Tafuta

2022.11.10 Papa kwa washiriki wa Kozi ya wakurugenzi na wafundaji wa Seminari kutoka Bara la Amerika Kusini. 2022.11.10 Papa kwa washiriki wa Kozi ya wakurugenzi na wafundaji wa Seminari kutoka Bara la Amerika Kusini. 

Papa kwa mapadre:Salini sana ili msiishie kwenye dampo la taka

Katika hotuba ya Papa Francisko bila kusoma kwa washiriki wa Kozi ya Wakurugenzi na Walezi wa Seminari Barani Amerika Kusini,alisisitiza ukaribu,huruma na upole kama tabia ya kuhani.Alishauri kufanya utambuzi vizuri wakati wa malezi na ikiwa mfundaji hana uwezo wa kutambua,anapaswa kumwambia askofu amtume mahali pengine.Onyo dhidi ya kutonyonyoa ngozi wenzao,kwa maana wote ni ndugu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Lazima kuwa na ukaribu, kwa sababu ni huzuni kuona mapadre ambao wanaongoza Parokia na wanapiga kelele au wale ambao kiurahisi wanaishi kama watatu au wanne katika nyumba ya kipadre  lakini hawajuhi kuzungumza kati yao. Ni kuwa na huruma kwa sababu ni mbaya kuona makuhani ambao hawana uwezo wa  kumbembeleza watoto, kubusu wazee au ambao ni wagumu kuelekea anayeomba msamaha wakati wa kuungama. Na zaidi lazima kusali zaidi kwa sababu kuhani ambaye atakuwa hivyo ataishia katika dampo la takataka. Ni mojawapo ya  maelezo ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Novemba 2022 aliyowambia wakurugenzi na walezi wa Seminari zote za Amerika Kusini, akiwapa mfano wa namna ambavyo Padre anatakiwa kuwa  yaani yule mwenye uwezo wa kukaribia, wa huruma na upendo, akibainisha lakini hata vikwazo na hatari ambazo zinaweza kujitokeza kama vishawishi.

Mara baada ya kuweka pembeni hotuba yake iliyokuwa ameandaa kurasa 12 na kuwakabidhi  wote ili kila mmoja ajisomee kwa utaratibu, Papa Francisko alipendelea kuzungumza moja kwa moja muda wote kwa lugha ya kispanyola na kusema kwamba anataka kubadilishana matatu au manne ya kile ambacho alihisi moyoni muda huo kwa ajili ya maisha yao, hasa kwa ajili ya maisha ya wafundaji katika seminari. Suala la kwanza alilokazia lilikuwa ni mwenendo na tabia mbele ya watu kwamba Hatuwezi kuwa na mapadre wanaoongoza parokia wakati ni wapaza sauti zao zote kwa ukali, wanaopakia kila kitu, wanaoishi kwa urahisi watu  watatu au wanne na hawajui kuongea au wasioweza kumbembeleza mtoto, kumbusu mzee au ambao hawaendi tu 'kupoteza angalau wakati' wa kuzungumza na wagonjwa, ndio  ni kupoteza wakati, lakini ambao uko kwenye mipango ya parokia na hayo yote. Hapana, hiyo sio nzuri, alibainisha.

Kutambua wakati wa malezi

Baba Fransisko alijikita katika  mada nyeti na changamoto ya malezi kwamba kipengele cha maisha ya kikuhani kimepitia mabadiliko kadhaa ya wakati kwa mfano  alikumbuka kuwa katika wakati wangu sote tulijumuishwa katika mfululizo, na malezi yalifanyika kwa mfululizo: 'Leo  hii ni hili, na hilo'. Na yule aliyedumu hadi mwisho aliwekwa wakfu  na wengine walianguka chini au waliondoka. Wakati huo makuhani wazuri waliweza kutoka namna hiyo, makuhani bora. Leo hii sio muktadha huo tena, kwa sababu ni zama nyingine, nyama nyingine, malighafi  nyingine. Kuna vijana wengine, wasiwasi mwingine; kwa hivyo, tuko hapo kuwafundisha vijana hawa. Baba Mtakatifu alibainisha kwamba majaribu huingia kwenye malezi  ambayo ni yale ya ugumu, yaani, wale vijana wote wanaokuja na mipango migumu ya mafunzo. Yameibuka mashirika ya kitawa ambayo ni maafa, ambayo yamelazimika kufungwa kidogo kidogo, mashirika yenye ugumu na kumbe isiwe hivyo,lakini nyuma ya ugumu  huo, kuna uozo halisi umefichwa. Papa alifichua

Yasitolewe majibu yaliyofungwa mapema

Kwa hiyo ni muhimu kutambua vizuri au kufanya maamuzi wakati wa malezi yote na jinsi ya kusindikiza vijana. Kama mfundaji  hana uwezo wa kupambanua kwa utambuzi, anapaswa kumwambia askofu wake: 'Sikiliza, nitume mahali pengine, sifai kwa hili', alisema Papa Francisko. Na maamuzi hayo yanahitaji ukimya,  sala, kusindikiza, yanahitaji uwezo wa kuteseka na kudhani kutokuwa na jibu tayari. Leo, hii majibu yaliyopangwa tayari hayafai kwa vijana; lazima tuwasindikize  na fundisho  lililo wazi, kwa hakika lakini lazima tuwasindikiza katika hali tofauti. Hata hivyo Papa Francisko katika hotuba yake hakukosa kutaja suala la kupungua kwa idadi ya miito na kusema kwamba “Ni tatizo la idadi ya waseminari, ambapo haiwezekani  kuwa na seminari yenye watu wanne, hapana. Utasikia wanasema hatuna zaidi. Unganeni ndio mwanzo na mwisho, aliwashuri.

Ukaribu na watu, mwenye huruma katika maungamo

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea alitoa pendekezo lingine  kwamba (Ni hali kama kichaa  niliyo nayo”, alisema mwenyewe) kuhusu ukaribu. Ambao hutafsiriwa kwa uthabiti katika kuzungumza na kutenda kwa mtindo wa Mungu, kwa hiyo ni kuwa na ukaribu. Hili lazima liwe la kuambukiza, yaani kuhani, mseminari, padre wote wawe karibu.  Karibu na nani? Na wasichana wa parokia? Papa aliuliza swali na kwamba  wengine wanaogopa kwamba labda baadhi yao wakiwa karibu baadaye wataoa. Lakini  je ukaribu na nani? Ukaribu vipi? Mungu yuko karibu na upendo na huruma. Na mambo haya matatu yanapaswa kutekelezwa kwa vijana. Ni lazima wawe makuhani wema, wenye upendo na zaidi wenye huruma. Hakika, kwa upande wake alisema jinsi ambavyo anaona uchungu kukutana na watu wanaokuja wanalia kwa sababu wameungama na kutokuelekezwa vizuri. Papa alisema, wakienda kuungama kwa sababu wamefanya kosa moja, mbili, elfu kumi... unamshukuru Mungu na kuwasamehe! Japokuwa kuna wengine wanasema,  lazima niombe ruhusa kwa askofu ...  Hii hutokea, lakini tafadhali,  Watu wetu hawawezi kuwa mikononi mwa wahalifu! Na kuhani anayefanya hivyo ni mhalifu katika kila neno. Upende usipende, Papa alifafanua.

Kusali  bila kukata tamaa

Papa akiendelea na hotuba yake alishauri wazi kwa mapadre wote ili wasali sana. Kuhani ambaye hasali huishia kwenye dampo la taka. Labda atavumilia hadi uzee, lakini kwenye pipa la vumbi, ambayo ni kuishi katika hali ya wastani. Simaanishi dhambi ya mauti, hapana, lakini  hali ya wastani, ambayo ni mbaya zaidi kuliko dhambi ya mauti. Kwa sababu dhambi ya mauti inakutisha na kwenda kuungama mara moja.  Ukiasi [Mediocrity] ni njia ya maisha, sio sana... Na unachukua faida ya kila kitu anachoweza na hivyo anavumilia hadi mwisho. Hapo ndipo padre asiyesali  anapoanguka. Kwa maana hiyo salini kwa umakini na waombe wale wanaowasindikiza kiroho wawafundishe jinsi ya kusali. Muwe na imani kwa jinsi mnavyasali pamoja na mwenzi wa kiroho. Tafadhali msikate tamaa kwa hilo.

Ukaribu na maaskofu kama watoto na baba yao

Baba Mtakatifu amebainisha kwamba Hatusali  kwa sababu ni lazima kusali bali kwa sababu ni lazima tujisikie hitaji la kuomba. Kadiri padre anavyojishughulisha zaidi, ndivyo anavyopaswa kupoteza muda katika maombi. Kwa maneno mengine, ukaribu na Bwana katika maombi unahitajika. Zaidi ya hayo, kuna maeneo matatu ambayo yalioneshwa na Baba Mtakatifu. Kwanza kabisa ule wa Askofu, ni ukaribu ambao hauwezi kujadiliwa. Hakuna Kanisa bila askofu. Yeye ni mnyonge. Wewe pia ni mnyonge. Kwa kifupi, kati ya bahati mbaya wataelewana. Lakini yeye ni baba yako. Na kama huna ujasiri wa kumwambia mambo usoni, husimwambie mtu mwingine, ukae kimya. Ama kwenda kwa askofu wako kama mwanamume, au umwombe Bwana kutatua tatizo. Lakini kuwa karibu naye, mtafute. Na askofu ndio lazima awe karibu na makuhani. Kwa hiyo uwe ni ukaribu kama watoto na sio kama walambaji miguu wanaojaribu kutaka kupata kitu. Na hii ina maana heshima.

Lakini mojawapo ya mambo ambayo hampaswi kamwe kujiruhusu kufanya ni kama ile ya wana wawili wa Nuhu ambao walicheka kwa sauti kubwa kwa baba yao mlevi. Badala yake fanyeni kama wa tatu kwenda na kumfunika. Ni kweli kwamba wakati mwingine wapo maaskofu huko ambao, Mungu apishe mbali... Naam, je utafanya nini mwanangu? Katika shamba la mizabibu la Bwana kuna kila kitu. Mfunike yeye ni baba yako. Uwe jasiri, zungumza naye, lakini usitumie nafasi hiyo ya  askofu ya mwili uliojeruhiwa na wenye dhambi ili kufurahiya kutoa maoni na wengine au kuhalalisha mambo yenu. Yeye ni baba yako."

Umakini dhidi ya  uvumi

Ukaribu sawa  na huo unatumika kati ya makuhani. Kwa maana hiyo makuhani wajihadhari na uvumi mojawapo ya tabia mbaya sana walizo nazo viongozi, alithibitishwa Baba Mtakatifu Francisko. “Sisi tuna masengenyo moyoni! tunachuna ngozi za wenzetu....ni ndugu zenu! ikiwa hamna suruali ya kusemea usoni, kuleni,  lakini hutamwambia mtu. vinginevyo kama majungu ya zamani!  Kuna majungu mengi  katika Kanisa, na kuna mengi sana kila mahali.  Majungu ya sifanyike kwa sababu hiyo yanaharibu maisha yetu, alisisitiza  Papa. Hatimaye  kwa maombi ya mwisho alisema kwamba unatakiwa ukaribu na watu wa Mungu. Kwa kuongeza alisema, Huwa ninaumia sana ninapo waona mapadre wakiwa wamekula wanga  yaani wenye mvi kiasi kwamba wamesahau watu mahali waliochukuliwa kutoka kwao. Kwa maana hiyo aliomba sana wasisahau washirika wao, kuwafundisha watoto kupenda kijiji, ambako wanatoka  na msisahau harufu ya watu wa Mungu.

Hotuba ya Papa bila kusoma kwa walezi wa seminari za Amerika Kusini
14 November 2022, 10:50