Papa:Faraja haijaribiwi ni zawadi ya Roho Mtakatifu

Katika katekesi yake Papa inayoongozwa na mada ya Utambuzi,ameeleza kipengele cha tisa kuhusu ‘faraja’ ambayo ni mwanga wa roho,unaoruhusu ufamilia na Mungu,inatoa amani na matumaini na kusaidia kuona Baba hata katika uchungu,lakini lazima kutambua kutofautisha kati ya faraja za uongo zinazopelekea kujifungia binafsi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumatano tarehe 23 Novemba 2022, ameendlea na mada ya Utambuzi kwa kujijita katika kipengele cha tisa za faraja. Baba Mtakatifu akianza amesema kwamba “Tuendelee na katekesi kuhusu utambuzi wa roho: kama inavyotokea kutambua kwa kile kitokezacho katika moyo wetu na katika roho yetu. Na baada ya kuzingatia baadhi ya mantiki ya kuwa na upweke, yaani giza la roho, leo tuzungumze kuhusu faraja ambayo ni mwanga wa roho na ambayo ni sehemu nyingine muhimu kwa kufanya mang’amuzi, na ambayo haipaswi, kudharauliwa, kwa sababu inaweza kujikopesha kwa kutokuelewana, na wale ambao hawaeleweki. Sisi tunapaswa kutambua nini maana ya faraja. Je ni nini maana ya faraja ya kiroho? Ni uzoefu wa furaha ya ndani, ambayo inaruhusu kutazama uwepo wa Mungu kwa mambo yote; na hiyo inatoa nguvu imani na matumaini na hata uwezo wa kufanya mema. Mtu anayeishi kwa faraja, hawezi kukata tamaa mbele ya matatizo kwa sababu anafanya uzoefu wa amani ya nguvu zaidi ya majaribu. Hii ni zawadi kubwa kwa maisha ya kiroho na kwa maisha yote katika ujumla wake. Ni muhimu kuiishi furaha hii ya kiundani.

Katekesi ya Papa 23 Novemba
Katekesi ya Papa 23 Novemba

Baba Mtakatifu akiendelea na mada hiyo amesema faraja ni vuguvugu la ndani, ambalo lingusa kwa kina sisi wenyewe. Halionekani, lakini ni laini, nyeti, kama tone la maji juu ya sifonji (Ignazio di L., Mafungu ya kiroho, 335): mtu anahisi kufunikwa na uwepo wa Mungu kwa namna ambayo daima ya heshima ya uhuru wake. Kamwe sio jambo hambalo haliendani, hapana, ambalo linatafuta kushurutusha utashi wetu, na hata si furaha ya kupita: kinyume chake, kama tulivyoona, hata uchungu, kwa mfano wa dhami binafsi inaweza kuwa sababu ya farijiwa. Tufikirie uzoefu aliouishi Mtakatifu Agostino, wakati anazungumza na Mama Monika kuhusu uzuri wa maisha ya milele: au ukamilifi wa furaha ya Mtakatifu Francis wa Assisi ambaye hata hivyo anahusisha hali ngumu sana za kubeba; na kufikiria watakatifu wengi, kike na kiume ambao walitambua kufanya mambo makubwa, si kwa sababu walijizingatia kuwa ni wenye akili na wenye uwezo, lakini kwa sababu waliweza kupata utamu wa amani ya upendo wa Mungu.

Katekesi ya Papa 23 Novemba
Katekesi ya Papa 23 Novemba

Ni amani ambayo alikuwa anaelewa kwa mshangao Mtakatifu Ignatius alipokuwa akisoma maisha ya watakatifu. Kufarijiwa ni kukaa kwa amani na Mungu, kuhisi kuwa kila kitu kimewekwa kwa amani na kila kitu kina maelewano ndani mwetu. Ni amani ambayo alihisi Edith Stein baada ya uongofu; mwaka mmoja baadaye akapokea Ubatizo, na anaandika kuwa:  “ Wakati nilijikabidhi ndani ya hisi hiyo  kidogo kidogo maisha mapya yalianza kunituliza na bila hata mvutano wa utashi wangu, kunisukuma kuelekea timilifu mpya. Mtiririko huu muhimu unaonekana kutoka katika  shughuli na kutoka kwa nguvu ambayo si yangu na ambayo, bila kunifanyia vurugu yoyote, inakuwa hai ndani yangu”(Saikolojia na Sayansi ya roho, Città Nuova, 1996, 116).” Papa Francisko ameongeza “Yaani amani ya kweli ni amani inayofanya hisia nzuri kuchipua ndani yetu. Faraja itazama awali ya yote tumaini, ni matazamio ya wakati ujao , inakuweka katika mchakato wa safari, inaruhusu kuanza mambo ambayo hadi wakati ule uliaacha daima, au hata kuyafikiria, kama ule  Ubatizo wa Edith Stein.  Kwa maana hiyo Faraja ni amani hiyo lakini ambayo si kwa kubaki pale umekaa na kustarehe, hapana, inakupatia amani na kukuvuta kuelekea kwa bwana na kukuweka kwenye mchakato wa safari ili ufanye mambo, ili kufanya mambo mema. 

Katekesi ya Papa 23 Novemba
Katekesi ya Papa 23 Novemba

Katika kipindi cha faraja, ikiwa sisi tumefarijika, tunakuwa na shauku ya kufanya mema daima. Kinyume chake inapokuwa ni kipindi cha ukavu, utashi wetu ni ule wa kujifungia binafsi na bila kufanya lolote… Faraja inasukuma mbele, katika huduma ya wengine, ya jamii, na watu. Faraja ya kiroho haiwezi kujaribiwa na huwezi kusema sasa faraja itakuja... hapana, haiwezi kufanyiwa majaribio na haiwezi kupangwa kwa mapenzi, ni zawadi ya Roho Mtakatifu. Inaruhusu kuwa na mazoea ya kifamilia na Mungu ambaye utafikiri anafuta umbali. Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, akifanya hija Roma akiwa na miaka 14, katika Madhabahu ya Msalaba Mtakatifu wa Yerusalemu, alitafuta kuugusa msumari na kuubusu, mmoja kati ya ile iliyomsulibisha Yesu. Teresa alihisi ujasiri wake huo kama usafiri wa upendo na usadikisho. Na baadaye akaandika “ilikuwa kweli ujasiri mkubwa. Lakini Bwana anatazama kina cha mioyo, anajua kuwa nia yangu ilikuwa safi […].  Nilikuwa nikitenda kama mtoto ambaye anaamini kila kitu kinachorohusiwa na kufikiria kama thamani binafsi za Baba” (Maandiko ya mkono wake Teresa, 183).

Baba Mtakatifu ameongeza kusema: “Kwa hivyo aliandika. Ni ya hiari: faraja inakuongoza kufanya kila kitu kwa hiari, kana kwamba sisi ni watoto. Watoto ni wa hiari, na faraja hukuletea, ndio, kwa utamu, na amani kubwa sana”. Kisichana cha miaka kumi na nne kinatupatia ufafanuzi angavu wa faraja ya kiroho: alihisi maana ya huruma kutoka kwa Mungu ambayo inafanya kuwa na shauku kubwa ya kushiriki maisha yake, ya kufanye kile ambacho yeye anapenda, kwa sababu tuhisi ufamilia na Yeye, tunahisi kuwa nyumba yake ni nyumba yetu, tunahisi kukaribishwa, kupendwa na kufarijiwa. Kwa faraja hiyo hatupaswi kukata tamaa mbele ya tatizo: kiukweli kwa shauku sawa na hiyo Teresa aliomba Papa ruhusa ya kuingia Shirika la Wakarmeli, kwa sababu yeye wakati ule alikuwa ni kijana mdogo sana na akakubaliwa.

Katekesi ya Papa 23 Novemba
Katekesi ya Papa 23 Novemba

Je hiyo inatualeza nini? Inaeleza kuwa faraja inatufanya kuwa na shauku, wakati tunapokuwa na wakati wa giza, ukavu na tunawaza  kusema kwamba sina uwezo wa kufanya hilo. Ukavu unakuangusha chuni. Unaona kila kitu ni giza na kusema mimi sina uwezo wa kufanya lolote. Lakini je una uhakika? Na kumbe ukihisi nguvu ya Mungu unakwenda mbele na ndiyo fraja inayo kusukuma kwenda mbele na kufanya mambo ambayo wakati wa ukavu huna uwezo na usingekuwa na uwezo wa kufanya hivyo,  hasa katika  kupiga hatua ya kwanza mbele. Huo ndio uzuri wa faraja. Lakini tuwe makini Papa ameonya. Ni lazima tutofautishe waziwazi juu ya faraja ambayo inatoka kwa Mungu, na faraja za uongo. Kitu kama hicho kinatokea katika maisha ya kiroho na kwa kile kinachotokea katika wanadamu: kuna asili na kuna uigaji. Ikiwa faraja ya kweli ni kama tone kwenye sifonji, ni laini na ya karibu, miigo yake ni ya sauti zaidi na ya kujionesha zaidi, ni shauku safi, ni moto katika nyasi, bila uthabiti, hutuongoza kujiondoa ndani yetu na sio kuwajali wengine. Faraja ya uwongo hatimaye hutuacha na utupu, mbali na kitovu cha maisha yetu. Kwa hilo ni lazima, tunapojisikia furaha, amani, tuna uwezo wa kufanya chochote kuitambua. Lakini tusichanganye amani hiyo na shauku unayopitia, kwa sababu shauku hiyo ipo leo hii na baadaye inaanguka na kutoweka.

Katekesi ya Papa 23 Novemba
Katekesi ya Papa 23 Novemba

Kwa sababu hiyo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa inabidi kufanya mang’amuzi hata ikiwa tunahisi kufarijika. Kwa sababu uongo wa faraja unaweza kugeuka hatari, ikiwa tunatafuta kama huo wenyewe kwa namna kali. Na kusahau Bwana. Kama ambavyo angesema Mtakatifu Bernardo, kwamba: “Wanatafuta faraja za Mungu na hawatafuti Mungu katika faraja. Kwa maana hiyo ameongeza kusema:  “sisi lazima kutafuta Bwana na Bwana kwa uwepo wake, atufarji, atufanye twende mbele. Na sio kutafuta Mungu ambaye anatupeleka katika faraja, hapana! Sio hivyo hatupaswi kujihusisha na matakwa hayo binafasi ya kichini chini. Huo ni mwenendo wa Mtoto ambaye alizunguziwa wakati wa katekesi iliyopita ambaye alikuwa akitafuta wazazi wake kwa sababu  kupata vitu  lakini si kwa ajili ya mambo ya wazazi. Baba, Mama na watoto wanajua kufanya mambo hayo, wanajua kufanya mchezo huo, na ikiwa familia inakuwa kinyume, wanakuwa na tabia ya kutafuta hapa na pale na hiyo sio faraja bali ni mafao. Hata sisi tuko hatarini ya kuhisi uhusiano na Mungu kwa tabia ya kitoto, kumtafuta kwa ajili ya mafao, kumpunguzia katika kitu  chetu cha kutumia, na huku tunapoteza zawadi iliyo kubwa ambayo ni Mungu. Kwa maana hiyo tunapaswa kwenda mbele katika maisha yake ambayo yanakwenda kati ya faraja za Mungu na ukavu wa dhambi za ulimwengu, lakini kwa kujua kutofautisha na kwa kujua kutofautisha ikiwa faraja ni za Mungu ambazo zinakupatia amani ya roho ya kina na inapokupatia shauku za kijuu juu ambazo si mbaya, lakini si faraja ya Mungu pia.

Katekesi ya 23 Novemba
23 November 2022, 15:40