Papa Francisko katika katekesi amesema Mazungumzo ni oksijeni ya amani!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kukutana na waamini na mahujaji waliofika kutoka pande za dunia kwenye Katekesi Jumatano tarehe 9 Novemba 2022, katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican amesema kwamba, Kabla ya kuzungumza kile nilichoandaa, ninataka kutoa umakini juu ya watoto wawili waliokuja hapa. Hawa hawakuomba ruhusa, hawakusema tunaogopa, wamekuja moja kwa moja. Ndivyo tunapaswa hata sisi kuwa na Mungu, moja kwa moja. Hawa wametupatia mfano wa jinsi ya kuwa na mwenendo na Mungu, na Bwana, kwenda mbele! Yeye anatusubiri daima. Nimefurahi kuona imani ya watoto hawa wawili na uhuru. Baada ya kumaliza kueleza hili ameanza kujikita juu ya ziara yake ya kitume katika Ufalme wa Bahrein, ambayo amekiri kwamba alikuwa haijua kweli na alikuwa hajui vizuri ufalme huo ulivyo. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amependa kushukuru wote ambao wanalimsindikiza katika ziara kwa msaada wa sala na kupyaisha utambuzi wa shukrani kwa Mfalme, Mamlaka nyingine, kwa Kanisa mahalia na watu kwa joto la makaribisho. Na vile vile amependa kuwashukuru waandaaji wa safari, kwani ili kufanya safari hiyo walikuwa ni watu wengi.
Baba Mtakatifu amekuta na utambuzi wa shukrani kwa Katibu wa Vatiana aliyejitika kufanya maandalizi makubwa ya hotuba, kuandaa kila kitu na wengi wanahusishwa, baadaye kuna kutafsiri, vikosi vya Ulinzi hata wa vya Kiswiss ambao wanafanya vizuri. Kwa maana hiyo ameongeza kuwa ni kazi kubwa! Kwa wote amependa kupyaisha shukrani zake kwa kile ambacho wanafanya kwa sababu amesema ili safari ya Papa iweze kuwa kufanikiwa. Baba Mtakatifu ameongeza kwamba inamjia akilini tu kwa haraka kuuliza ni kwa nini Papa alipendelea kutembelea Nchi hiyo ndogo yenye wingi wa kiislam? Ikiwa kuna nchi nyingi za Kikristo, na kwa sababu gani hakwenda katika moja ya nchi hiyo au nyingine kati ya hizo? Papa amependa kujibu maswali hayo kwa maneno matatu: mazungumzo, mkutano na mchakato wa safari.
Akianza na mada ya Mazungumzo amesema fursa ya safari hiyo iliyotamaniwa sana ilitokana na mwaliko wa Mfalme kwenye Jukwaa kuhusu Mazunguzmo kati ya Mashariki na Magharibi. Mazungumzo ambayo yanasaidia kugundua utajiriuliopo kwa watu wengine, tamaduni nyingine na imani nyingine. Huko Bahrain ni kisiwa kilichoundwa na visiwa vidogo ambacho amesema kimetusaidia kujua kwamba hatupaswi kuishi tumejibagua, lakini kwa kukaribiana. Huko Bahrain ambalo ni kisiwa kimojawapo wanakaribiana na wanachanua. Inahitajika suala hilo kwa sababu ya amani, na mzungumzo ambayo ni oksijeni ya amani. Papa ameomba kwamba kuwa wasisahau hili mazungumzo kwamba ni oksijeni ya aman. Hata katika maisha ya nyumbani. Ikiwa yanafanyika malumbano kati ya mwanamme na mwanamke, baadaye yafanyike mazungumzo kwa amani. Katika familia, mazungumzo pia yanahitajika kwa sababu mazungumzo yanahifadhi amani.
Karibu miaka 60 iliyopita ya Mtaguso wa II, kwa kuzungumzia juu ya ujenzi wa amani walikuwa wanathibitisha kuwa katika kazi hiyo inahitaji kuwa watu wanaopanua akili yao na mioyo yao, mbali na mipaka yao ya taifa, kwa kuachia mbali kila ubinafsi wa kitaifa na kila mapendeleo ya madaraka juu ya mataifa mengine na kumwilishwa kwa maana hiyo na mantiki ya kina kuelekea ubinadamu wote, ambao unazima ugumu kuelekea umoja kamili (Gaudium et spes, 82). Huko Bahrain kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu Francisko amebainisha alivyohisi hitaji hilo na kuwataka ulimwengu wote wahusika wa kidini na kiraia watazame nje ya mipaka yao, jumuiya zao kwa ajili ya kutunzana pamoja. Ni kwa kufanya hivyo tu inawezakana kukabiliana na mada fulani za ulimwengu kwa mfano zile za kusahau Mungu, janga la njaa, ulinzi wa kazi ya uumbaji, na amani. Na kwa pamoja inawezekana kufikiriwa hayo.
Jukwaa kwa ajili ya mazungumzo kwa jina la “Est e Ovest per la coesistenza umana”, Magharibi na Mashariki kwa ajili ya kuishi kibinadamu, kwa maana hiyo lilitoa ushauri wa kuchagua njia ya kukutana na kukaa kinzani. Ni jins gani inahitajika hali hiyo ya kukutana, Papa Francisko amesisitiza. Aidha amefikiria juu ya uwehu wa vita, ambapo waathirika wanaoteseka huko Ukraine na migogoro mingine mingi ambayo haitasuhuluhishwa kamwe kwa njia ya mantiki za kitoto za silaha, lakini ni kwa njia ya nguvu ya mazungumzo ya upole. Zaidi ya Ukraine, ambayo inateseka, lakini Papa amesema inawezekana kufikiria vita vingine ambavyo vimedumu kwa miaka, na kufikira uko Siria zaidi ya miaka 10! Kufikiria watoto wa Yemen na huko Myanmar, kwa wastani kila mahali! Kwa sasa iliyo karibu ni Ukraine, na vita hivyo vinafanya nini? Vinaharibu ubinadamu na kuharibu kila kitu. Migogoro hawezi kutatuliwa kwa njia ya vita. Haiwezekani kuwapo mazunguzmo bila kuwapo neno la pili la Mkutano.
Baba Mtakatifu Francisko ameendelea kuelezea kuwa huko Bahareni walikutana na mara nyingi alisikia kuibuka kwa shauku ambayo kati ya Wkristo na Waislam mikutano inaongezeka, ambayo inaimarisha mahusiano thabiti, na yanajikita kwa kiasi kikubwa ndani ya moyo. Huko Bahrain kama watumiavyo utamaduni wa huko magharibi, watu wanaweka mkono wao katika kifua cha moyo kama ishara ya kusalimana. Kwa maana hiyo hata yeye alifanya hivyo ili kuweka nafasi ndani yake aliyekuwa akikutana naye, kwa sababu bila ukarimu, mazungumzo yanabaki utupu ya kijuujuu, yanabaki masuala ya mawazo ambayo sio ukweli. Kati ya mikutano mingi, Papa Francisko amekumbuka kwa mara nyingine tena ya Kaka yake Imam Mkuu wa Al-Azhar, na aule wa vijana katika Shule ya Moyo Mtakatifu, wanafunzi ambao walimpatia mafundisho kwa sababu wanasoma kwa pamoja Wakristo na Waislamu.
Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kwamba, Tangu utoto na ujana lazima kujijua, kwa namna ya kwamba mkutano wa kidugu unajitokeza, ili kupinga migawanyiko ya kiitikadi.Baba Mtakatifu Francisko amependa kushukuru Shule ya Moyo Mtakatifu, Sr. Rosalyn mkuu wa Shule hiyo ambaye anaendesha vizuri na vijana walioshirikishisha ushuhuda wao, kwa sala, ngoma na nyimbo, na anakumbuka vizuri hivyo ameshukuru sana. Lakini pia Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka wazee ambao walitoa ushuhuda wa hekima kidugu, na kwa maana hiyo amekumbuka mkutano wa Muslim Council of Elders, yaani Baraza la Kiislamu la Wazee ambalo ni Shirika la Kimataifa, lililoanzishwa miaka ya hivi karibuni ambalo linahamasisha uhusiano mwema kati ya jumuiya za kiislamu, katika kujikita juu ya kuheshimiana , utaratibu na amani, wakipinga itikadi kali na vurugu.
Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo ameelekea katika neno la tatu la safari. Katika ziara yake huko Bahrain amesema haipaswi kuonekana kama matukio yaliyotenganaisha, kwa maana yanafanya kuwa sehemu ya mchakato wa safari iliyozinduliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II alipokwenda huko Morocco. Kwa maana hiyo ziara yake ya kwanza katika Ufalme wa Baharain imewakilishwa kwa mara nyingine tena, Mchakato wa safari kati ya waamini Wakristo na Waislamu. Si katika kuchanganya au kupuuza imani hapana, si mazungumzo yaliyochakachuliwa, bali kwa ajili ya kijenga mshikamano kidugu katika jina la Baba Ibrahimu, ambaye alikuwa mhujaji juu ya ardhi chini ya mtazamo wa huruma ya Mungu mmoja wa Mbingu, Mungu wa amani. Kwa njia hiyo, kauli mbiu ya ziara yake ilikuwa “Amani duniani kwa watu wenye mapenzi mema”. Baba Mtakatifu Francisko ameuliza kwa nini anasema kuchakachua? Kwa sababu ili kufanya mazungumzo kunatakiwa kuwa na utambulisho binafsi, inapaswa kuanzia na utambusho hasa. Ikiwa huna utambulisho, huwezi kuzungumza kwa sababu hujuhi hata wewe ni nani. Na ili mazungumzo yawe mazuri lazima yaanzie na utambulisho binafsi, wa kujijua na hivyo kuweza kuzungumza.
Mazungumzo, kukutana na safari huko Bahrain pia yalitendeka kati ya Wakristo, kwa mfano, Baba Mtakatifu amesema mkutano wa kwanza, kiukweli, ulikuwa wa kiekumene, wa sala ya amani, na Patriaki mpendwa na Ndugu Bartholomayo na kaka na dada wa madhdhebu mengune mbalimbali na ibada. Ilifanyika katika Kanisa Kuu, lililowekwa wakfu kwa Mama Yetu wa Arabia, ambapo jengo hilo linaibua hema, ambalo, kwa mujibu wa Biblia Takatifu, Mungu alikutana na Musa jangwani, katika safari ndefu. Kaka na dada katika imani, ambao alikutana nao huko Bahrain, kiukweli wanaishi katika safari wao kwa sehemu kubwa ni wafanykazi wahamiaji ambao, mbali na nyumbani kwao, wanasimika mizizi yao kwa Watu wa Mungu na familia zao katika familia kubwa ya Kanisa. Inapendeza kuona wahamiaji hao, Wafilipino, Wahindi na kwingineko, Wakristo wakikusanyika na kujiimarisha katika imani. Na hawa wanaendelea mbele kwa furaha, wakiwa na hakika kwamba tumaini la Mungu haliwakatishi tamaa (rej. Rum 5:5).
Kwa kukutana na Wachungaji, watawa kike na kiume, wahudumu wa kichungaji na katika Misa ya sikukuu na ya kusisimua iliyoadhimishwa uwanjani, waamini wengi, pia kutoka nchi nyingine za Ghuba, aliwapelekea upendo wa Kanisa zima. Hiyo ilikuwa safari, Papa alibainisha. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko amependelea kuelezea kwa wote furaha rahisi na nzuri. Kwa kukutana kwao na kusali pamoja, walihisi pamoja moyo mmoja na roho moja. Kwa kufikiria mchakato wao wa safari, uzoefu wao wa kila siku wa mazungumzo, amebainisha, kila mmoja alihis kuitwa kupanua upeo, na hivyo ameomba kupanua mioyo na sio kufungwa na kuwa migumu. Papa amesema Fungua mioyo yenu, kwa kuwa sisi sote ni ndugu na kwa udugu huo wa kibinadamu uende mbele zaidi. Panua upeo, uwazi, panua mambo yanayokuvutia na tujitolee kufahamiana na wengine. Ukijitolea kuwajua wengine, hutatishiwa kamwe. Lakini ikiwa unaogopa wengine, wewe mwenyewe utakuwa tishio kwao. Njia ya udugu na amani, ili kuendelea, inahitajika kwa kila mmoja. Mimi ninatoa mkono wangu, lakini ikiwa hakuna mkono mwingine kwa upande mwingine, haisaidii Mama yetu atusaidie katika safari hiyo! Papa amehitimisha.