Tafuta

2022.10.24 Papa Francisko amekutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa Kitaalimungu Yohane Paulo II kwa ajili ya Sayansi ya Ndoa na Familia. 2022.10.24 Papa Francisko amekutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa Kitaalimungu Yohane Paulo II kwa ajili ya Sayansi ya Ndoa na Familia. 

Papa Francisko:Serikali na Kanisa ziwe karibu na familia&udugu kijamii wenye nyufa!

Taasisi ya Kipapa ya Yohane Paulo II ya Taalimungu ya Sayansi ya Ndoa na Familia imekutana na Papa Francisko mjini Vatican ambapo amesisitiza haja ya kufafanua maono ya Kikristo ambayo hayaishii kwenye kifungo cha ndoa,bali yanajikita katika kutafakari uzazi,udugu na uzoefu wa udugu wa familia ya jamii nzima ya wanadamu.Familia inabaki kuwa "sarufi ya kianthropolojia" isiyoweza kubadilishwa mapendo msingi wa wanadamu.

Na Angella Rwezaula;  – Vatican.

Baba Mtakatifu Jumatatu 24 Oktoba 2022 amekutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Taalimungu  ya Yohane Paulo II kwa ajili ya Syansi ya Ndoa na Familia. Katika hotuba yake ameanza na salamu kwa Kardinali Kevin Farell  rais wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha kwa msaada anao utoa katika baraza hilo  na kumshukuru Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Kansela wa Taasisi hiyo kwa maneno aliyomwelelekea ambaye  alimtaka kuwa: “Ninaamini ni mwenye tuzo ya Nobel kwa ajili a ubunifu!. Hakusahau kusalimu Monsinyo  Philippe Bordeyne, Makamu wa Chuo hicho katika vitengo vya nje, maprofesa na wanafunzi wote, pamoja na wenzi wa ndoa  ambao wameanza kozi  ya kudumu katika Taasisi hiyo. Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa imepita miaka mitano tangu ilipochapishwa barua yake  binafsi  Motu proprio Summa familiae cura, kuhusu (Utunzaji wa Familia) ambayo alipendelea kuwekeza kuhusu urithi ulioachwa na Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye alianzisha Taasisi hiyo mnamo 1981. 

TAASISI YA KIPAPA YA TAALIMUNGU YA YOHANE PAULO II
TAASISI YA KIPAPA YA TAALIMUNGU YA YOHANE PAULO II

Papa Francisko amesema alikuwa na nia ya kutoa mwako mpya na nafasi pana ili kukabiliana na changamoto ambazo zilikuwa zinajiwakilisha katika milenia ya tatu. Kwa hayo iliendelezwa na kuhakikisha ubora wa elimu katika nidhamu za kitaalimungu na katika sayansi za binadamu na kijamii. Kwa njia hiyo Papa anahisi kwa namna ya pekee umuhimu kwa sababu inafungamanisha taaluma za lazima kwa ajili ya utambuzi na mang’amuzi ya thamani za uhusiano binafsi na zile za kifamilia. Taalimungu yenyewe ili iweze kuwa katika hali ya upana huo inaalikwa kushirikiana katika maono ya kikristo kwa wazazi, umwana, kindugu na sio tu uhusiano wa wenzi wa ndoa bali ni unafanana na uzoefu wa wa familia, katika maono ya jumuiya nzima ya kibinadamu. Utamaduni wa imani kiukweli unaalikwa kujipima, bila ujinga na bila hofu, kwa mabadiliko ambayo yagusa dhamiri ya sasa ya uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke, kati ya upendo na kizazi na kati ya familia na utamaduni.

Baba Mtakastifu Francisko amewapongeza na kuwatia moyo juhudi zao za kupeleka mbele kwa umakini na ubunifu wa mipango ya mafundisho ambayo yanafuata urithi na usasisho wa mwanzilishi wa Taasisi hiyo. Ni jitihada ambazo siku hadi siku zinajaza umihimu wa shughuli za  kipapa kwa kuchangia taasisi, kueleweka katika umuhimu wake, na  kutumikia Kanisa baada ya huduma ya Petro ambayo  ni zawadi inayopokelewa na wakati huo huo, kusambazwa. Kwa sababu hiyo Papa ameongeza kusema kuwa, mtu yeyote ambaye anasoma kiungo chake kipya na mafundisho  hai katika suala la upinzani dhidi ya utume  uliopokelewa na taasisi yake ya asili atakuwa amekosea sana. Kiukweli mbegu inakua na kuzaa maua na matunda. Utume wa Kanisa unahimiza leo hii kwa dharura ufungamanishwaji  wa Taalimungu ya uhusiano wa ndoa na udhati zaidi wa taalimungu ya hali ya kifamilia.

Msukosuko ambao haujawahi kutokea, mwanzo na ambao kwa wakati huu unajaribu uhusiano wote wa familia unawaweka katika kuwa na umakini wa kufanya mang’amuzi ili kupokea mbegu za matumaini na huruma ya Mungu. Baba Mtakatifu Francisko amesema wote sio manabii wa matukio, lakini  ni wa matumaini. Kwa maana hiyo, katika kufikiria sababu za mgogoro,  ni lazima kutopoteza kamwe mtazamo hata wa ishara za faraja ambazo wakati mwingine za kushangaza, zenye uwezo wa uhusiano wa kifamilia na zinazoendelea kujionesha, kwa ajili ya jumuiya ya imani, ya jamii ya raia, na ya kuishi kibinadamu. Baba Mtakatifu amekumbusha wote wanajua   ilivyo na thamani katika wakati mazingira yanakuwa magumu na vikwazo, uimara, upinzani, na ushirikiano wa mahusiano ya familia. Familia inabaki kuwa “sarufi ya kianthropolojia” isiyoweza kubadilishwa mapendo ya  msingi wa wanadamu.

TAASISI YA KIPAPA YA TAALIMUNGU YA YOHANE PAULO II
TAASISI YA KIPAPA YA TAALIMUNGU YA YOHANE PAULO II

Nguvu ya vifungo vyote vya mshikamano na upendo hujifunza siri zake ndani mwake, katika familia. Sarufi hii inapopuuzwa au kukasirishwa, mpangilio mzima wa mahusiano ya kibinadamu na kijamii hupata majeraha yake. Na wakati mwingine ni majeraha ya kina sana. Kwa mfano: je, kazi ya kujitolea ya kijamii labda haileti kutoka katika vifungo hivi vya uzazi na vya kindugu vya upendo  ambao ni ishara na njia za mahusiano wake bora? Je! ulinzi wa wasio na ulinzi hautokani na kuwatunza waliozaliwa? Udugu sio uzoefu rahisi, bila shaka, lakini je, kuna njia bora zaidi ya kuzaliwa kama kaka na dada kufikia kuelewa maana ya kuwa  wote na kwa wote, binadamu sawa? Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo ameonesha ni vizingiti vipi vya changamoto ambazo vinahimiza kuanza kwa upya kuwasha taa inayoanza  na upendo wote wa kifamilia  na sio ule wa wenzi  tu bali kwa jamii nzima. Ubora wa ndoa na wa familia unaamua ubora wa upendo wa kila nafasi ya mtu na uhusiano wenyewe wa jumuiya ya binadamu. Kwa njia hiyo wajibu uwe wa Serikali na ule wa Kanisa Kanisa kusikiliza, kwa mtazamo wa upendo wa karibu, mshikamano na wema, ambao usaidiei katika kazi ambazo zinafanywa tayari na wote, na kuwatia moyo wito kwa ajili ya ulimwengu wa kibinadamu na  uweze kuwa wa mshikamano zaidi na wa kidugu zaidi.

“Ni lazima tulinde familia lakini tusiifunge, tuifanye ikue inavyopaswa kukua. Lazima kuwa makini na  itikadi zinazoingilia kuelezea familia kutokana na  mtazamo wa kiitikadi. Familia sio itikadi, ni ukweli. Na familia hukua na uhai wa ukweli. Lakini itikadi zinapokuja kuelezea au kuchora familia nini kinachotokea na kila kitu kinaharibiwa. Kuna familia ambayo ina neema hiyo ya mwanaume na mwanamke wanaopendana na kuumba kila mmoja wao kwa wao, na ili kuelewa familia lazima kila wakati kwenda  kwenye ukweli, na sio katika itikadi”. Papa amesisitiza kwa nguvu kwamba “Itikadi huharibu, itikadi zinahusika kutengeneza barabara ya uharibifu. Jihadharini na itikadi!” Hatupaswi kungoja familia iwe kamilifu, hii ni kweli, ili iwe kamili kutunza wito wake na kuhimiza utume wake. Ndoa na familia daima zitakuwa na kutokamilika hadi tuwe Mbinguni.” Baba Mtakatifu Francisko amesema Yeye huwa anawauliza wale ambao wanataka kuonana  ikiwa wanataka kupigana, kwa chochote wanachotaka, lakini isiwe kwa muda mrefu na lazima wafanya amani, hasa kabla ya siku kumalizika. Uwezo huu wa kupona unaoiweka familia katika hali ngumu ni neema, kwa sababu ikiwa haitapona, vita baridi ya siku inayofuata ni hatari. Na bado, wanakabidhi kutokamilika kwao  wenyewe kwa Bwana, kwa sababu ya kuchota  kutoka katika  neema ya sakramenti baraka kwa kiumbe walichokabidhiwa  kwa ajili ya upitishaji wa maana ya maisha, sio maisha ya mwili tu  kwani inawezekana na Mungu.

TAASISI YA KIPAPA YA TAALIMUNGU YA YOHANE PAULO II
TAASISI YA KIPAPA YA TAALIMUNGU YA YOHANE PAULO II

Baba Mtakatifu aidha amesema mengi, katika jamii hii iliyojaa nyufa, inategemea na kugunduliwa kwa upya kwa furaha iliyofanywa upya ya tukio la familia lililoongozwa na Mungu.Kwa miaka thelathini umwilisho wa Mwana wa Pekee ulihusisha kuishi na kukita mizizi ndani ya familia na vifungo vya pamoja vya hali yake ya kibinadamu. Haukuwa wakati rahisi wa “kungoja” ulikuwa wakati wa kuelewa na hali ya kawaida ya kibinadamu, iliyokaliwa na macho yaliyowekwa kwenye mambo ya Baba” (rej. Lk 2:49). Katika hilo Baba Mtakatifu amewasimulia juu ya uzoefu aliokuwa nao kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, kabla ya janga la uviko. Kuna wenzi wa ndoa ambao walikuwa wanaonekana vijana lakini walikuwa wanaadhimisha miaka  60 kwa sababu walioana mmoja akiwa na miaka 18 na mwingine miaka 20, hivyo aliwauliza ikiwa wao walikuwa hawachoki baada ya miaka mingi. Hawa walitazamana na kutulia tuli baadaye wakaanza kulia kwani walisema wanapandana. Hili lilikuwa jibu baada ya miaka 60. Hii imekuwa taalimungu  bora na nzuri zaidi juu ya familia ambayo aliiona.

Bwana awasindikize na shauku ya imani yao na msimamo wa  akili yao, katika kazi ngumu ya kusaidia, kutunza, kushangilia na  ndio, pia kushangilia kwa  baraka hii ya uumbaji na ya kikanisa ambayo ni familia.  Papa ameonesha furaha kujua na kutambua kwamba wanajitolea kwa ahadi hii pia kupitia ukomavu wa hali ya familia na roho ya sinodi ya jumuiya ya wasomi yenyewe. Mama wa Bwana, ambaye zaidi ya sisi ni mtaalam katika kiungo hiki kati ya siri ya kuokoa ya kiumbe kipya na hali ya familia ya upendo wa kibinadamu, awaongoze na kuwahifadhi. Amewabariki kwa moyo mkunjufu, na kama kawaida, kwa sababu Papa ni mwombaji, amesema tafadhali wamwombee.

Papa na Taasisi ya Kipapa ya Yohane Paulo II
24 October 2022, 15:36