Papa:Michuano ya mpira isaidie makutano,udugu na amani kati ya watu
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake na kuanza salamu zake, katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, Jumatano tarehe 23 Novemba 2022 amewasalimia wachezaji, washabiki na watazamaji ambao wanafuatilia tukio la mpira wa kuwania Kombe la Dunia huko Qatar kwamba: “ Mchezo wa mpira wa dunia unaoendelea Qatar uwe ni fursa ya kukutana na maelewano kati ya mataifa na kusaidia udugu na amani kati ya watu”.
Mateso ya kutisha kwa watu wa Ukraine
Katika dunia ya leo, iliyoharibiwa na vita, sala ya Papa Francisko ni kwa ajili ya amani duniani na mwisho wa migogoro yote, kwa namna ya pekee mawazo yake yamewandea kwa mateso ya kutisha ya watu wa Ukraine waliouawa. Katika fursa ya Sherehe ya Jumamosi 26 Novemba ya ukumbusho wa Holodomor, inayojikita kuangamizwa na njaa ya 1932-33 ambayo ilisababishwa na Stalin, pia ni fursa sio tu ya kuwaombea waathirika wa mauaji hayo ya kimbari, lakini pia kwa Waukraine wengi, watoto, wanawake na wazee, watoto wanaoteseka kuuawa kwa sababu ya uchokozi leo hii.
Papa amesali kwa ajili ya waathirika wa tetemeko Indonesia
Baba Mtakatifu Francisko amekuwa na wa sala kwa ajili ya watu waliokufa na majeruhi wa Indonesia ambao wamepata janga la tetemeko la ardhi mnamo tarehe 21 Novemba 2022 katika kisiwa cha Giava, ambapo wamekufa watu zaidi ya 250. Baba Mtakatifu Francisko mawazo yake yameelekea hata haki za wavuvi ambapo amesema kwa kazi yao katika Siku ya Kimataifa ya Uvuvi iliyofanyika tarehe 21 Novemba inachangia usalama wa vyakula, lishe na kupunguzwa kwa umasikini duniani. Baba Mtakatifu Francisko amepongeza mpango wa RedWeek in Polonia, yaa Mpango wa Juma ljekundu nchini Poland linalojikita kuwakumbuka wakristo wanaoteseka na vijana wa siku ya vijana Lisbon (WYD) itakayofanyika mwaka kesho.
Padre Ambrosoli na salamu kwa Wascalabrini
Baba Mtakatifu Francisko pia amemkubuka Padre Giuseppe Ambrosoli, mmisionari wa Kikomboni na daktari aliyetangazwa kuwa mwenyeheri Dominika 20 Novemba 2022 huko Kalongo nchini Uganda, mahali ambapo alifia mnamo 1987. Ushuhuda wake maalumu usaidie kila mmoja wetu kuwa na hadhi ya Kanisa moja linalotoka Nje. Hata hivyo kabla ya kuanza katekesi, Baba Mtakatifu alikuwa amekutana na Kikundi cha Kimataifa cha Mtandao wa Wahamiaji cha Shirika la Wascabrini, amewashukuwa kwa ujio wa ona kwa kazi yao inatimizwa kwamba Bwana awabatiki wote na kuwatakia kwamba waweze kwenda mbele kwa kazi hiyo hiyo.