Papa Francisko huko Asti akutana na binadamu yake Carla
Na Angella Rwezaula
Katika Dominika ya XXXIV ya Mwaka, tarehe 20 Novemba ambayo ni Sherehe ya Kristo Yesu Mfalme wa Ulimwengu, sambamba na Siku ya 37 ya vijana Kijimbo, kwa upande wa Baba Mtakatifu imemkuta katika ziara ya kichungaji jimbo katoliki la Asti Italia.
Ziara yake ilianza Jumamosi tarehe 19 Novemba 2022 kwa nia ya kumtembelea binadamu yake Carla Rabezzana anayeishi mjini Portacomaro, ili kumpongeza na kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 90 ya kuzaliwa. Lakini pia hata kuwaona ndugu zake ambao alikutana nao kwa karibu ambayo itahitimishwa kwa kuadhimisha Misa Takatifu kwa matukio yote katika Kanisa kuu la Jimbo Katoliki la Asti, Kaskazini mwa Italia.
Kwa upande mwingine siku ya leo ni ya kipekee kwa sababu ndiyo siku ambayo vijana wanaungana na Maaskofu, pamoja na viongozi mahalia kuadhimisha Siku ya XXXVII ya Vijana Ulimwenguni katika ngazi ya kijimbo ambayo inaongozwa na kauli mbiu: “Basi Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda” (Lk 1:39). Ni mada ambayo itaongoza Siku ya Vijana Kimataifa itakayoadhimishwa katika jimbo kuu la Lisbon nchini Ureno kuanzia tarehe 1-6 Agosti 2023.
Kwa upande wa Video fupi iliyoko juu inaonesha matukio ya Baba Mtakatifu Francisko kwa siku ya Jumamosi kuanzia Vatican hadi kuufika huko Asti kutembelea maeneo, kupokelewa na Binadamu yake hata kutembelea kituo cha wakaribishwa hasa wenye kuhitaji