2022.10.27  Papa amekutana na Mapadre, watawa wa kikie na kiume wanaoishi Roma. 2022.10.27 Papa amekutana na Mapadre, watawa wa kikie na kiume wanaoishi Roma. 

Papa kwa Jumuiya ya Madagascar Roma:matunda ya utume yategemea umoja

Papa akikutana na Umoja wa Mapadre na Watawa wa Madagascar wanaoishi Roma katika fursa ya ziara ya kitume ya Baraza la Maaskofu Madagascar,kati ya mengi amesema matunda ya utume wao yanategemea umoja unaohamasishwa."Jamii zetu na kwa bahati mbaya hata katika Kanisa,kuna shuhuda ya hutafutaji wa masilahi ya kibinafsi na kuna masenyenyo mengi"

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, alhamisi 27 Oktoba 2022 amekutana mjini Roma Umoja wa Mapadre na Watawa wa kike na kiume kutoka Madagascar ambao wanaishi Roma. Katika hotuba yake amefurahishwa kukutana nao na kuwasalimu viongozi wa Umoja huo  kwa ziara hiyo ambayo amesema imemwezesha kuwafahamu wao matarajio na matumaini yao kama watu waliowekwa wakfu katika utume jijini Roma. Pia amemsalimu Askofu Marie Fabien, Rais wa Baraza la Maaskofu  Madagascar ambaye amefanya juhudi kufanikisha mkutano huo na amemshukuru kwa uwepo wake na kwa Baraza lake. Baba Mtakatifu Francisko amesema uwepo wao, wakati Maaskofu wao wako katika ziara yao ya Kitume jijini Roma ilikuwa ni kielelezo cha umoja wao wa sala na safari ya kiroho waliyofanya kwenye makaburi ya Mitume Petro na Paulo. Kwa hakika, kuzaa matunda ya utume wao pia kunategemea umoja mnaohamasishwa, kati yao  na Wachungaji wao ambao ni muhimu sana, yaani umoja huo.  Baba Mtakatifu Francisko amesema huo ni ushuhuda ambao unaalikwa kupelekwa  kwa jamii  yao yote. Hii ni kwa sababu “Ulimwengu wetu unahitaji umoja, ni wakati ambapo  sisi sote tunahitaji umoja, tunahitaji upatanisho, tunahitaji umoja, na Kanisa ambalo ni nyumba ya umoja” (Katekesi, tarehe 25 Septemba 2013).

Umoja wa Mapadre na Wataza kutoka Madagascar wanaoishi Roma wamekutana na Papa
Umoja wa Mapadre na Wataza kutoka Madagascar wanaoishi Roma wamekutana na Papa

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa  leo hii , katika jamii zetu na kwa bahati mbaya wakati mwingine pia katika Kanisa, kuna shuhuda ya hutafutaji  wa masilahi ya kibinafsi na kuna masenyenyo mengi, na gumzo ni utaratibu wa siku kwa mana hiyo ametoa onyo: “ tafadhali msisengenyane,  bali zungumzeni mmoja na mwingine kwa wema kwa sababu masengenyo ni silaha ya utengano. Mtazamo huu wa masenyenyo, wa virusi vya ubinafsi, unatishia kuishi pamoja kwa amani kati ya watu, kama vile kati ya wana na binti wa nchi moja".  Kwa maana hiyo mbele ya kukabiliwa na hali hiyo, uzoefu wao wa kibinafsi na wa jumuiya kama watawa, kwa ajili ya Kristo Baba Mtakatifu Francisko amesema ni uthibitisho kwamba maisha yanaweza kuishi kwa njia tofauti katika mwanga wa Injili, ambayo inatoa furaha ya kweli.

Umoja wa Mapadre na Wataza kutoka Madagascar wanaoishi Roma wamekutana na Papa
Umoja wa Mapadre na Wataza kutoka Madagascar wanaoishi Roma wamekutana na Papa

Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amewatia moyo wa kutembea daima pamoja na kufanya uwepo wao jijini Roma kuwa fursa ya thamani, ambayo itawawezesha kujitajirisha na kufanya upya imani yao katika nyayo za watu wakuu watakatifu waliotangulia hapa. Papa amewasihi  wao waunde kama familia moja kubwa ya kiroho, ambayo ndani mwake wanaheshimiana, wanapendana na kusaidiana. Kwa njia hiyo wataweza kuwa ishara za matumaini kwa Makanisa yao mahalia ya  Madagascar, ambalo linatarajia mengi kutoka kwao. Amewakabidhi kila mmoja wao kwa Bikira Maria. Na awasaidie kulinda kwa uaminifu utambulisho wao kama makuhani, wanaume na wanawake watawa, walei, katikati ya mabadiliko ya wakati huu. Mama yetu na awaombee, ili daima wawe wazi na ukarimu kwa kaka na dada  zao  hasa wale wanaopitia nyakati ngumu. Wawe na umoja, waungane na maaskofu, ambao ni wachungaji. Na ameomba Baraka za Mungu juu yao, kwa Kanisa la Madagascar na kwa taifa lao zima.

HOTUBA YA PAPA KWA UMOJA WA MAPADRE NA WATAWA WA MADAGASCAR ROMA
27 October 2022, 12:45