Tafuta

Papa Francisko:Tumwombe Mungu kujua kilicho ndani ya mioyo yetu

Katika Katekesi yake Papa Francisko,ameendelea mzunguko wa utambuzi ambapo amesisitizia suala la tamaa nzuir.Lazima kumwomba Mungu ili kujua na kutambua kile ambacho Mungu ameweka ndani ya mioyo yetu.Tamaa nzuir inayoongoza maisha si tamaa ya kitambo tu bali ni hamu ya Mungu.

Na Angella Rwezaula; -Vatican

Baba Mtakatifu Francisko Katika Mzunguko wa Katekesi kuhusu Utambuzi, baada ya kutafakari sala na kujijijua binafsi, Jumatano tarehe 12 Oktoba 2022 katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa maujaji na waamini waliofika, amependa kuzungumza juu ya kiungo kingine cha lazima hasa juu ya tamaa nzuri. Kiukweli, utambuzi ni aina ya utafiti, na daima utafiti hutokana na  kitu ambacho hatuna lakini ambacho kwa njia fulani tunajua, na tuna ustadi. Ujuzi huu ni wa aina gani? Waalimu wa kiroho wanaonesha neno tamaa ambalo, msingi wake, ni hamu ya utimilifu lakini ambayo kamwe haipati utimilifu kamili, hadi inakuwa ishara ya uwepo wa Mungu ndani yetu. Tamaa  sio hamu ya wakati huo, hapana. Neno la Kiitaliano linatokana na neno la Kilatini zuri sana, hili linashangaza yaani  de-sidus, kwa maana ya halisi ya ukosefu wa nyota , tamaa ni ukosefu wa nyota, ukosefu wa hatua ya kumbukumbu inayoongoza njia ya uzima; inaibua mateso, kokosekana, na wakati huo huo mvutano wa kufikia mema ambayo hatuna.

Katekesi ya Papa Francisko 12 Oktoba 2022
Katekesi ya Papa Francisko 12 Oktoba 2022

Tamaa nzuri  basi ni dira ya kuelewa nilipo na ninaenda wapi, hakika ni dira ya kuelewa ikiwa bado au ninakwenda, mtu ambaye hatamani kamwe ni mtu aliyesimama, labda ni mgonjwa na karibu ya kufa. Ni dira ambayo inanifanya kuona kama ninakwenda au kama nimesimama. Na je inawezekanaje kuitambua? Baba Mtakatifu amesema,  basi tufikirie, tamaa  ya dhati ambayo inajua jinsi ya kugusa kwa undani kamba za utu wetu, kwa sababu hiyo haizimiki mbele ya shida au vikwazo. Ni kama vile wakati tuna kiu: ikiwa hatupati kinywaji, hatukati tamaa, badala yake, utafutaji unakuwa wa zaidi na zaidi katika mawazo yetu na matendo yetu, mpaka tunakuwa tayari kutoa sadaka yoyote ili kuweza kutuliza. Vikwazo na kushindwa havizuii tamaa nzuri, hapana, kinyume chake hufanya iwe hai zaidi ndani yetu.

Tofauti na shauku  au hisia za wakati huo, tamaa nzuri hudumu kwa muda, hata kwa muda mrefu, na huwa na tabia ya kujikamilisha. Ikiwa, kwa mfano, kijana anataka kuwa daktari, atalazimika kufanya kozi ya masomo na kazi ambayo itachukua miaka michache ya maisha yake, kwa hivyo atalazimika kuweka mipaka, na kusema hakuna kufanya mchezo, kwani  awali ya yote kwa kozi nyingine za masomo, lakini pia kwa burudani na vikengeushi vinavyowezekana, hasa wakati wa masomo mazito zaidi. Hata hivyo, tamaa nzuri  ya kutoa mwelekeo wa maisha yake na kufikia lengo hilo, ili kuwa daktari kwa mfano, inamruhusu kushinda matatizo haya. Tamaa nzuri  inakufanya uwe na nguvu, inakufanya uwe na ujasiri, daima inakufanya uendelee kwa sababu unataka kufikia lengo  hilo: “Ninatamani hilo”. Kwa hakika, thamani inakuwa nzuri na kupatikana kwa urahisi zaidi inapovutia. Kama mtu fulani alivyosema, “zaidi ya kuwa wema ni muhimu kuwa na tamaa nzuri ya kuwa hivyo”. Kuwa mwema kunavutia, na sote tunataka kuwa wema, lakini je, tuna shauku ya  kuwa wema?

Katekesi ya Papa Francisko 12 Oktoba 2022
Katekesi ya Papa Francisko 12 Oktoba 2022

Baba Mtakatifu Francisko amesema,  inashangaza kwamba Yesu, kabla ya kutenda muujiza, mara nyingi anauliza mtu kuhusu hamu yake: “Je! Unataka kuponywa?” Na wakati mwingine swali hili linaonekana kuwa lisilofaa, kwa sababu inaonesha wazi kwamba yeye ni mgonjwa! Kwa mfano, alipokutana na mtu aliyepooza kwenye bwawa la Betzatà, ambaye alikuwa huko kwa miaka mingi na hakuweza kuwa na wakati mwafaka wa kuingia majini. Yesu alimwuliza: “Je, wataka kuwa mzima?” ( Yh 5:6 ). Ni kwa nini? Kiukweli, majibu ya aliyepooza yanaonesha mfululizo wa upinzani wa ajabu kwa uponyaji, ambao haukutazama yeye peke yake. Swali la Yesu lilikuwa mwaliko wa kufafanua moyo wake, kupokea hatua iliyobora inayowezekana, ili asijifikirie tena na juu ya maisha yake kama mwenye kupooza, akibebwa na wengine.  Badala yake mwanamume aliye kuwa kitandani hakuonekana kushawishika hivyo.

Katika mazungumzo na Bwana, Papa ameongeza kusema, tunajifunza kuelewa kile tunachotaka  juu ya ukweli wa maisha yetu. Mlemavu huyo ni mfano wa kawaida wa watu: kwa mfano wengine wanasema: “Ndiyo, ninataka,  lakini sitaki, sifanyi chochote. Kutaka kufanya kunakuwa kama udanganyifu na hauchukuliwi hatua yoyote. Wapo wale watu ambao wanaonesha wanataka na wakati huo huo hawataki. Hii ni mbaya, kwa sababu  huyo mgonjwa  kwa miaka 38, kila wakati alikuwa na malalamiko. Katika maneno yake anasema: “unajua Bwana  kwamba maji yanapoanza kusonga na wakati wa muujiza, mtu mwenye nguvu kuliko mimi anaingia  na  mimi nimekwish[ Photo Embed: Katekesi ya Papa Francisko 12 Oktoba 2022]a chelewa, analalamika na kulia”.  Kwa maana hiyo Papa ametoa angalisho: “kuweni waangalifu kwani malalamiko ni sumu, sumu ya roho, sumu ya maisha kwa sababu hayakufanyi utamani kuendelea mbele.” Kwa kukazia zaidi, ametoa onyo dhidi ya malalamiko kwamba wanapolalamika katika familia, wanandoa wanalalamika wao kwa wao, watoto,  baba au mapadre kwa askofu au maaskofu juu ya mambo mengine mengi ...  Haipaswi kufanya hivyo kwa sababu mkijikuta mnalalamika lazima muwe waangalifu kwa sababu ni kama dhambi, na hiyo  hairuhusu hamu ya kukua. Mara nyingi ni tamaa nzuri ambayo hufanya tofauti kati ya mpango uliofanikiwa, thabiti na wa kudumu, na matamanio elfu na nia nyingi nzuri ambazo, kama wasemavyo “kuzimu imejengwa” yaani ile ya  “Ndio, ningependa... lakini hufanyi chochote”.

Katekesi ya Papa Francisko 12 Oktoba 2022
Katekesi ya Papa Francisko 12 Oktoba 2022

Enzi tunayoishi inaonekana kupendelea uhuru wa kuchagua, lakini wakati huo huo inadhoofisha tamaa, wewe  unataka kujiridhisha kila wakati,  na  mara nyingi unaishia katika shauku za wakati huu tu.  Kwa maana hiyo  lazima tuwe waangalifu ili tusiharibu tamaa nzuri. Tumeshambuliwa na mapendekezo elfu na mipango,  uwezekano, ambao unahatarisha kutuvuruga na hairuhusu kutathmini kwa utulivu kile tunachotaka.  Mara nyingi, tunakutana na watu, kwa mfano  tufikirie vijana wakiwa na simu zao za mkononi, wanaonekana, wanatafuta, lakini, je wewe  unasimama kufikiri? Hapana. Inatokea kila wakati, kuelekea mwingine. Tamaa nzuri haiwezi kukua hivyo, kwa sababu wanaishi kipindi cha  wakati huo, uliojaaa wakati na tamanio halikui. Watu wengi wanateseka kwa sababu hawajuhi wanataka nini katika maisha yao; labda hawakuwahi kuwasiliana na tamaa  yao ya kina, na hawakuijua kamwe.  Ukiuliza Je unataka nini katika maisha yako? utajibiwa “Sijuih”. Kwa hiyo ni hatari ya kupitia maisha ya mtu kati ya majaribio na manufaa ya aina mbalimbali, bila kufika mahali popote na kupoteza fursa za thamani. Na kwa hivyo baadhi ya mabadiliko, ingawa yamekusudiwa kinadharia, fursa zinapotokea hazitekelezwi kamwe, hakuna shauku kubwa ya kupeleka  jambo mbele.

Ikiwa Bwana angetuuliza leo hii, kwa mfano, kwa yeyote kati yetu, kama swali alilomwuliza kipofu huko  Yeriko: “Unataka nikufanyie nini?” (Mk 10,5), au  “mnataka niwafanyie nini?  Je tungejibu nini?  Papa ameuliza umati.  Pengine, hatimaye tunaweza kumwomba atusaidie kujua tamaa  kubwa kwake, ambayo Mungu mwenyewe ameiweka mioyoni mwetu na kusema kwamba:  “Bwana, ninaomba nijue matamanio yangu, niwe mwanamke, mwanamme  wa matamanio makubwa” Bwana  labda atatupatia nguvu ya kufanya hivyo. Ni neema kubwa sana, kwa msingi wa wengine wote ili  kuruhusu Bwana, kama ilivyo katika  Injili, kufanya miujiza kwa ajili yetu. Tumwombe “Bwana utupatie matanaio na kuyafanya kukua”. Kwa sababu yeye pia ana tamanio kubwa kwa ajili yetu: kutufanya kuwa washiriki wa utimilifu wake wa maisha.

Katekesi ya Papa na wito kwa ajili ya kistisha vita na vurugu nchini Ukraine 12 Oktoba 2022
12 October 2022, 12:28