Hija ya Kitume ya Papa Francisko Bahrain: Vijana huko Awali pandeni mbegu ya udugu
Na Angella Rwezaula,-Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi jioni tarehe 5 Novemba 2022, akiwa katika hija yake ya kitume nchini Bahrain kuanzia tarehe 3hadi 6 Nvemba, amekutana na vijana huko Awali katika shule ya Moyo Mtakatifu. Katika hotuba yake kwanza kabisa amewashukuru uwepo wao kwa wingi kutoka mataifa tofauti na wenye shauku. Amemshukuru Sr. Rosalyn kwa maneno ya hotuba yake ya kumkaribisha na jitihada ambazo kwa pamoja na wengine wanapeleka mbele shule ya Moyo Mtakatifu. Baba Mtakatifu aidha alishukuru kuona kwamba katika Ufalme wa Bahrain ni eneo la makutano na mazungumzo kati ya tamaduni na imani tofauti. Na kwa kuwatazama wao ambao sio wa dini moja na hawana hofu ya kukaa pamoja, amefikiria kwamba bila imani tofauti nchi hiyo isingewezekana. Na pasingekuwapo wakati ujao. Katika unga wa ulimwengu, wao ndio chachu njema ya kufanya unga ukue, kushinda vizingiti vingi vya kijamii na kiutamaduni, mambo mabaya na kuhamasisha kuchanua kwa udugu. Ni vijana wenye kuwa na ari na kama wasafiri ambao ni watafiti hivyo wasiogope kukabiliana katika mjadala, kusikika sauti zao zichanganyikane na wengine na kugeuka kuwa msingi wa jamii rafiki na kijamii.
Huo ndio msingi katika muktadha mgumu na wingi ambao wanauishi ili kufanya kuanguka baadhi ya kuta kwa kutarajia ulimwengu unaostahili kipimo cha binadamu na udugu zaidi, hata kile ambacho kina maana ya kukabiliana na changamoto nyingi. Kwa kuhamasishwa na shuhuda za maswali yao Baba Mtakatifu amependa kuwapa mialiko mitatu ambayo si kama kuwafundisha jambo fulani lakini kama kuwatia moyo. Suala la kwanza amesema ni Kukumbatia utamaduni wa kutunza. Tayari Sr. Rosalyn alitumia kielelezo cha kutanza mmoja na mwingine kwa maana hiyo ni kuendeleza tabia ya ndani kwa upana, kuwa na mtazamo wa umakini ambao unapelekea kuondokana na ubinafsi na kuwa wakarimu kwa kushinda sintofahamu na kutoa msukumo kwa wengine. Hayo ndio mapya, dawa dhidi ya ulimwengu uliojifunga, wa ubinafasi, unao wararua watoto wake, dhidi ya ulimwengu uliofungwa na huzuni ambao unasababisha kutokujali na upweke.
Ikiwa hawajifunzi kusaidiana kwa wale ambao wanawazunguka kuanzia na mji, jamii na kazi ya uumbaji ni kuishia katika maisha kama vile anayekimbia, anayehangaika na kufanya mambo mengi na mwishowe anabaki na huzuni kwa sababu hakuona ladha ya kina ya furaha ya urafiki na kupewa bure na Mungu. Na hakutoa ulimwenguni alama ile ya kipekee ya uzuri ambao ni Mungu peke yake anaweza kutoa na hakuna mwingine. Kama Mkristo Papa amesema kwamba anamfikiria Yesu na kuona utendaji wake dauna ulikuwa umejikita kwenye utunzaji. Kwa maana hiyo baba Mtakatifu amesisitiza jinsi ilivyo vizuri kugeuka wahunzi wa utunzaji, na wasanii wa mahusiano. Lakini hili linahitaji kama ilivyo kwa maisha yote, mazoezi yasiyo isha. Kwa maana hiyo vijana wasishau awali ya yote kujitunza binafsi, si tu nje lakini kuanzia ndani, sehemu iliyojificha zaidi na yenye thamani. Je ni ipi ? Ni roho, ndani ya moyo wao. Je ni jinsi gani ya kutunza? Katika kujibu Papa amewaomba wajaribu kuusikiliza kwa ukimya, kutafuta nafasi ya faragha ili kuwa na mawasiliano ya undani waweze kuhisi zawadi ya jinsi wao walivyo, kuipokea na kuishi kwao, si kuiacha ipotelee mikononi mwao. Papa amwambia kwamba wasiangukie kuwa kama watalii wa maisha yao ambapo watalii hutazama kile cha nje tu, na kijujuu. Na katika ukimya inawezekana kuzungumza na Mungu.
Na upendo sio liwaya au filamu ya mapenzi. Kupenda ni kuwa na moyo kwa ajili ya mwingine, kumsaidia mwingine kutoa muda binafsi, kama zawadi binafsi kwa yule mwenye kuhitaji, kuthubutu ili kufanya maisha kuwa kama zawadi ambayo inatoa maisha mengine zaidi. Papa Francisko amewaomba wasisahau kamwe kuwa wao wote ni tunu msingi, ya kipee na yenye thamani. Kwa maana hiyo wasiache maisha katika safe kwa kufikiria kwamba ni vizuri kuwa na zaidi na kwamba muda wa kutumia bado haujatimia. Vijana wengi wako hapo kama wa mpito kwa sababu ya kazi au mara nyingi hata kazi ya kudumu.Lakini ikiwa wanaishi na mawazo ya kitalii, haiwezekana kupokea wakati uliopo na kuna hatari ya kutupa vipande vipande vya maisha yote! Papa ameongeza kusema ni jinsi gani ilivyo nzuri, kunyume chake kuacha alama sasa ya mchakato wa safari iwe njema kwa wafanyakazi wenzao na hata kazi ya uumbaji. Kutunza jumuiya na wengine unapoishi ni jambo zuri , mahali ambapo mwenyezi Mungu anapenda uwepo.
Mwaliko wa pili ambao Baba Mtakatifu Francisko amewapatia vijana hao ni kupanda mbegu ya udugu. Akirejea ushuhuda wa kijana aitwaye Abdulla kuwa ni lazima kuwa bingwa na sio katika uwanja wa mchezo tu, bali katika maisha. Hiyo ni kweli kuwa bingwa wa udugu, Papa amesisitiza. Lakini hata hivyo hiyo ni changamoto leo hii ili kushinda ya kesho, ambapo changamoto za jamii zetu, daima zinakuwa na utandawazi na utumaduni mwingi, kwa maana hiyo Papa ametoa mfano kwamba watazame zana na teknolojia ambayo ulimwengu unatoa lakini hazitoshi kufanya ulimwengu uwe na amani na udugu. Pepo za vita, kiukweli hazitulii kwa ajili ya maendeleo ya kiufundi. Inasikitisha sana kuona katika kanda nyingi mivutano na hatari zinaongezeka na wakati mwingine kuongezeka migogoro. Lakini daima inajitokeza kwa sabababu hawa hawafanyi kazi ndani ya moyo wao, na wanaacha wavutwe mbele na mitazamo ya wengine, kwa namna hiyo ya sintofahamu za kikabila, kiutamaduni, kidini na pengine husababisha matatizo na hofu ambazo zinabagua na zaidi fursa kwa ajili ya kukua pamoja. Baba Mtakatifu ameongeza kusema kwamba na inapofikiriwa kuwa na nguvu ya udugu ambao unatufungamanisha kuna hatari ya kinzani.
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea ameabainisha kwamba kama vijana wenye uwezo wa moja kwa moja wa kuunda mawasiliano na urafiki, kushinda hukumu na misimamo mikali ya kiitikadi, Papa amewaomba wawe wapandaji wa udugu na watakuwa wapokeaji wa wakati ujao kwa sababu, ulimwengu utakuwa na wakati ujao kwa njia ya udugu tu. Ni mwaliko ambao amesema ameupata kutokana na imani yake na uzoefu wake. Kiukweli Biblia inasema hasiye mpenda jirani yake anayemwona, hawezi kumpeda Mungu hasiye mwona. Na hiyo ni mari tuliyo nayo ambayo ilitoka kwake. Anaye Mpenda Mungu anampenda hata ndugu yake 1Yh 4, 20- 21. Yesu anaomba kutotengenisha kamwe upendo kwa Mungu na kwa jirani, ili kufanya kuwa sisi sote ni ndugu (Lk10,29-37). Ni kwa ajili ya wote na wala zi kwa yule anipendaye tu, ni kusikia kaka na dada yaani wote wa ulimwengu uliokabidhwa na kwa kila kiumbe. Kama vijana hasa mbele ya tabia za kubaki na sintofahamu, kujionesha bila kujali mateso ya wengine, kufikia hata kuanzisha vita na migogoro, wao wanaitwa kutenda na ndoto mpya ya udugu na urafiki kijamii ambao huishii katika maneno tu [Ft 6]. Maneno hayatoshi kwa sababu kuna haja ya ishara za dhati za kupeleka mbele kila siku.
Papa ameomba wajiulize pia ikiwa wako wazi kwa wengine. Je ni marafiki wa watu ambao hawaingii katika mzunguko wao, imani yao na ukawaida wao. Je wanatafuta kukutana nao. Njia ni ile ya maneno machache kama alivyosema Nevin kwamba kuunda uhusiano mwema na wote. Kwa maana hiyo vijana wanayo ari kubwa ya kusafiri na kujua ardhi mpya, kushinda mipaka ya maeneo. Kutokana na hiyo Papa amewaomba wasafiri hadi ndani mwao, wapanue mipaka ya ndani, kwa sababu wanaweza kuangusha hukumu dhidi ya wengine, wapunguze nafasi za kutoaminiana na kuvunja kuta za hofu, ili urafiki kidugu upate kuchanua. Baba Mtakatifu ameomba waache wasaidiwe na sala ambayo inapanua moyo na kumfungulia mkutano na Mungu ambaye anasaidia kuona yule ambaye wanakutana naye kama kaka na dada. Katika hilo, Papa amesema ni maneno mazuri kutoka kwa nabii asemaye:Labda hakutumbwa na Mungu mmoja? Kwa nini sasa tunamtendea mwingine vibaya [Ml 2,10]. Jamii kama hiyo yenye utajiri mkubwa imani, tamaduni na lugha tofauti wanaweza kugeuka kuwa uwanja wa mazoezi ya udugu. Wao wako kwenye mlango wa bara lenye mataifa mengi la Asia ambalo mtalimungu mmoja papa amesema alilifafanua kama bara la lugha. Kwa maana hiyo wapate kujivunia na kuwa na maelewano ya lugha moja ya upendo na mabingwa tofauti wa udugu.
Papa akijikita kwenye mwaliko wa tatu ulikuwa unatazama changamoto ya kufanya chaguzi ya maisha. Wao wanatambua vema juu ya uzoefu wa maisha ya kila siku kwamba hakuna maisha hata kidogo bila changamoto za kukabiliana nazo. Daima mbele yake kuna changamoto na kuna njia mbili ambapo unaweza kuchangua mojawapo, kujiweka karibu, kuthubutu na kuamua. Lakini hiyo inahitaji mkakati mwema na siy wa kushitukiza kwa kuishi kimhemko au mara moja tu. Na jinsi gani ya kujiandaa, uwezo kwa kuchagua, wa ubunifu, ujasiri na shauku? Akijibu swali la Merina Papa amesema inabidi kutambua ni mwelekeo gani wa maisha. Kwa uzoefu wake akiwa kijana kama wao, maisha yake yalikuwa kawaida. Kipindi cha ujana kila mmoja anakipitia kwa kukabiliana na vipindi tofauti vya changamoto. Kwa maana hiyo inabidi kwenda mbele bila kuogopa lakini kamwe wasitembee peke yao kwani Mungu hawaachi peke yao anawashika mkono ikiwa watamwomba. Yeye anasindikiza na kuongoza. Kwa maana hiyo inabidi kujifunza kutofautisha sauti. Je kwa namna gani, kwa njia ya sala ya ukimya na mazungumzo ya ndani ya moyo ambayo yanaleta amani. Mwanga huo wa Mungu unatoa nuru ya kukuondoa katika njia potovu, hisia , mihemko na viburi vinavyogubika. Kwa sababu Bwana anataka kujaribu kutumia akili yao, hisia zao za ndani na shauku. Mungu anataka kuwasaidia kutofautisha kati ya kile kilicho muhimu na kile kinachozidi, yaani kile chema na kile kinachofanya mabaya kwao na wengine, kile cha haki na kinachozalisha ukosefu wa haki na ghasia.
Kwa mungu hakuna aliye mgeni, labda ni binadamu tu mara nyingi anayekuwa mgeni kwake. Mbele ya matukio ya kuchagua, haipaswi kwenda mbele pekee. Inahitajika kuwa na msaidizi. Awali ya yote kabla ya ushauri kutoka kwenye Intarneti, Baba Mtakatifu amewaomba watafute washauri katika maisha, watu wenye hekima na uaminifu ambao wanaweza kuwasaidia. Kwa maana hiyo amefikiria wazazi na walimu, lakini pia hata wazee kwa mfano babu na bibi na watu wa kiroho. Kila mmoja anahitaji kuwa na msindikizaji katika mchakato wa safari ya maisha. Papa Francisko amewambia jinsi ambavyo dunia inawahitaji wao, ubunifu wao, ndoto zao na ujasiri wao, shauku yao na tabasamu, furaha yao inayoambukiza na hata wehu wao kidogo ambao wanajua kupeleka katika kila hali na hata kusaidia kutoka kati mtego wa mazoea, mantiki za kurudia ambazo wakati mwingine zinawagubika maisha yao. Kwa njia hiyo amewathibitisha vijana hao kwamba Kanisa liko pamoja nao na linawahitaji sana wao kwa kila mmoja wao, ili kuweza kupyaishwa, kuvumbua njia mpya, kufanya uzoefu wa lugha mpya, kugeuka kuwa furaha zaidi na karimu. Wasipoteza kamwe ujasiri wa kupenda na kuishi yaliyo makuu. Utamaduni wao waufanye kuwa wa utunzaji na kuuneza, wageuke mabigwa wa udugu, wakabiliane na changamoto za maisha kwa kuacha waelekezwe na ubunifu amifu kwa Mungu na kwa mashauri mema, amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake na amehitimisha kwa maneno haya: God be with you! Allah ma’akum! Dio sia con voi yaani Mungu ae nanyi.