Tafuta

Ziara ya Kitume ya Papa Francisko Baharain,ushuhuda wa vijana

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Ni Shule ya Moyo Mtakatifu ya Awali, iliyo ya pekee katoliki nchini Bahrain, ndiyo  Baba Mtakatifu aliwasili katikati ya alasiri ya Jumamosi tarehe 5 Novemba 2022. Hata hiivyo kabla ya kwenda kwenye Taasisi hiyo, Baba Mtakatifu alikutana na ugeni wa Mtukufu Hamad bin Isa Al Khalifa, Mfalme wa Bahrain na ambapo aliweza kumshukuru kwa mapokezi makubwa aliyopewa na nchi yake.

Kabla ya Mkutano na Vijana Baba Mtakatifu alikutana na Mfalme wa Bahrain
Kabla ya Mkutano na Vijana Baba Mtakatifu alikutana na Mfalme wa Bahrain

Mkurugenzi Sr. Roselyn Thomas akimpokea Papa kwenye lango laShule ya Moyo Mtakatifu pamoja na walimu wawili na baadhi ya wanafunzi walimavalisha shada la maua. Na wakati huo Mkutano na vijana, wapatao 800 waliohudhuria, uliandaliwa katika ukumbi mkubwa wa mazoezi ya jengo hilo. Baada ya kufika katika taasisi hiyo  mapokezi yalikuwa yanajumuisha baadhi ya nyimbo, ngoma yenye mavazi ya kiutamaduni na shuhuda tatu. Kwa maana hiyo walikuwa na muda wa kukutana na kusherehekea na mgeni anayesubiriwa kwa muda mrefu, mwenye thamani zaidi katika historia ya miaka 74 ya shule hiyo kama alivyo sema Sista Roselyn Thomas, wakati wa kuwasilisha taasisi hiyo, ambayo wanafunzi na wafanyakazi wanatoka katika mataifa 29 tofauti na kuishi kwa pamoja  kama ishara ndogo ya kuishi pamoja kwa amani na utamaduni wa utunzaji.

Mkutano wa Vijana na Papa  huko Bahrain
Mkutano wa Vijana na Papa huko Bahrain

Mkurugenzi huyo kwa maana hiyo alimshukuru sana Baba Mtakatifu Francisko kwa huduma yake ya unyenyekevu kama mwongozo na alisisitizia furaha iliyoonekana ya watoto na vijana kwa uwepo wake  Papa na kwamna anao uhakika kuwa maneno yake ya hotuba yangeweza kuwatia moyo na nguvu ili waweze kuwa tumaini la mustakabali mzuri, raia hai ambao watafanya kazi ya kutengeneza ulimwengu kuwa mahali pazuri zaidi

Mkutano wa Vijana wa Shule ya Moyo Mtakatifu huko Bahrein
Mkutano wa Vijana wa Shule ya Moyo Mtakatifu huko Bahrein

Ushuhuda wa kwanza uliotolewa kwa Papa Francisko ulikuwa wa  Luteni Abdulla Attiya Sayed, mwanafunzi wa zamani wa Shule ya Moyo Mtakatifu na kwa sasa anahudumia  kama mshiriki wa Walinzi wa Kifalme wa Bahrain. Yeye alikulia katika familia ya Kiislamu na kusomea katika shule katoliki na maishani  alisema alijikuta akikabiliwa na changamoto nyingi. Kwa upande wake alisema, “Maisha yamenifanya nitambue kwamba kufanya kazi kwa bidii, kujitolea na kujitoa kunahitajika ili kufanikiwa. Katika miaka yangu 16 ya maisha ya kimichezo, nilipata mafanikio (...) lakini ninatambua na kukubali kwa unyenyekevu mkubwa kwamba medali na vikombe hatimaye vinapata kutu lakini kinachobaki zaidi ni  urafiki na udugu unaodumu milele”.

Mkutano wa Vijana na Papa  huko Bahrain
Mkutano wa Vijana na Papa huko Bahrain
Mkutano wa Vijana wa Shule ya Moyo Mtakatifu huko Bahrein
Mkutano wa Vijana wa Shule ya Moyo Mtakatifu huko Bahrein

Kwa upande wa ushuhuda wa Merina Joseph Motha ambaye alikulia katika mazingira ya Kikatoliki na sasa anajishughulisha na huduma ya Wahadhiri na  kama mhudumu wa usomaji wa masomo Kanisani na kama mwanakwaya wa parokia alisema kwamba, Nilikuwa na bahati ya kuwa na familia nzuri, nyumba nzuri na vipaji vingi kutoka kwa Bwana. Zaidi yahayo, jumuiya ilihisi kuhimizwa sio tu kufuata njia za Mungu, lakini pia kugundua mimi ni nani na ninaweza kuwa nini katika ulimwengu huu. Pamoja na ujana, hata hivyo, kulikuwa na mabadiliko kwani kuwa kijana inamaanisha kuingia katika awamu ya maisha ambayo inahusisha uzoefu mwingi usiojulikana. Katika umri huo unahitaji mwongozo, kutembea pamoja na wengine, lakini matukio mengine hayawezi kudhibitiwa, alisema. Kwa njia hiyo tunaweza kupoteza vipaumbele, kuanguka katika utamaduni wa kutojali, na kuanza kujichukia sisi wenyewe na wale walio karibu nasi na hata kusahau mizizi yetu wenyewe. Kwa hiyo ni muhimu kufanya maamuzi, si kubebwa na hisia na kuimarisha imani.

Mkutano wa Vijana na Papa  huko Bahrain
Mkutano wa Vijana na Papa huko Bahrain
05 November 2022, 18:30