Tafuta

Papa amekutana na Tume ya Kimataifa ya Taalimungu Papa amekutana na Tume ya Kimataifa ya Taalimungu 

Papa Francisko kwa watalimungu:enendeni zaidi ya mapokeo sio kurudi nyuma

Katika mkutano na wajumbe wa Tume ya Kimataifa ya Taalimungu,iliyoanzishwa na Mtakatifu Paulo VI mwaka 1969,Papa amezungumzia uaminifu wa ubunifu kwa Mapokeo na ameshauri kuwa na imani na upendo kwa kujitolea kutekeleza huduma ya taalimungu kwa njia ya mchakato kisinodi ambao una uwezo kutokea kusikiliza,kujadiliana na kutambua.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana Alhamisi tarehe 24 Novemba 2022 na Tume ya Kitaalimungu kimataifa ambap amemshukuru Kardinali Luis Francisco Ladaria Ferrer, S.I., Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa pa Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Rais wa Tume ya Kipapa ya Kanisa la Mungu , Tume ya Kipapa ya Biblia Takatifu na Tume ya Taalimungu Kimataifa kwa maneno na kuwashukuru wote kwa ukarimu, umahiri na upendo ambao wanauweka katika huduma yao katika mwaka wao wa tano wa shughuli ya Tume ya Kitaalimungu kimataifa. Ameshukuru kwa zana ambazo leo hii wanazo na wamweze kuanza kuazana nazo kwa kazi ya umbali, kwa kushinda tatizo ambalo lilitokana na janga la uviko. Papa amepongeza hata kukaribisha mapendekezo ya mada tatu wazojikita nazo: Ya kwanza ni ile ya sasa ambayo haiwezi kuanza na daima kutoa matunda ya imani ya kikristo iliyoaminia na Mkutano wa Nicea, katika kuhitimisha miaka 1700 tangu kunza kwake mnamo (325-2025).

Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa
Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa

Pili ni uchunguzi wa baadhi ya masuala ya kianthropolojia yanayojitokeza leo hii na yenye umuhimu mkubwa kwa safari ya familia ya kibinadamu, katika mwanga wa mpango wa kimungu wa wokovu; na ya tatu ni kuongezeka kwa kina ambapo  leo inazidi kuwa wa dharura na maamuzi  ya taalimungu ya uumbaji katika mtazamo wa Utatu, kusikiliza kilio cha maskini na cha dunia. Kukabiliana mada hizi , Tume ya Kitaalimungu Kimataia inaendelea na jitihada za upyaisho na huduma yake. Papa amewaalika  kulitekeleza baada ya kufuatiwa na Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, ambao kwa  miaka sitini baada ya kuanzishwa kwake, ndio dira ya uhakika ya safari ya Kanisa,  ya sakramenti katika Kristo, ya muungano na Mungu na umoja wa wanadamu wote(Katiba dogm. Lumen gentium, 1).

Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa
Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa

Kwa maana hiyo baba Mtakatifu Francisko amependa kutazama na kuwalekeza miongozo mitatu ya hatua katika kipindi hiki cha kihistoria: wakati mgumu bado, kwa mtazamo wa imani, uliojaa ahadi na tumaini linalotiririka kutoka katika Pasaka ya Bwana aliyesulubiwa na kufufuka. Mwongozo wa kwanza ni ule wa uaminifu wa ubunifu kwa maokeo. Ni suala la kudhani kwa imani na upendo na kushuka kwa ukali na uwazi kujitolea kutekeleza huduma ya taalimungu,   kusikiliza Neno la Mungu, maana ya imani  ya Watu wa Mungu, Majisterio na karama, na katika kupambanua alama za nyakati,  kwa ajili ya kuendeleza Mapokeo ya Kitume, kwa msaada wa Roho Mtakatifu, kama ilivyoandikwa kwenye Wosia wa Neno la Mungu (Dei Verbum  n. 8). Hakika, Papa Mstaafu Benedikto wa kumi na sita alielezea Mapokeo kama "mto ulio hai ambao asili yake huwepo daima" (Katekesi, Aprili 26, 2006); ili "kumwagilia ardhi tofauti, kulisha  sehemu za mbali kijiografia tofauti, na kuifanya nchi iwe  bora zaidi, iliyo bora zaidi ya utamaduni huo.

Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa
Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa

Kwa njia hii, Injili inaendelea kufanyika mwili katika pembe zote za dunia, kwa njia mpya daima” (rej. Veritatis gaudium, 4d). Baba Mtakatifu ameongeza kusema kwamba mapokeo, asili ya imani au inakua au inazimika. Kwa sababu alikuwa anasema mmoja wa wana muziki kuwa utamaduni na uhakika wa wakati ujao n asio kipande cha makumbusho. Ndio unafanya kukua Kanisa kutoa chini kwenda juu kama mt ina mizizi.  Badala yake, mwingine alisema kwamba jadi ni "imani mfu ya walio hai": unapojifungia hapo. Mapokeo kwa kusisitiza hapo Papa amesema hutufanya twende katika hilo, kwa mwelekeo huo: kutoka chini hadi juu: yaani kuwa wima. Leo hii kuna hatari kubwa, ambayo ni kurudi katika mwelekeo mwingine: yaani wa kurudi "nyuma". Kwa mfano amesema kwenda nyuma ina maana ya kusema kwamba , daima ilifanyika hivyo, ni vema kurudi nyuma , ambamo kuna uhakika, n asio kwenda mbele na mapokeo. Mwelekeo huu wa mlalo, kama tulivyoona, umesogeza baadhi ya harakati , vyama vya Kanisa, kubaki wima kwa wakati fulani, kurudi nyuma. Wao ndio walio nyuma.

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba harakati fulani amesema ili kuleta kitu cha kihistoria au kilichozaliwa mwishoni mwa Mtaguso wa Kwanza wa Vatican,  katika kujaribu kuwa mwaminifu kwa mpokeo kwa hivyo leo hii wanakua katika mfumo wa kuagiza zawadi na vitu vingine. Nje ya mwelekeo huo wa  wima, ambapo hukua, dhamiri ya kimaadili hukua, dhamiri ya imani hukua, pamoja na kanuni hiyo nzuri ya Vincent wa Lérins aliyosema 'ut annis consolidatetur, dilatetur tempore, consolidatetur aetate', yaani ‘kuunganishwa katika miaka, kuongezwa kwa wakati, kuunganishwa katika umri’. Na hii ndiyo kanuni ya ukuaji. Badala yake, kurudi nyuma kunakuongoza  fikiraza  zifuatazo: daima imefanywa kwa njia hiyo, ni bora kwenda kwa njia hiyo, na haikuruhusu kamwe kukua. Katika hatua hiyo amesema  kwamba wanataalimungu lazima wafikiri kidogo  ili kusaidia.

Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa
Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa

Mwongozo wa pili unahusu fursa, ili kutekeleza ipasavyo na kwa dhati kazi ya kukuza na kukuza Injili, kuwa wazi kwa uangalifu katika  mchango wa taaluma mbalimbali kutokana na mashauriano ya wataalam, wakiwemo wasio Wakatoliki, kama inavyotarajiwa kwenye Sheria za Tume (taz. n. 10). Hili ni suala ambapo Papa alitaka kuliibua katika Waraka wa Kitume wa  Veritatis gaudium  yaani ….- ya kufanya kuthamini "kanuni ya utofauti wa nidhamu: sio sana katika muundo wake "dhaifu" wa taaluma nyingi, kama njia ambayo inapendelea uelewa bora kutoka katika  maoni mengi ya kitu cha kujifunza; bali kutoka katika hali yake ya "nguvu" ya uasi, kama uwekaji na uchachushaji wa maarifa yote ndani ya nafasi ya Nuru na Uzima inayotolewa na Hekima itokayo katika Ufunuo wa Mungu.(n. 4c).

Hatimaye, mwongozo wa tatu ni ule wa ushirikiano. Unapata umuhimu fulani na inaweza kutoa mchango maalum katika muktadha wa mchakato wa sinodi ambamo Watu wote wa Mungu wanakusanyika katika kipiengele cha 75 kinasema: “Kama ilivyo kwa wito mwingine wowote wa Kikristo, huduma ya mwanataalimungu , pamoja na kuwa mtu binafsi, ni wa jumuiya na wa pamoja. Kwa hiyo sinodi ya kikanisa inawafanya wanataalimungu  kufanya taalimungu katika mfumo wa sinodi, wakikuza miongoni mwao uwezo wa kusikiliza, majadiliano, kutn’amua na kuunganisha wingi na aina mbalimbali za  watu na. michango". Wanataalimugu lazima waende zaidi yak wa kutafuta kwenda zaidi. Lakini hiyo ametofauitisha kama katekista, Katekesta lazima atoa mafundisho sahihi, mafundisho yenye msimamo , na hata mapya , baadhi ni mema lakini thabiti. Katekesia aeneza mafundisho thabiti. Kwa mtaalimungu anayehatarisha  kwenda mbele zaidi, itakuwa ni majisterio ambayo itamzuia.

Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa
Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa

Lakini wito wa mtaalimungu siku zote anaendesha hatari ya kwenda mbele zaidi, kwa sababu anatafuta, na anajaribu kuifanya taalimungu iwe wazi zaidi. Lakini usiwahi kutoa katekesi kwa watoto na watu wenye mafundisho mapya ambayo wewe huna uhakika. Mgawanyiko huu sio wangu, ni Mtakatifu Ignatius wa Loyola, ambaye Papa anaamini kwamba  alielewa kitu kuliko yeye. Kwa hivyo Papa amewatakia katika roho hii ya kusikilizana, mazungumzo na utambuzi wa jumuiya, ufungue sauti ya Roho Mtakatifu, kazi tulivu na yenye matunda. Mada walizokabidhiwa na utaalamu wao ni muhimu sana katika hatua hii mpya ya utangazaji wa Injili ambayo Bwana anatuita tuishi kama Kanisa katika huduma ya udugu wa ulimwenguni pote katika Kristo. Kwa hakika, tunatualika tuwe macho kikamilifu kwa mfuasi ambaye, kwa mshangao mpya daima, anatambua kwamba Kristo, “hasa kwa kufunua siri ya Baba na ya upendo wake, pia humfunua mwanadamu kwa ukamilifu na kumdhihirisha yeye aliye mkuu wake (Gaudium et spes, 22); na hivyo anatufundisha kwamba “sheria ya msingi ya ukamilifu wa binadamu, na kwa hiyo pia ya mabadiliko ya ulimwengu, ni amri mpya ya upendo.” (Gs, 38).

Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa
Papa amekutana na Tume ya Taalimungu Kimataifa

Baba Mtakatifu ameongeza kusema kwamba na neno moja alisema, la mshangao  na kwamba  ni muhimu, labda sio sana kwa watafiti lakini ndio kwa maprofesa wa taalimungu , kujiuliza ikiwa masomo ya taalimungu huibua  mshangao kwa wale wanaoyafuatilia. Hiki ni kigezo kizuri, kinaweza kusaidia. Kwa kuhitimisha ameshukuru tena huduma yao yenye thamani ambayo kweli ni yenye thamani. Kwa moyo amewabariki kila mmoja na washirika wao. Amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake. Kwa kuwatamza washiriki hao amesema kwamba anafikiri ni muhimu kuongeza idadi ya wanawao , si kwamba ni katika mtindo lakini kwa sababu wao wana mawazo tofauti na wanaume na wanaifanya taalimungu  kuwa kitu cha ndani zaidi na kitamu zaidi pia.

Hotuba ya Papa kwa wataalimungu kimataifa
24 November 2022, 15:40