Ez 34:16). Kwa kuongezea katika ufafanuzi wa neno chunga Baba Mtakatifu Francisko amesema Kanisa haliadhimishi Mtaguso ili kujistahi, bali kujitoa kwa wengine. Hakika, Mama yetu mtakatifu na wa Kiharakia, anayebubujika kutoka moyoni mwa Utatu, yupo kwa ajili ya upendo. Yeye ni watu wa kikuhani (taz. Lumen Gentium, 10), aliyokusudiwa kutoonekana mbele ya macho ya ulimwengu, bali kuutumikia ulimwengu.
Tusisahau kwamba Watu wa Mungu wanazaliwa wakiwa “wanyonge” na kufanywa upya ujana wao kwa kujitolea, kwa kuwa ni sakramenti ya upendo, “ishara na chombo cha ushirika na Mungu na umoja wa wanadamu wote” (Lumen Gentium, 1). Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu ameomba kurudi kwenye Mtaguso ambao uligundua tena mto ulio hai wa tamaduni bila kubaki kulilia kwenye mila.ziliopita. Mtaguso uligundua tena chanzo cha upendo, si kubaki kwenye vilele vya milima, bali kushuka chini kama njia ya huruma kwa wote. Turudi kwenye Mtaguso na tusonge mbele zaidi ya sisi wenyewe, tukipinga jaribu la kujinyonya. Kwa mara nyingine tena, Bwana analimbia Kanisa lake: chunga. Na anapokula, anaacha tamaa ya zamani, majuto kwa kupita ushawishi wa zamani, na kushikamana na mamlaka. Kwa maana ninyi, watu watakatifu wa Mungu, ni watu wa wachungaji. Ninyi hamko hapa kujichunga wenyewe, bali wengine yaani wengine wote kwa upendo. Na ikiwa inafaa kuonesha wasiwasi fulani, inapaswa kuwa kwa wale ambao Mungu anawapenda zaidi yaani maskini na waliotengwa (rej. Lumen Gentium, 8; Gaudium et Spes, 1). Kanisa linakusudiwa kuwa, kama Papa Yohane alivyoeleza: “Kanisa la wote,na hasa Kanisa la maskini” (Ujumbe kwa Redio tarehe 11 Septemba 1962).
Je! Unanipenda? Baadaye Bwana alisema: chunga kondoo wangu". Hamaanishi baadhi ya kondoo, tu bali wote, kwa kuwa anawapenda wote, akiwataja kwa upendo kuwa “wangu”. Mchungaji Mwema anawaangalia nje na anataka kundi lake liwe na umoja, chini ya uongozi wa Wachungaji aliowapatia. Alitaka sisi na hiyo ni njia ya tatu ya kuangalia Kanisa. Mtaguso unatukumbusha kwamba Kanisa ni ushirika katika sura ya Utatu (taz. Lumen Gentium, 4.13). Ibilisi, kwa upande mwingine, anataka kupanda magugu ya mgawanyiko. Kwa njia hiyo “Tusikubali kushawishiwa na vishawishi vyake au majaribu ya ubaguzi. Ni mara ngapi, baada ya Mtaguso Wakristo walipendelea kuchagua upande mwingine katika Kanisa, bila kutambua kwamba walikuwa wakivunja moyo wa Mama yao! Ni mara ngapi walipendelea kushangilia chama chao badala ya kuwa watumishi wa wote? Kuwa na maendeleo au ubinafsi badala ya kuwa kaka na dada? Kuwa wa kulia au kushoto, badala ya kuwa na Yesu? Kujionesha kama walezi wa ukweli au waanzilishi wa uvumbuzi badala ya kujiona kuwa watoto wanyenyekevu na wenye shukrani wa Mama Mtakatifu wa Kanisa.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba hivyo sivyo Bwana anataka tuwe. Sisi ni kondoo wake, kundi lake, na tunaweza tu kuwa pamoja na kama kitu kimoja. Hebu tushinde ubaguzi wote na kuhifadhi ushirika wetu. Na sisi sote tuzidi kuwa wamoja, kama Yesu alivyoomba kabla ya kutoa maisha yake kwa ajili yetu (rej. Yn 17:21). Na Maria, Mama wa Kanisa, atusaidie katika hili. Shauku ya umoja ikue ndani yetu, hamu ya kujitoa katika umoja kamili kati ya wale wote wanaomwamini Kristo. Ni vyema leo hii kama ilibvyokuwa wakati wa Mtaguso, wawakilishi wa jumuiya nyingine za Kikristo wawepo pamoja nasi. Asante kwa uwepo wenu”, Papa amewashukuru.
Kwa kuhitimisha amesema: “Tunakushukuru, ee Bwana, kwa zawadi ya Mtaguso. Wewe unayetupenda, tukomboe kutokana na dhana ya kujitosheleza na kutoka kwa roho ya ukosoaji wa kilimwengu. Wewe unayetulisha kwa upendo, utuongoze kutoka kwenye vivuli vya kujinyonya. Ninyi mnaotamani tuwe kundi lililounganishwa, tuokoe na aina za ubaguzi ambazo ni kazi ya mikono ya shetani. Na sisi, Kanisa lako, pamoja na Petro na kama Petro, sasa tunakuambia: “Bwana, wewe wajua yote; mnajua kwamba sisi tunawapenda ninyi” (taz. Yn 21:17).