Vijana na watoto walimuaga Papa Francisko akiondoka
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ilikuwa ni mshangao wa Baba Mtakatifu kwa watoto mara baada ya kufika katika uwanja wa mpira wa “Censin Bosia” wa Asti, kabla ya kuondoka kurudi jijini Vatican ambapo Papa Francisko aliwatembelea watoto na vijana 1,340 wakiwakilisha maparokia na vituo vyao vya malezi katika jimbo la Asti.
Kitendo cha kumwona vijana walipaza sauti yao wakisema “tunamtaka Papa”. Wawili kati yao, ambao ni mapacha walimpelekea Papa hata maua ya njano na nyeupe na wengine michoro yao kama salamu kutoka kwao Asti. Mtoto ndogo mwingine alimkabidhi Baba Mtakatifu Jezi nyeupe na nyekundu ya kikundi cha Mpira cha Asti namba 10 iliyoandikwa jina Begoglio.
Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko alisindikizwa kwa nyimbo na vifijo kwa upande wa vijana katika kitengo cha Kichungaji na Kikundi cha Chama chaVijana wakatoliki cha Asti ambao kwa hakika waliweza kutumbuiza na kucheza.
Baba Mtakatifu Francisko kabla ya kupanda Elikopta yenye namba 500 L nyeupe aliwasalimia kikosi cha zima moto na wawahusika wa kutoa huduma za haraka na baadaye vijana waliendelea kupaza sauti wakisalimu “kwaheri Francisko”na hatimaye Papa alimkumbatia kwa kumuaga Askofu Marco Prastaro wa Jimbo katoliki la Asti. Elikopta ilifika mjini Vatican mida karibu saa 9.30 alasiri.