Papa amebariki sanamu inayohusu wasio na makazi maalum katika kuelekea siku ya Maskini duniani
Na Angella Rwezaula, – Vatican.
Jumatano tarehe 9 Novemba 2022, wakati wa Katekesi ya Kawaida, Baba Mtakatifu Francisko amebariki Mchongo wa sanamu mpya katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican kwa kutaka kuonesha hali halisi ya watu wasio kuwa na makazi. Sanamu hiyo inaitwa “Sheltering” na ni mchango wenye ukubwa wa kawaida kama mtu ambao unaonesha sura ya hasiye kuwa na malazi akiwa amejifunika na blanketi inayovutwa na Njiwa akiwa anapaa. Ni katika muktadha wa Siku ya 6 ya Maskini Duniani ambayo itaadhimishwa katika Dominika ya 33 ya Kipindi cha Mwaka wa kawaida tarehe 13 Novemba 2022. Mchongo huo umetengenezwa na msanii mkanada Timothy Schmalz, ambaye tayari amefanya uzoefu katika kambi ya sanamu za kidini ulimwenguni pote.
Kazi yake tayari inajulikana ni ile “Malaika bila kujua ” (Angels Unawares), ambayo ilijikita katika kielekezo cha Wahamiaji na Wakimbizi, ambayo iliwekwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mnamo 2019 na ambayo pia ilibarikiwa na Baba Mtakatifu pia . “Sheltering” kwa maana hiyo imewekwa kwa ajili ya kutoa chachu ya kuangazoa matatizo ya wasio na makazi maalum ulimwenguni pote, na kuweza kuwatia moyo wa kutafuta suluhisho thabiti, sambamba na utume wa Kampeni ya nyumba 13 , ambao ni Mpango wa Familia ya Mtakatifu Vincenzo wa Pauli ulimwenguni. Familia Kubwa ya Vincenti ni harakati yenye mashirika tofauti ya kitawa na vyama vya kutme vya kilei pamoja na mashirika ya upendo ambayo yanauhishwa na maisha katika huduma ya Mtakatifu Vincenzo de’ Paoli, ambaye aliwaita wote ambao wawe matajiri na masikini, wanyenyekevu na wenye nguvu kuweza kuhudumia wote kwa zana zote ili kuweza kufafanua maana ya umaskini ambao ni sura inayopendwa na Kristo na chachu ya kusaidia maskini moja kwa moja au kinyume chake (Katiba yao ya Shirika CM. Roma, 29 Juni 1984).
Familia ya Mtakatifu Vincenti kwa maana hiyo imejitoa katika kampeni hiyo ya FamVin Homeless Alliance (FHA), ikiwa na lengo la kufikia hatima ya matukio ya wale wasio kuwa na nyumba na kubadilisha maisha ya watu wapatao bilioni 1,2 ambao duniani kote wanaishi bila nafasi ambayo inaweza kufafanuliwa kama nyumba. Kwa maoni yake kuhusu uzinduzi wa "Sheltering", Mark McGreevy, Mratibu wa Kampeni hiyo ya FHA na Rais wa DepaulInternationalGroup, alithibitisha kuwa Sanamu hiyo inafanya tamko kali sana kuhusu mada ya wale wasio na makazi na inalazimsha kuwa na utambuzi wa watu wasio kuwa na makazi maalum ambao wanazungukia ulimwengu mzima. Kabla ya kutatua matatizo ya wasio na makazi, lazima kuwaelewa. Lazima kusimama na kuwasikiliza historia zao na kuwahusisha katika suluhisho ambayo yanazaa mabadiliko ya muda mrefu. Hakuna ambaye anapaswa abakii bila nyumba. McGreevy mkuu wa FHA kupitia Kampeni ya Nyumba 13, amebanisha kwamba wanataka kukaribisha watu 10,000 ulimwenguni kote, ifikapo mwisho wa 2023, katika zaidi ya nchi 160 ambapo Familia ya Mtakatifu Vincenti tayari inafanya kazi. Kwa mujibu wake alisema Hii ni hatua ya kwanza tu katika mpango kabambe wa kubadilisha maisha ya watu wengi kati ya bilioni 1.2 ambao kwa sasa hawana makazi duniani.
Na kwa upande wake, Tomaž Mavrič, Mkuu wa Shirika la Utume wa Mtakatifu Vincent wa Paulo na Mabinti wa Upendo wa Mtakatifu Vincent wa Paulo alieleza: “Uvuvio wa Yesu na Mtakatifu Vincent wa Paulo unatuongoza kuota ndoto kubwa, lakini kwa unyenyekevu wa kina. Ndoto ni kwamba wakati fulani katika historia wanadamu wote wanaweza kuwa na makazi bora, mahali pazuri pa kuita nyumbani". Hata hivyo Sanamu ya Schmalz iliwasilishwa kwa mara ya kwanza katika wiki muhimu inayohusu tatizo la ukosefu wa makazi duniani kote. Na tarehe 13 Novemba 2022, kwa hakika, Siku ya 6 ya Maskini Duniani itaadhimishwa, ambayo inaakisi dhamira isiyotikisika ya Baba Mtakatifu Francisko kuhusu mada hiyo kwamba: "Ikiwa tunataka maisha kushinda kifo na kwa heshima kuokolewa kutoka kwa udhalimu, njia ni yako: ni kufuata umaskini wa Yesu Kristo, kushiriki maisha kutokana na upendo, kuumega mkate wa kuwepo kwa mtu pamoja na kaka na dada kuanzia na mdogo, wale ambao wanakosa mammbo muhimu, ili usawa uundwe, maskini ni huru kutoka katika taabu na tajiri kutoka ubatili, wote wawili bila kuwa na matumaini ”.
Ikumbukwe Siku ya Maskini Duniani ilianzishwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa Waraka wake wa kitume wa Misericordia et Misera, yaani, Huruma na Maskini, iliyochapishwa mnamo tarehe 20 Novemba 2016 wakati wa kuhitimisha mwisho wa Jubilei maalum ya Huruma. Tangu wakati huo kunzia mwaka 2017, kila mwaka katika Dominika ya 33 ya kipindi cha Mwaka wa kawaida, inaadhimishwa tukio hilo la Siku ya Maskini duniani.