Papa:amani inahitajika kwa watu wa Ukraine wanaoteseka kwa ukatili
Na Angella Rwezaula - Vatican
Ukatili mwingi, ukatili mwingi ndio maneno ya Papa aliyorudia mara mbili na kwa sauti ya kusisimua zaidi, akiondoka katika maandishi yaliyoandikwa kana kwamba anasisitiza kwa maneno ya maumivu na hofu kwa kile ambacho kinaendelea kutesa kwa miezi tisa na idadi ya watu wa Ukraine kutokana na vifo vingi vinavyosababishwa na wale wanaofanya vita. Mabomu, utekaji nyara, ghasia, mateso na mashambulizi hata kwa ndege zisizo na rubani, kama yale yaliyotokea tarehe 8 Novemba 2022 usiku katika jiji la Dnipro. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko ametaka kusasisha mwaliko wake wa kuiombea Ukraine inayoteswa, kwa sababu tangu kuanza ombi lake ambalo halijawahi kukoma kwa ajili ya taifa hilo lililoshambuliwa tangu Februari 24. Katika ombi hilo kwa Mungu, Baba Mtakatifu pia amewahusisha waamini wote waliokuwapo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na wale waliounganishwa kwa njia ya mitandao katika mabara matano.
Papa amesema Tumwombe Mungu wa amani kwa ajili ya watu hawa ambao wanahangaika sana na wanaoteseka kwa ukatili mwingi, ukatili mwingi, kwa upande wa wale ambao wanafanya vita. Wakatili, amerudia neno ambalo tayari limetumika katika mahojiano kwenye ndege wakati wa safari ya kurudi kutoka Bahrain. Usemi ambao pia unaleta akilini shutuma kali zilizotolewa na Papa katika Katekesi ya mwezi Agosti uliopita. "Wale wanaopata mapato kutokana na vita na biashara ya silaha ni wahalifu wanaoua ubinadamu".
Kifo cha Askofu mkuu wa Orthodox wa Cyprus, na kwa huzuni, mkubwa, tena mwishoni mwa katekesi yake Papa pia amekumbuka kifo cha Chrisostomos II, Askofu mkuu wa Kiorthodox wa Cyprus, aliyefariki alfajiri ya tarehe 7 Novemba 2022, akiwa na umri wa miaka 81, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mwezi Desemba mwaka mmoja uliopita alimkaribisha Papa wakati wa safari yake ya kitume kisiwani humo. Na kuhusu safari hiyo, Papa Francisko amesema anakumbuka kwa upendo wa shukrani mikutano ya kindugu ambayo walishiriki huko Cyprus, wakati wa ziara yake mwaka janahuku akiungana na maombolezo ya kitaifa ya watu wa Cyprus, kwa kutoweka kwa yule aliyemtaja kuwa mchungaji mwenye kuona mbali, mtu wa mazungumzo na mpenda amani, ambaye alijaribu kukuza upatanisho kati ya jamii tofauti za nchi hiyo.